Busara iliyotumiwa kwa Samuel Sitta, ndiyo itatumika kwa Edward Lowassa?.

Naomba utambue kuwa Kikwete kama Mwenyekiti wa CCM hana mamlaka ya kusema nani akose wala nani apate, na mbaya zaidi CCM haiongozwi na maamuzi ya mtu mmoja mmoja bali vikao vya chama.

Halafu Membe ni zaidi.ya fisadi asiyetakiwa katika nchi hii, mfano mzuri ni pale anaposhutumiwa na Waislamu wenzake kula fedha zao,

Na uelewe pia kuwa LOWASSA ni mtu asiyefananishwa na mgombea yeyote ndani na nje ya CCM
Ni kweli Kikwete hana Mamlaka hayo ndo maana naye alikatwa 1995
Lowasa hafanani na hao Wagombea kwa kuwa ni Mwizi na amewazidi wenzake kuiba ijapo wote ni wezi
 
Ni wananchi .. Rais Kikwete akisema kwa sasa nafasi ya Rais wa Tanzania ni kwa Wazanzibari.
yafanyike yote kama chukua Lowasa na Membe tupa huko lakini si kusema nafasi ya sasa ni ya Zanzibar...hapa ndipo utakapo sikia CCM wamegeuka Chama Cha UPINZANI tu wanapomaliza kulitaja jina la mgombea wao toka Zanzibar.

Manake kuna kosa moja kubwa ambalo kwa wenye akili zao wamelifumbia macho...na muda wake wa kusahihisha ni sasa na kitendo tu cha kuwaza mtu toka Zenj ni kukaribisha hatari isiyofikilika kwenye vichwa vya watu makini.Kulikuwa na Serikali mbili Nchi moja...leo ni.....Nchi Mbili...Sasa kama haya yalishasikia dhahiri..basi HATEGEMEKI hata kidogo!!!eti kuna swala la Uzanzibar hapo kukwaa kiti cha Urais yani ukisikia CCM ikiaga IKULU rasmi ni siku wanataja jina la Mgombea huyo...kwa kuwa NAAMINI hakuna Kiongozi yoyote anaweza kulifilia hilo hata japo kulisogelea.

Bila kusahau JADI yetu...ambayo ipo siku zote leo ni kesho ni...yani AUTOMATICALLY ...sasa huyo atakae simama na kuanzisha hilo basi ATAKUWA ameamua KUKIUA chama chake mwenyewe na UKAWA kiulaini wataanza kuhesabu makabati na viti vya Ikulu.Kuna watu wengi sana potential kukalia kiti hicho cha CCM toka Tanganyika aka Tanzania Bara uitaji kukumbuka kovu ambalo watu wanatafuta cream ya kulainisha ngozi kovu lipotee.
 
Jambo linguine LA kheri wangewapitisha Lowassa na Membe waende kwenye NEC (5 bora) wanachama waamue, atakayeshindwa kupenya pale afahamu kuwa amekataliwa na wenye Chama. Hapa Chama kinaweza kubaki usalama.

Na atakaye leta chokochoko apewe onya kali ikiwa na kufukzwa Hana Chama. Wenye maamuzi kwenye Chama wakishaamua MTU mwenye hila atakosa hoja
 
Ukitaka kuuongelea ubaya wa mtu jaribu kuuwekawwazi na thibitisha, usiandike usichofahamu maana sisi wachambuzi tutakushangaa....ukimtoa Lowassa sasa hivi ni nani mwingine mwenye ushawishi na mvuto kwa wananchi? Jibu ni HAKUNA Lowassa is the selling brand popote anapopita lazima umati uzizime na umlaki tena kwa sauti zenye matumaini na matarajio..Rais...rais...rais...rais...sasa leo umsimamishe nani zaidi yake?..Lowassa ndio jibulla Watanzania kwa sasa...ENL 2015

Unajitekenya alaf unacheka!
 
Watanzania tunapotafakari umati wa watu wanaofurika kwa fisadi mamvi lazima pia tukumbuke huko nyuma, baada ya kujiuzuru mwaka 2008 huyu Mh Mamvi alikuwa anafanya nini. Mamvi kampeni hakuanza sasa.... Mamvi alianza mara baada ya kung'olewa u pm 2008! Alianza kimya kimya makanisani, misikitini, bodaboda kila kona ya nchi anamwaga pesa Na kuandaa makuwadi wake ambao watamfanyia kaz ya kumsafisa aonekane Ni lulu! Ndio maana wanaosema anawanunua watu hawakosei! Hafai kuwa Rais wa Tanzania.
 
Jambo linguine LA kheri wangewapitisha Lowassa na Membe waende kwenye NEC (5 bora) wanachama waamue, atakayeshindwa kupenya pale afahamu kuwa amekataliwa na wenye Chama. Hapa Chama kinaweza kubaki usalama.

Na atakaye leta chokochoko apewe onya kali ikiwa na kufukzwa Hana Chama. Wenye maamuzi kwenye Chama wakishaamua MTU mwenye hila atakosa hoja

Hapana. CC iwafyeke tu wote BM Na Mamvi. Hawastahili kuingia 5bora.
 
Wakati ule Six akivuma kwa Standard and Speed huku akionekana kukubalika hata na wapinzani lakini wakati huo huo akionesha kuikera CCM akagombea tena baada ya awamu ya kwanza kuisha na huku akionekana ndiye mgombea aliyekuwa mwenye uhakika wa kushinda.

Kwakuwa chama kilishaona ameshindwa kukipendelea hasa katika ule mjadala wa richmond, alipogombea mara ya pili kilimwacha apite mpaka hatua za mwisho lakini kwenye kupitisha jina moja kikaja na mbinu ya kumwengua kimtindo kwa kutangaza kuwa wakati huo ulikuwa ni wa wanawake hivyo wanaume wawapishe wanawake. Hivyo ndio ukawa mwisho wa viwango na kasi. Angelalamika nini wakati yeye sio mwanamke?

Wakati huu tena tunapoelekea uchaguzi mkuu mchezo unaelekea kujirudia tena. Wanawake wanne wametia nia lakini mtifuano mkubwa uko kwa wanaume wengine wakijiapiza kuwa bila wao hakuna Tanzania.

Kiona mbali changu kinaniambia kuwa wanaume wote watalizwa kwa kigezo kuwa "sasa umefika wakati wa kuwa na rais mwanamke Tanzania hivyo wanaume wawapishe wanawake" Kama kuna atakayetokea kutokuridhika itabidi akabadili jinsia yake ili aruhusiwe kugombea na wanawake "wenzake" vinginevyo imekula kwao.

Ndipo hapo waliomwaga mabilioni ya kununua watu ili waende wakawabembeleze eti kugombea watakapo tamani kuwa ni heri wangetumia mabilioni hayo kujibadilisha jinsia ili wapate nafasi ya kupambana na wanawake wenzao lakini wakati maamuzi yakipitishwa watakuwa wamechelewa.

Wataachwa vinywa wazi. Mama aliyekuwa msaidizi wa Bani kini muni kesha ingia na usishangae ni mkakati tu wa kuwaweka wale wengine ili wamsindikize kama ilivyo kuwa kwa Anna wakati wa uspika.

Tatizo linaweza kuwa anatokea kaskazini kwani wagombea kutoka kaskazini iwe wa upinzani au wa chama twawala wanaonekana kupigwa vita sana na hata kajumuia ka chama kalishaweka msimamo kuwa rais hatatoka kaskazini.

Tatizo la chama chetu ni kuwa viongozi wa upinzani wakitoka kaskazini eti huo ni ukanda, wa kwake chenyewe hawasemi ni ukanda. Sasa timu kubwa ya wagombea inatoka kaskazini sijui watafanyaje?

Tuisubiri hiyo siku.
 
Miezi 4 kabla ya Uchaguzi Wa Tanzania mpaka sasa tunajadili vigezo vya hovyo sana, tunajadili Mgombea Urais kama vile tunajadili mgombea U miss
 
Urais na uspika wa bunge ni vitu tofauti, spika anaongoza watu wanaoitwa waheshimiwa huku rais anaongoza Tanaka la watu wa kila aina ....

Pia kumfananisha Membe aka Bakary na Lowassa ni vitu viwili tofauti.. Membe kajiunga ccm 2003,, Lowassa kajiunga ccm 1975
kuna Mtu ameitwa BAKARY NI NANI?NA NI KWELI KUNA MGOMBEA ANAITWA BAKARY? MBONA WANANCHI WENGI HATUJUI/
NA TUTAJUAJE?
 
ni wananchi wachache waliotegemea mwaka 2010 kama samuel sitta angeweza kuwekwa kando na ccm kama mgombea uspika kwa tiketi ya ccm.

Makundi yaliyojitokeza ndani ya ccm ambayo msingi wake ulikuwa ni hoja ya ufisadi yalipelekea jina la samuel sitta kuwekwa kapuni kwa kisingizio cha zamu ya wanawake. Hii ilikuja baada ya andrew chenge kujitokeza kutaka kugombea uspika kwa tiketi ya ccm huku akidai uongozi wa spika sitta ulikuwa wa kinafiki, majungu, uzandiki na kila aina ya mbinu za kuwapaka watu matope kwa lengo la kujijengea umaarufu binafsi huku ukiathiri kwa kiwango kikubwa utendaji wa serikali ya ccm.

samuel sitta alikuwa ni kiwakilishi kwenye kundi lililokuwa linadai kupambana na mafisadi ndani ya ccm, wakati huo huo, andrew chenge alikuwa anawakilisha kundi lililokuwa linadaiwa ni mafisadi ndani ya ccm.

kwa kuepuka mpasuko uliokuwa unainyemelea ccm, busara kidogo ndani ya ccm ilitumika kuzima mpasuko huo kwa njia ya wakose wote kwa kuyaweka kapuni majina ya samuel sitta na andrew chenge kwa madai eti kwa sasa ni muda wa kuwapa nafasi wanawake.

Mbinu ya wakose wote haikuanzia kwa samuel sitta, mwaka 2008, tulishuhudia mbinu ya wakose wote kutoka kwa mwenyekiti wa ccm-taifa, rais kikwete baada ya umoja wa vijana wa ccm kugawanyika katika makundi ambayo yalikuwa yanahatarisha umoja huo. Maajenti wa makundi katika pande mbili walienguliwa ili wakose wote.

miaka mitano baadaye, makundi haya yameibuka tena ndani ya ccm kwa kumtumia edward lowassa kama kiwakilishi cha kundi linalodai linafanyiwa fitna na kuonewa wivu ndani ya ccm na kundi lingine linalomtumia bernard membe kama kiwakilishi cha kundi linalopambana ufisadi.

ccm kwa sasa iko njia panda katika kutoa maamuzi hasa ikichukuliwa mwenyekiti wa ccm taifa, rais kikwete ni kama kinyonga. Ni kiongozi anayebadilika na kutoa maamuzi ya kisiasa kulingana na upepo wa kisiasa.

ccm ya sasa imegawanyika kwa kiwango kikubwa kuhusu edward lowassa na bernard membe katika mchakato wa ugombea urais kiasi kwamba, maamuzi yoyote yatakayomnufaisha mmoja kati ya edward lowassa na bernard membe kuna uwezekano mkubwa yataiacha ccm katika makovu yasiyo na tiba ya kisiasa.

ccm ya sasa imechoka, inavuja damu nyingi ya kisiasa na imedhoofishwa sana na watu kama edward lowassa na bernard membe. Ccm ya sasa haiwezi kusema fulani ana makosa na fulani hana makosa. njia rahisi ni kuwafanya wakose wote.

Je, yaliyowatokea andrew chenge na samuel sitta kwenye kiny’ang’anyilo cha uspika wa bunge la tanzania ndiyo yatakayowatokea edward lowass
a na bernard membe katika mbio za kuwania urais wa tanzania ili kuinusuru ccm?.

kwa yale yanaendelea ndani ya ccm, sitashangaa nikisikia kauli ya mwenyekiti wa ccm-taifa, rais kikwete akisema kwa sasa nafasi ya rais wa tanzania ni kwa wazanzibari.

ha! Atoke zanzibar alafu apabne na nani? Ukawa???
 
Mazingira yako tofauti sana katika kufananisha. Kwa haraka tunaweza kusema Sitta aliitia doa CCM wakati ule na ikakikosesha chama kura, pili mama aliwekwa ili kuendeleza ubabe wa kundi la wenye pesa na kuwasafisha mbele ya umma huku serikali ikipumua na katika kufanya hili kulichochea ghiriba,chuki na makundi mno tofauti labda na ilivyokusudiwa na chama. Nasema hivi kwasababu kwanza serikali haikuwahi kutulia na ndo maana tunaona toka 2010 mawaziri wamebadilshwa mara 3 kufuatia kashfa ambazo nyingi zimechochewa na uhasama wa toka 2008 , lakini pia makundi yamezidi kuwa dhairi na yakiongozwa na uhasama wa hatari. Sasa leo ni mazingira ya kukinusuru chama kising'olewe madarakani huku upinzani chini ya Ukawa ukiwa kwenye peak, kwahiyo kwasahivi si tu kupata mtu wa kuneutrlise makundi bali pia ni kumpeleka mtu wa kuishinda nguvu ya Ukawa na kichama mtu ambaye ataweza kuirudisha CCM katika uongozi wa kimaadili ili kiwe na uhakika hata kwa uchaguzi wa 2020.
 
1.Ni zamu ya Zanzibar-Lowasa......................................!!!!!!!!!!!!!!!!!!!??????????????????
2.Ni zamu ya wanawake-Migiro........................................!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!?????????????????????????
 
Mazingira yako tofauti sana katika kufananisha. Kwa haraka tunaweza kusema Sitta aliitia doa CCM wakati ule na ikakikosesha chama kura, pili mama aliwekwa ili kuendeleza ubabe wa kundi la wenye pesa na kuwasafisha mbele ya umma huku serikali ikipumua na katika kufanya hili kulichochea ghiriba,chuki na makundi mno tofauti labda na ilivyokusudiwa na chama. Nasema hivi kwasababu kwanza serikali haikuwahi kutulia na ndo maana tunaona toka 2010 mawaziri wamebadilshwa mara 3 kufuatia kashfa ambazo nyingi zimechochewa na uhasama wa toka 2008 , lakini pia makundi yamezidi kuwa dhairi na yakiongozwa na uhasama wa hatari. Sasa leo ni mazingira ya kukinusuru chama kising'olewe madarakani huku upinzani chini ya Ukawa ukiwa kwenye peak, kwahiyo kwasahivi si tu kupata mtu wa kuneutrlise makundi bali pia ni kumpeleka mtu wa kuishinda nguvu ya Ukawa na kichama mtu ambaye ataweza kuirudisha CCM katika uongozi wa kimaadili ili kiwe na uhakika hata kwa uchaguzi wa 2020.

Good analysis mkuu, na kwa maoni yangu mtu pekee wa ku-neutralize haya makundi at the same time akimudu kushinda nguvu ya ukawa ni Makongoro Nyerere
 
yafanyike yote kama chukua Lowasa na Membe tupa huko lakini si kusema nafasi ya sasa ni ya Zanzibar...hapa ndipo utakapo sikia CCM wamegeuka Chama Cha UPINZANI tu wanapomaliza kulitaja jina la mgombea wao toka Zanzibar.

Manake kuna kosa moja kubwa ambalo kwa wenye akili zao wamelifumbia macho...na muda wake wa kusahihisha ni sasa na kitendo tu cha kuwaza mtu toka Zenj ni kukaribisha hatari isiyofikilika kwenye vichwa vya watu makini.Kulikuwa na Serikali mbili Nchi moja...leo ni.....Nchi Mbili...Sasa kama haya yalishasikia dhahiri..basi HATEGEMEKI hata kidogo!!!eti kuna swala la Uzanzibar hapo kukwaa kiti cha Urais yani ukisikia CCM ikiaga IKULU rasmi ni siku wanataja jina la Mgombea huyo...kwa kuwa NAAMINI hakuna Kiongozi yoyote anaweza kulifilia hilo hata japo kulisogelea.

Bila kusahau JADI yetu...ambayo ipo siku zote leo ni kesho ni...yani AUTOMATICALLY ...sasa huyo atakae simama na kuanzisha hilo basi ATAKUWA ameamua KUKIUA chama chake mwenyewe na UKAWA kiulaini wataanza kuhesabu makabati na viti vya Ikulu.Kuna watu wengi sana potential kukalia kiti hicho cha CCM toka Tanganyika aka Tanzania Bara uitaji kukumbuka kovu ambalo watu wanatafuta cream ya kulainisha ngozi kovu lipotee.
Mkuu DSN;

Unataka kusema kwa sasa hakuna nafasi ya Mzanzibari kuteuliwa kuwa mgombea Urais kupitia CCM?.
 
Miezi 4 kabla ya Uchaguzi Wa Tanzania mpaka sasa tunajadili vigezo vya hovyo sana, tunajadili Mgombea Urais kama vile tunajadili mgombea U miss

Mkuu usiwe unasoma kila mada huku! Nyingine ziache, zina wenyewe. Tafuta mada ambazo unafiti then toa mchango wako! Huo ndo ukomavu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom