Bus la Maning nice linanyanyasa abiria

bora mmesema humu sitapanda hili basi tena. Sio rafiki wa watoto na jamii kumbe. Unazuia godoro mwanafunzi akalale wapi? Na ametoka mbali na nyumbani sababu ya pesa kidogo? Hivi wangelrihusu aende si ingekuwa social corporate responsibility?
 
bora mmesema humu sitapanda hili basi tena. Sio rafiki wa watoto na jamii kumbe. Unazuia godoro mwanafunzi akalale wapi? Na ametoka mbali na nyumbani sababu ya pesa kidogo? Hivi wangelrihusu aende si ingekuwa social corporate responsibility?
Naunga mkono hoja, ikitokea nasafiri njia ambayo hilo basi linafanya safari zake silipandi
 
Na nyie abiria wengine (mleta uzi ukiwa mmoja wao) mlichukua hatua gani kuzuia unyanyasaji huo? Maamuzi ya kuikalia kimya dhuluma ni sehemu ya ushiriki wako. Ni wakati sasa watanzania tusimame na kujitetea/kuteteana, imagine binti mdogo wa shule anapambana na wanaume wanne halafu kuna mwanaume na misuli yake au mwanamke na nguvu zake amekaa tu anasubiri afike nyumbani awasimulie majirani wasikitike na kuhuzunika
 
Nadhani hao wajinga( Kondakta) wanajisahau kuwa huu ni utawala wa mama..utawala wa kunyanyasa watu na kuwaita wanyonge ulikwisha..
 
Mimi kama mpita njia nilijaribu kupiga picha tiketi ya huyo mwanafunzi na kuituma kwa trafiki kibaha na pia kutoa taarifa kwa afisa wa LATRA Morogoro 0738 000 054

Sent from my SM-N920S using JamiiForums mobile app
 
Kwelikabisa wakatoe taarifa mapema atasaidiwa bila ya shida kabisa.
 
Statement yako ya mwisho imenichekesha na kunipa mawazo.
 
Bei ya elfu kumi kwa ilo godoro ni sahihi labda tu uyu mwanafunzi akuambiwa bei mapema.
Sitakaa nije nitetee mbwa hao, makondakta nimekumbana nao katika mazingira tofauti tofauti wakaninyanyasa sana

Tukio la huyo dada naliona kama copy and paste kasoro install tu na nilichofanyiwa mwaka jana kwenye gari ya mkulima.

Makondakta idadi hiyohiyo (midume kama mimi) yaling'ang'ania betri yangu ya sola eti yakaondoka nayo kisa yanadai nauli na mimi kwa hasira nikayaacha yakazunguka nayo siku tatu ndipo siku nipo kwenye mambo yangu nikaiona gari nikaifwata nikaichukua betri yangu bureeee.

Nilifurahi lakini nilichukia kidogo kwakuwa nilichokuwa nimedhamiria ni betri ipotee nikawashtaki niwasumbue kidogo

Basi mpaka leo siwapendi hao jamaa halafu nakutana nao bado japo wenyewe wamenisahau ila mimi nawakumbuka na nategea siku mmojawapo ajiingize kwenye anga zangu au ajilete ana shida fulani ndo atajua hajui

Mtu anaweza akasema mimi mgumu au sijui nini lakini sivyo ngoja nirewind hii stori utaelewa. Nilinunua vitu kadhaa wabebaji wakapakia kwenye keriya juu huko nikaongea na huyo mkuu wao nikamuorodheshea vitu nilivyonavyo akasema nilipe elfu 10 nikalipa

Kisha nikachukua kimzigo changu kingine na betri nikaingia nayo ndani sasa pale wakawa wananizuia wanasema ikapandishwe juu nikalazimisha nikaingia navyo. Wakasumbua sana mule ndani wanasema betri ni kitu hatari hivyo huwa wanashika hela kubwa nilipe elfu 15 nyingine kwajili ya betri tu ikabidi nimuite yule mkuu wao akawaambia waniache elfu kumi niliyolipa inatosha

Basi wakaambiana sawa, sawa kumbe vile wamekonyezana. Yule bwana akanipa namba yake akasema nimpigie kwa lolote (aliwaelewa mapema). Basi kufika nishuke sasa ndipo hapo utata ulipoanzia

Nilimpigia yule jamaa akaniambia hiyo betri wataacha ofisini nikachukue hawakuacha wakarudi nayo Dar ndipo nikaamua kuwaacha wazurure nayo. Sijui aliwachukulia hatua gani lakini alionesha kukasirika sana wale wajamaa kumdharau na akasema lazima awashughulikie
 
Mabasi ya kusini yana upumbavu mwingi sana.....yaani ukiweka hata kibox kwenye gari wanataka ulipie cha ajabu anayedai hiyo nauli ni kondakta lakini kwenye kukata tiketi huulizwi kuhusu mizigo.......hao ni MATAPELI.....

Hii niliishuhudia Tashrif bus na Maning nice
 
Hiyo njia bus langu ni Baraka classic huwezi nitoa wana mabasi mazuri siti nzuri na wasikivu kwa abiria
 
Hawa mabwana Ni wasumbufu Sana nilifikiri Ni Mimi kumbe Kuna wengi wametatizwa nao. Niliapa sitapanda Wala kutuma mzigo wangu kwao kwa usumbufu nilioupata. Hivi mmiliki Ni Mwenye asili ya Somali?
 
Kusini hata sanduku la nguo unalipia
 
Poleni.

Login • Instagram
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…