Buriani Kingunge…Lakini…!!!

Buriani Kingunge…Lakini…!!!

Huyo mbwa aliye muuma pengine kuna masharti yalikiukwa (masharti ya ufugaji). Wataalamu wa sheria na katiba kipengele cha mazishi ya wanaopa kwa kushika katiba kipo?

RIP
 
Huyu mzee sijui kwanini alikua anataka Lowasa awe Rais? Ina maana hakumuelewa KBS nyerere enzi za uhai wake kwanini alikua hataki kusikia lowasa anaisogelea ukulu? Ngoja akakutane nae huko sijui atamjibu nini
 
Alituangusha sana wakati wa Bunge la Katiba Mpya.Kama angekomalia mabadiliko ya katiba as alivyokomalia Lowassa na UKAWA...Tungekuwa na Katiba Moya iliyokusudiwa na Warioba.

Alibumbiwa mpaka nafasi ya Waganga wa Tiba Asilia,lakini hakuitumia vyema,na mabadiliko yale aliyotamani kupitia Lowasa na siyo yule "Nyapala" wa CCM(Kama alivyomuita mwenyewe) yaliadhibiwa na Katiba aliyokataa kuibadili.

Yote kwa yote!!Apumzike kwa Amani!!!Wanasema "Kifo cha Mende" ni maarufu kuliko vifo vya Wadudu wote watambaao
Fikra na maamuzi mengi ya wanasiasa hutawaliwa na "maslahi".
 
Mleta Uzi nawe umemsema Mzee Kingunge kwa muundo wa kung'ata na kupuliza eeeh!?

Mleta uzi, Mwenyezi Mungu anakuona!!

R.I.P Mzee Kingunge.

Poleni wafiwa wote.
 
Swali ni watanzania tutamkumbuka kwa lipi litakalo dumu vizazi kwa vizazi? Lipi katuachia la kum enzi? Nadhani tuna cha kujifunza.
 
Nilichojifunza ni kuwa kwenye siasa hakuna misimamo ya kudumu,hakuna rafiki wa kudumu wala adui wa kudumu..
 
Alifaidi sana makusanyo ya Ubungo Terminal
 
Buriani Kingunge…Lakini…!!!

0*UJdTfTjE1Q1fc-Is.

Mwanasiasa mkongwe kabisa nchini Tanzania, Kingunge Ngombale Mwiru amefariki leo baada ya afya yake kudhoofika katika siku za hivi karibuni. Katika namna ambayo ni kifo tu kinaweza kufanya, wanasiasa mbalimbali bila kujali tofauti zao wamekuwa wakitoa salamu zao za rambirambi kufuatia kifo hicho.

Kwa mujibu wa mila na desturi za Kiafrika, “marehemu huwa hasemwi vibaya.” Lugha inayopaswa kutumika kumwelezea mtu aliyefariki inapaswa kuwa ya hudhuni, upole na unyenyekevu. Kumkosoa marehemu hata kama anastahili kukosolewa hutafsiriwa kama “roho mbaya” au hata “uchawi.”

Sambamba na lazima ya “kutomsema vibaya marehemu” ni kasumba isiyopendeza ya unafiki wa “mchana kweupe” pindi kunapojitokeza msiba.

Naam, kwenye misiba tunakuta watu walewale waliompa wakati mgumu marehemu alipokuwa hai wakigeuka na kujifanya malaika wenye uchungu mkubwa kufuatia kifo hicho. Imezoeleka miongoni mwetu kuwaongelea vizuri mno wenzetu waliotangulia mbele ya haki ilhali tulitumia muda mwingi wa uhai wao kuwasema vibaya.

Kwanini tumwonyesha mtu upendo anapofariki badala ya kumpatia upendo huo alipokuwa anauhitaji zaidi akiwa hai? Hakuna maelezo sahihi zaidi ya UNAFIKI, sie ni wanafiki wazuri na sote twafahamu hilo.

Na kama ilivyo kawaida, kauli za wanasiasa na watu mbalimbali kuhusu kifo cha Kingunge zinashabihiana: kila mmoja amepatwa na uchungu mkubwa kutokana na kifo hicho, na kila mmoja anamwona mwanasiasa huyo kama mfano bora wa uongozi wa taifa letu. Hata wana-CCM waliomkosea heshima mzee huyo alipoamua kujitenga na chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, leo wanamzungumzia kwa heshima kubwa.

Lakini mimi ni nani kuwahkumu waliompenda Kingunge kwa dhati na waliomchukia? Na pengine wala hakuna ubaya kwa mtu kukuchukia katika sehemu kubwa ya uhai wako lakini akaguswa mno na kifo chako kiasi cha kuwa na majonzi zaidi ya waliokupenda wakati wa uhai wako. Kifo ni fumbo moja gumu kabisa kwa mwanadamu kulielewa japo kiduchu.

Tukiweka kando majonzi ya kuondokewa na mwanasiasa huyo mkongwe, pengine si vibaya kuangalia ‘legacy’ yake kwa Tanzania yetu. Kwa bahati mbaya, mwanasiasa huyo hana mengi ya kukumbukwa baada ya kifo cha swahiba wake marehemu Baba wa Taifa Julius Nyerere.

Kwa upande mmoja, licha ya ukweli kwamba Kingunge na wafuasi wengine wa Mwalimu walikuwa karibu na kiongozi huyo, kimsingi uongozi wa taifa ulikuwa mikononi mwa mtu mmoja: Nyerere. Kwamba Nyerere alikuwa na uwezo mkubwa sana kiuongozi kiasi cha kutohitaji kushirikisha viongozi wengine, au kwamba viongozi wengine walikuwa waoga “kulazimisha” kushirikishwa katika uongozi wa taifa, nafasi finyu katika makala hii hairuhusu mjadala wa aina hiyo.

Kilicho bayana ni kwamba akina Kingunge waliendelea kuwa watu wa karibu wa Mwalimu hadi alipong’atuka, na taratibu wakaanza kuchukua mielekeo binafsi, ambapo baadhi ilikinzana waziwazi na alichosimamia Mwalimu.

Kuna wachambuzi wengi tu wa kisiasa wanaodhani kwamba akina-Kingunge “walimsaliti” Mwalimu kwa kushindwa kudumisha kile alichopigania nao. Lakini kuna wanaodhani kwamba akina-Kingunge walilazimishwa na mazingira kuafikiana na Mwalimu, pengine hata pale ambapo hawakuafikiana nae, lakini mazingira ya zama za “chama kushika hatamu” yalikuwa hayaruhusu mawazo mbadala.

Lakini pia pengine sio kuwatendea haki akina-Kingunge kwa kuchukua mielekeo tofauti na ile aliyosimamia Mwalimu.Tuchukulie mfano “mauaji ya itikadi ya Ujamaa” yaliyofanyika katika kinachoitwa “Azimio la Zanzibar.” Japo Azimio hilo linalaumiwa kwa “kuiua” itikadiya Ujamaa, mazingira yaliyokuwepo wakati huo yalilazimisha taifa likumbatie mageuzi yaliyokuwa yakitokea sehemu mbalimbali duniani, kubwa zaidi ikiwa ni anguko la ukomunisti katika uliokuwa muungano wa jamhuri za kisosahalisti za kisovieti (USSR).

Kuna wanaodhani pia kwamba Mwalimu hakuwa na “waumini wenzie” wala “wanafunzi” bali alizungukwa na kundi la watu waliokuwa wanasubiri wakati wao ufike waanze kufakamia keki ya taifa. Lakini pengine kama nilivyoeleza awali, hakukuwa na misingi imara ya kuendelea kile alichoamini Mwalimu na “waumini wenzie” na “wanafunzi wake.”

Je Kingunge legacy ya Kingunge inaweza kuwa ipi hasa? Kwa mtizamo wangu, na kwa bahati mbaya, alipoteza mapema fursa muhimu kwa mwanasiasa huyo kuwa mrithi halisi wa Baba. Licha ya heshima kubwa aliyojijengea katika duru za siasa, aliamua kuelemea pande ambazo laiti Mwalimu angekuwa hai, zingewafarakanisha.

Mwaka 2015 alipochukua uamuzi wa kujiweka kando ya CCM hakufanya hivyo kwa vile chama hicho kilikuwa kimbilio la mafisadi au kilisaliti misingi iliyowekwa na Nyerere, bali alichukua uamuzi huo kwa sababu jina la swahiba wake, Edward Lowassa, lilikatwa na katika vikao vya mchakato wa CCM kupata mgombea wake katika nafasi ya urais kwenye uchaguzi mkuu uliopita.


0*r_VqU5jyf2nVAdar.jpg

Kuna wanatafsiri uamuzi wa akina Kingunge, Lowassa, Sumaye, nk waliohama CCM na kwenda vyama vya upinzani kwa kisingizio cha “kuing’oa CCM” ni walafi tu wa madaraka waliokuwa wakitafuta fursa nyingine ya “kula keki ya taifa” kupitia kambi ya upinzani. Na pengine ndio maana mchango wa wana-CCM hao wa zamani kwenye siasa za upinzani sio mkubwa “kihivyo.”

Nihitimishe makala hii kwa kutoa salamu za pole kwa familia, ndugu na jamaa wa marehemu Kingunge, na kutoa rai kwa wanasiasa wengine kujifunza kutumia vema imani waliyonayo wananchi kwa wanasiasa hao, na hatimaye kutengeneza legacy nzuri pindi watakapoitwa mbele ya haki.

Rest in Peace Mzee Kingunge Ngombale Mwiru

CHANZO:

umeandika upuuzi gani wewe
 
Mzee Kingunge ndio aliekuwa mpishi mkuu wa siasa,lakini mtekelezaji mkuu hakula na kuwagawia watu wake mapishi yote,tatizo liko hapo.Laiti mtekelezaji mkuu angewapa watanzania mapishi yote ya Mzee Kingunge labda Tanzania ingekuwa imepiga hatua kubwa.
R.I.P Mzee Kingunge.
 
MABADILIKO gani unayodai alikuwa akitamani wakati yeye alishabadilika kitambo kutoka mjamaa mpaka ubepari ambao unachagizwa na ufisadi.

Waulize Jiji la Dar kuhusu ubepari wa kampuni ya Kingunge na familia yake!

Alichokuwa anapigania ni status quo katika kuendeleza ufisadi.
Kwamba vyombo vya usalama vilikuwa vinamwogopa Kingunge? Vilikuwa vimepigwa ngazi na Kingunge? Tunapowaambia nyie maCCM ni hovyo kabisa mifano yenyewe ni kama hii!
 
Yaani mtu akifa akiwa ccm ni dhahiri anafikia tanuru la moto moja kwa moja..
Mzee ni kama aliliona hilo ikabidi atubu aungane na wanyonge..!!
 
Huyu mzee sijui kwanini alikua anataka Lowasa awe Rais? Ina maana hakumuelewa KBS nyerere enzi za uhai wake kwanini alikua hataki kusikia lowasa anaisogelea ukulu? Ngoja akakutane nae huko sijui atamjibu nini
Habari za mitaani hizo!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom