Burkina Faso yapata rais wa mpito

Burkina Faso yapata rais wa mpito

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
8,269
Reaction score
25,308
141117082239_burknafaso_president_512x288_bbc_nocredit.jpg

Rais wa mpito wa Burkina Faso Michel Kafando

Aliyekuwa waziri wa mambo ya nje Burkina Faso Michel Kafando, ametajwa kuwa rais wa mpito nchini humo.
Jitihada zimekuwa zikiendelea nchini humo kumchagua kiongozi wa mpito kufuatia kuidhinishwa hapo jana na jeshi na viongozi wa mashirika ya kiraia kwa mpango wa mwaka mzima utakaohakikisha kufanyika uchaguzi.

Kafando alikuwa mmoja kati ya watu wanne ambao wangechukua wadhifa huo, wakiwemo waandishi wawili na msomi mmoja.
Viongozi wa mashirika ya kiraia na wawakilishi wa jeshi walishughulika hadi usiku katika mji wa Ouagadougou kuamua nani atachukua wadhifa huo wa rais wa mpito.

Kwa mujibu wa makubaliano hayo ya mpito, ilikuwa ni lazima awe raia ambaye hatogombea katika uchaguzi huo.
Mwishowe walimchagua raia aliyependwa zaidi na jeshi, mwenye umri wa miaka 72 na waziri wa mambo ya nje wa zamani Michel Kafando, Sasa ni lazima amchague waziri mkuu ambaye anaweza kuwa raia au afisa wa jeshi kuongoza serikali ya watu 25 ya mpito.

Chanzo: BBC Swahili
 
Hongera zao. Na sisi tunakusanya nguvu hadi kieleweke maana waliopo wanatuzingua tuuuu
 
Inaonekana huyu jamaa alikuwa memba mzuri ya klabu ya gongo maana lips zake ni balaa.
 
Hata hapa Bongo kwa hali ilipofikia tinahitaji mpango huu ili tupate Rais mpya.
 
Back
Top Bottom