Busara kidogo zinahitajika hapa

Busara kidogo zinahitajika hapa

Peculiar

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2015
Posts
821
Reaction score
689
Wakuu,
Jamaa yangu mchumba wake kaposwa, na mchumba wa jamaa kakubali ndoa.

Ameniomba ushauri,nimemwambia akubali tu matokeo hataki ushauri huu kwa sasa, anachotaka yeye ni kujua namna gani anaweza akapindua matokeo.

Nikajaribu kumuuliza, binti nampenda nani zaidi kati yake na alitoa posa,akasema binti kamwambia ukweli kuwa wote walimtongoza, ila huyo aliyetoa posa hakumkubali wala kumkataa, kashtuka tu kaitwa kupewa taarifa za posa yake,akashindwa kukataa mbele ya kikao,binti akakubali, hivyo barua ya mahari ikajibiwa ila bado haijalipwa. Na binti anapenda zaidi kufanya maisha na yeye kuliko huyo aliyetoa posa.

Nikamuuliza sasa wewe unatakaje ilhali unaona mtu ashakubali, akasema anataka kujua kama akipeleka yeye posa yake itasikilizwa au ndio wa kwanza atapewa kipaumbele zaidi,anasema binti yupo dilemma, nampenda yeye na anajutia kukubali.

Mi navyoona ni kama hana chake tayari, ila sikutaka kumvunja moyo, nikamwambia poa ngoja tuulizie wazoefu wa mambo tuone inakaaje hii.
Akajibu poa, nakutegemea bro.

Nimeona niilete hapa nipate machache, maana binafsi posa juu ya posa sijawahi i-experience!

Karibuni wakuu
IMG_20180506_074740.jpg
 
Ngoja niwe first halaf ntakupa ushauri kias
 
Mwambie apeleke vyote (Posa, mahali na tarehe ya kumchukua Dija) kwa siku moja
 
Wazaz

Hawa hawana lawama,maana aidha hawajui mahusiano ya mtoto wao,na jamaa labda japo hatufaham alishaenda kutambulishwa kwao au lah japo kwa jicho la tatu inaonekana hawajawah kwenda kwa wazaz wa mwanamke..na hapa lazima tuangalie kwa ukarib zaid kama jamaa wako alishakwenda kwa mzaz wa mwanamke na wakafahamiana lazima kuna walakin mkubwa,,hapa watavaa lawama cz wanajua kwamba binti yao ana mahusiano na mshkaji wako,,pia unaweza kuona kama wazaz wanamjua kijana mwenzako na wakakubali kupokea posa nyingind ni waz hawamtaki mshkaji wako.

Msichana

Yeye ndo anaishukilia ndoa,anajua anampenda nan,na mahusiano yake na mshkaji wako labda hayakua serious sana kias jamaa katokea tu huko kaamua kuwavaa wazaz na wazaz wakaona poa tu,ila pia hapa naweza mlaum kidgo huyu dada,kama hampend na kwa nn kakubali,kama anaanza kufuga tatzo huko mbelen unategemea nn? Ameshindwaje kumwambia mama au baba yake kwamba yy ana mtu anaemoenda kwa hyo posa wasipokee,? Labda anawaheshim na kuwaogopa sana wazaz bt je ndo wakuamulie maisha yako ya ndoa? Kwa nn kakubali? Kaogopa nn? Je hao wazaz wa huyo aliekubaliwa posa wana uhusiano kias gan na wazaz wa mwanamke? Hapa mwanamke kaamua sio kwa bahat mbaya,ameitwa kaulizwa na kakubali ss anasemaje tena aliogopa kukataa ilihal kashakubali?

Jamaa wako

Wamedum kwa muda gan?walipanga nn? Kwa nn jamaa hakupewa taarifa mapema kwamba kuna mtu anataka kutoa posa? Unadhan mwanamke hakujua? Au unadhan huyu dada hamjui huyo mtu? Lazima wanajuana na anaonekana yupo serious kuliko mshkaji wako,so nae analawama japo sio sana kama mwanamke..

Nini afanye? Atulie,akae na yule mwanamke,amuulize toka koyon yy anaamuaje,maana mahusiano yyte yabashikiliwa na mwanamke,ukwel wake ndo itakua suluhisho pekee kwa jamaa yako,ila sidhan kama wazaz wenye uelewa wanaweza pokea posa mbili,hata kama bado posa haijapokelewa ile ya awali,,na akiona mwanamke anamwambia kwamba anaogopa kuwakwaza wazaz wake bas amuache kwa amani,wala asi mind,maana mungu kamwinyesha rangi halis mapema kabla ya ndoa,mpe pole mwambie subira yavuta heri ila ngoja ngoja huumiza matumbo[emoji12] [emoji12] [emoji12] [emoji12]
 
Maamuzi anayo mwanamke...

Kama amekubali inaamana kaona jamaa anampotezea muda haeleweki...

Jamaa anashtuka kuvuta shuka wakati tayari kushakucha...


Cc: mahondaw
 
Ngoja niwe first halaf ntakupa ushauri kias
umeongea vema mkuu,

Labda kwa maswali yako,
Uhusiano wao una karibia mwaka.

Anavyodai walipanga mengi, na alimuahidi mwezi wa sita haufiki wataonekana kwao.

Ila mbaya ilomgharimu jamaa, ni alipotea kidogo, akaingia machimbo kuzitafuta,na alimuaga anavyodai, Mawasiliano na binti yakawa chini kidogo alipokua huko, ila kwa sasa alivyorudi wameendelea kuwasiliana/kuonana vizuri tu,na binti ndio kamwambia yote hayo.

Pia nimemshauri aachane naye kwa amani kama unavyosema, yeye anataka kupambana,hataki kukubali kuwa Kapinduliwa.

Nimepata neno la kumwambia kutoka katika mchango wako. Be blessed
 
eti "hakumkubali wala hakumkataa" nashindwa kuelewa maana yake kwahyo ni staki nataka au, kwanini asiwe na jibu moja.
Usimwamini mwanamke anaelialia au mbwa anaechechemea.
 
Maamuzi anayo mwanamke...

Kama amekubali inaamana kaona jamaa anampotezea muda haeleweki...

Jamaa anashtuka kuvuta shuka wakati tayari kushakucha...


Cc: mahondaw
Na huo ndio ukweli, ambao jamaa nimemwabia kagoma kumeza ili apone kisa mchungu.

Kuna mkuu Katoa wazo sasa sijui kama linawezekana, sijui, nitalichukua na kumfikishia machache nitayaokota hapa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom