Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 23,275
- 33,877
Rufiji,R.I.P gwiji. Halafu hakuna kitu kinaitwa nyimbo hii ni wimbo huu.
Jamii yetu ikiwemo wewe na mimi, hili linatuhusu. Hakuna wa kumnyooshea kidole.BURIANI SALUM ZAHORO
Makala hiyo hapo chini niliandika miezi miwili iliyopita.
Naiweka tena tuisome kama kumbukumbu ya Salum Zahoro aliyefariki jana na kuzikwa jana hiyo hiyo:
SALUM ZAHORO MWIMBAJI WA "TANGANYIKA NA UHURU" 1961 NI MGONJWA SANA ANAHITAJI MSAADA
Tarehe 9 Desemba TBC walirusha kipindi cha kumbukumubu ya uhuru kipindi kikijikita zaidi katika mchango wa watu walioishi Magomeni ya miaka ya 1950.
Niliwashauri TBC kutumia nyimbo ya Salum Zahoro na Kiko Kids, ''Tanganyika na Uhuru,'' katika kipindi chao na kwa hakika hili walilipenda sana na wakaipiga nyimbo hii wakati wa kumaliza kipindi.
Nimeweka clip fupi ya mwisho wa kipindi Salum Zahoro akiimba nyimbo hii.
Umri wa nyimbo hii ni sawasawa na umri wa miaka 59 kipindi cha uhuru wa Tanganyika.
Salum Zahoro aliimba nyimbo hiyo akiwa kijana labda wa miaka 20 akiwa kiongozi wa Kiko Kids Tabora.
Katika nyimbo hii utamsikia Salum Zahoro akiwataja viongozi wa Serikali ya Uhuru - Julius Nyerere, Abdallah Fundikira, Nsilo Swai, Tewa Said Tewa, Kawawa na wengineo.
Picha hii pamoja na nyimbo hiyo kaniletea Hamisi Delgado kutoka Ujerumani ambae ni mzaliwa wa Tabora na akimjua Salum Zahoro toka yeye bado kijana mdogo.
Nilimfahamisha Delgado maradhi ya Mzee Salum Zahoro alipokuja likizo na siku ya pili tu alikwenda kumjulia hali nyumbani kwake ambako alifahamishwa kuwa Mzee Salum Zahoro amelazwa Hospitali ya Amana.
Delgado alikwenda kumuona hospitali.
Inatia simanzi na kusikitisha kuwa wazalendo wetu waliojenga taifa hili hatuwathamini. Hapa sitasema mengi kwani tatizo hili kwa sasa ni maarufu hakuna asiyelijua.
Miezi michache iliyopita nilipokea simu usiku kutoka kwa Juma Mwapachu akaniambia kuwa yuko na Mzee Steven Hiza aliyetunga nyimbo, ''Tanzania Yetu ni Nchi ya Furaha,'' akiwa na Atomic Jazz Band ya Tanga.
Juma Mwapachu akanieleza masikitiko yake kwa hali ambayo amemkutanayo Mzee Hiza wakati nyimbo hii yake ndiyo imekuwa kama utambulisho wa taifa letu ukipigwa na steshini zote za radio na televisheni.
Aliniuliza nini tufanye ili Mzee Hiza na wanamuziki wetu walioitumikia nchi hii angalau waonje faida ya jasho lao lau kama tumechelewa.
Hii ndiyo hali ya mashujaa wetu waliohamasisha Watanzania katika kujenga taifa hili na kuleta maendeleo.
Picha ya Mzee Salum Zahoro akiwa amelazwa hospitali.
https://youtu.be/kb7etyo820c
View attachment 1693896
Sadaktaa Sheikh Mohammed.Rufiji,
Hili la "nyimbo," na "wimbo," lilijitokeza hapa nami nikajieleza.
Mimi nazungumza Kiswahili cha Kidarasalama ambako ndiyo kwetu.
"Nyimbo," ndivyo nilivyokuta wazee wangu wakizungumza.
Nimekuta wakisema, "saa," si "masaa."
Wakisema, "upungufu," si "mapungufu."
Hii ndiyo tofauti baina yetu.
Nguruvi3,Buriani Mzee Salum Zahoro
Hili la Wazee kutothaminiwa linatia uchungu. Mfano mzuri ni hiyo nyimbo ya Tanzania yetu ni nchi ya furaha' ambapo mtunzi hafaidiki na jasho lake kama walivyo wengi
Kuna sehemu nyingi ya tatizo.
Kwanza, ni kwa serikali zetu kutothamini watu waliotoa michango yao nyakati hizo.
Pili,ni watu waliokuwa madarakani 'wakalewa' na kujisahau leo wanatazama nyuma na kubaini tatizo.
Mfano, hivi Mzee Mwapachu, Mayor Sykes, Mayor Kitwana Kondo, akina Kandoro, Rais Kikwete n.k.ambao ni wenyeji wa maeneo wanayoishi hawa wazee hawakuliona tatizo hili wakiwa madarakani?
Walifanya nini wakati wakiwa na 'power' ?
Tatu, watu wanaowafahamu hawa wazee kama akina Mohamed Said wamefanya nini kuonyesha maisha yao ? Kuandika taarifa mzee akiwa Hospitali ni too late, kuandika Buriani ni jambo jema lakini linasaidiaje hali?
JokaKuu
Tuna rahis asiyejua historia na asiyejali kituRufiji,
Hili la "nyimbo," na "wimbo," lilijitokeza hapa nami nikajieleza.
Mimi nazungumza Kiswahili cha Kidarasalama ambako ndiyo kwetu.
"Nyimbo," ndivyo nilivyokuta wazee wangu wakizungumza.
Nimekuta wakisema, "saa," si "masaa."
Wakisema, "upungufu," si "mapungufu."
Hii ndiyo tofauti baina yetu.
Rufiji,
Hili la "nyimbo," na "wimbo," lilijitokeza hapa nami nikajieleza.
Mimi nazungumza Kiswahili cha Kidarasalama ambako ndiyo kwetu.
"Nyimbo," ndivyo nilivyokuta wazee wangu wakizungumza.
Nimekuta wakisema, "saa," si "masaa."
Wakisema, "upungufu," si "mapungufu."
Hii ndiyo tofauti baina yetu.
Kichuguu,Singular nouns (zinazohesabika) za kiswahili zinazoanza na "w," wingi wake huanza "ny." Kwa mfano Wimbo-Nyimbo (Albamu ina nyimbo nyingi zunri, ila kuna wimbo mmoja nilioenda sana) , Wembe-Nyembe (Kasha lina nyembe 12 lakini kinyozi hutumia wembe mmoja tu kumnyoa mteja wake), Wakati-Nyakati: kwa maana ya kipindi fulani kwa siku (Wakati wa usiku siyo muda mzuri kwenda nje ila kuna nyakati nyingi ambapo kunakuwa hakuna haja ya kutokwenda nje usiku). Kwa hiyo unaposema nyimbo una maana ya nyimbo nyingi, siyo wimbo mmoja.
View attachment 1697135
View attachment 1697136
Kuna maneno mengi kwenye kiswahili leo ni mapya kutokana na utamaduni kubadilika. Zamani sana watu walikuwa hawajali muda kwa hiyo inawezekana hawakuwa wanahesabu masaa; ni kama ambavyo hatukuwa na utamaduni wa kufanya matengenezo ya vitu vyetu mpaka viharibike kabisa, kwa hiyo hatukuwa na neno la ukarabati.Kichuguu,
Ahsante kwa.juhudi yako lakini zingatia kuwa hata hiyo "standard Kiswahili," imetuletea maneno ya "s" class na "u" class ambayo hayakuwa na plural ya wingi.
Leo tuna "masaa" na tuna, "mapungufu," maneno mimi katika Kiswahili chetu cha Kidarisalama hayakupata.kuwa na wingi.
Kichuguu,Kuna maneno mengi kwenye kiswahili leo ni mapya kutokana na utamaduni kubadilika. Zamani sana watu walikuwa hawajali muda kwa hiyo inawezekana hawakuwa wanahesabu masaa; ni kama ambavyo hatukuwa na utamaduni wa kufanya matengenezo ya vitu vyetu mpaka viharibike kabisa, kwa hiyo hatukuwa na neno la ukarabati.
leo hii elewa kuwa neno saa lina maana mbili; maana moja ni ile ya kuonyesha muda (o'clock) ambalo halina wingi; Utaamka saa moja, ufike nyumbani kwangu mbili na nusu na kadhalika. Lakini vile vile neno saa lina maana ya kuonyesa urefu wa muda (hour) katika kipindi fulani, ambalo lina wingi: kutoka Dar kwenda Morogoro safari inachukua muda saa moja au inachukua muda wa masaa mawili. Hili neno liliwahi kujadiliwa zamani sana na Sheikh Suleiman Kilemile katika kipindi cha baraza la kiswahili RTD zaidi ya miaka 25 iliyopita kwa hiyo halina ubishi.
Hilo la upungufu na mapungufu pia nina imani liko hivyo hivyo unavyopinga kwa kufuata isimu ya kiswahili.
Siyo swala la kiswahili cha bara wala cha Dar es salaamu au cha Mombasa au cha Tanga au cha Zanzibar, bali tunaongelea kiswahili kufuatana na isimu ya lugha yenyewe kama inavyotambulika na BAKITA. Kiswahili cha makabila mbalimbali kinaweza kuwa kinachanganya na lugha zao za asili lakini kiswahili cha BAKITA ni hicho tunachokuambia, inawezekana na wewe unaongea kiswahili cha kabila lako kwa hiyo hufuati isimu ya kiswahili bila kujielewa. Nimeishi na wamarekani wengi ambao hawana lugha nyingine bali ni kiingereza tu lakini wanaongea kiingereza broken sana, kwa mfano anaweza kupinga jambo kwa kusema "I don't know nothing!" Kwa hiyo na wewe inawezekana umeazaliwa na kukulia dar es Salaam na unajua kiswahili tu, lakini ni hicho kiswahi cha "I don't know nothing"Kichuguu,
Mimi sina tatizo na Kiswahili anachozungumza mzaliwa wa bara kwake yeye, "darasa," anaweza akatamka kama, "dalasa."
Hivyo ndivyo alivyojfunza na ndivyo anavyozungumza.
Anaweza kutamka, "masaa," "lisaa" nk.
Sina tatizo asilani.
Kama ulivyosema hicho ni Kiswahili kipya.
Tuna rahis asiyejua historia na asiyejali kitu