Burudani na mazoezi karne 21

Burudani na mazoezi karne 21

Alex Moshi

New Member
Joined
Jul 21, 2021
Posts
1
Reaction score
0
Burudani na mazoezi yamekuwa na umuhimu mkubwa katika karne hii. Viongozi katika nchi nyingi wamekuwa wakijaribu katika kuhimiza wananchi wao katika swala zima la kufanya mazoezi.

Kuwepo na majanga mengi na maswala mengi muhimu yamewafanya watu wengi kusahau pia mazoezi na burudani katika maisha haya yamekuwa na nafasi kubwa. Nakala nyingi katika kurasa,vitabu na magazeti mengi kumekuwa na majadiliano mengi ya maswala kama COVID-19 na Uchumi kupanda au kushuka ila ni watu wachache wamejaribu kuongelea umuhimu wa kuwepo na mazoezi na burudani kama vile mziki wafanyao wasanii wetu kama Diamond platnumz, Alikiba, Nandy na wengine wengi.

Mimi ni miongoni mwa watu wenye kukumbana na changamoto nyingi katika maisha ila nimekuwa nikijiliwaza na burudani mara kwa mara lengo likiwa ni kuweka akili yangu vizuri na kuendelea na shughuli zangu za kila siku.

Kwa kumalizia na hili ni vyema kufanya mazoezi kuepukana na magonjwa mbalimbali na kuimarisha afya zetu.
 
Back
Top Bottom