Bwana Mapesa
JF-Expert Member
- Apr 28, 2011
- 2,551
- 1,777
Huyu alikuwa mlezi kwangu, ndiye aliyenitafutia shule wakati namaliza O level ili nianze safari ya kwenda advance level(alikuwa rafiki wa baba yangu mzazi na walishirikiana mengi pamoja na suala la elimu yangu) . Nilimjua kama msomi mwanasheria ambaye alikuwa mzoefu katika uongozi wa umma watu wa mbeya na kwingine alipopita wanaweza shuhudia hili (ingawa hakuna aliyekamilika mapungufu yanaweza kuwepo kwani ndo sifa ya kila mwanadamu). Niwe mkweli niliumia sana kusikia mkuu wa mkoa akimtaja kama mtu wa hovyo asiyeweza fanya nae Kazi pale kigamboni siku ya uzinduzi wa daraja la NYERERE. Niliumia zaidi sababu nilijua kuwa wakati ule marehemu alikuwa na hali mbaya kitandani nchini India. Siamini kama mkuu wa mkoa hakulitambua hili. Lakini katika kujiona msafi, mcha mungu akaamua kumpiga jiwe maiti, kwa hili nashindwa kuamini kama Makonda kweli ni mcha mungu, sababu kwa mtu yoyote mcha mungu asingeweza kuyafanya yale wakati anajua fika mzee Kabwe alikuwa kitandani. Hayo yamepita lakini imeniuma zaidi kuona mtu aliyepata sifuri O level na anayetumia vyeti sio vyake kumkataa mtu msomi, mwenye vyeti vyake na kufanikiwa kumtoa kwenye nafasi yake kwa aibu.
Makonda kama unataka ahueni katubu na muombe radhi marehemu Kabwe labda mizimu yake itaacha kukuandama. Umewakosea wengi ila hili la Kabwe litakutafuna milele.
Sasa nimeamini hakuna jiwe litakalo salia juu ya jiwe.
Makonda kama unataka ahueni katubu na muombe radhi marehemu Kabwe labda mizimu yake itaacha kukuandama. Umewakosea wengi ila hili la Kabwe litakutafuna milele.
Sasa nimeamini hakuna jiwe litakalo salia juu ya jiwe.