Buriani "Hayati Moringe Sokoine" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Buriani "Hayati Moringe Sokoine"

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by buhange, Apr 12, 2012.

 1. buhange

  buhange JF-Expert Member

  #1
  Apr 12, 2012
  Joined: Oct 23, 2011
  Messages: 494
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Ni sekunde, dakika, masaa, siku, miezi na miaka kadhaa sasa tangu mpendwa wetu Hayati Moringe Sokoine, Waziri mkuu wa zamani atutoke kwa ajali mbaya ya gari akiwa safarini kuelekea Dar es Salaam kutokea Dodoma, hatimaye leo tunaazimisha miaka kadhaa ya kifo chake, Kwa tuliokuwepo na ambao hatukuwepo kipindi cha utendaji wake, lakini tukiwa tumepata fursa ya kusikia aina ya uchapa kazi wake enzi zake!, Nini wito wako kwa viongozi wetu wa sasa ktk kumuenzi Mpigania haki huyu na maendeleo ya wanyonge ktk enzi hizo? Atakumbukwa daima.
   
 2. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #2
  Apr 12, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Sina uhakika kama serikali yetu au wanazuoni wetu wameandaa shughuli au mdahalo wowote wa kumbukumbu ya shujaa huyu.
  Sijisikii vizuri sana kwa shujaa huyu kusahaulika kiasi hiki.
   
 3. Jeji

  Jeji JF-Expert Member

  #3
  Apr 12, 2012
  Joined: Jun 28, 2011
  Messages: 1,981
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  kutakuwa na misa/sala leo saa 9 alasiri eneo
  ilipo tokea ajali iliyo muua hayati Moringe Sokoine.
  nilisikia jana bungeni na Waziri mkuu atahudhuria.
   
 4. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #4
  Apr 12, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 569
  Trophy Points: 280
  Yaani Hayati E. M. Sokoine alikuwa ni mchapakazi haswaaaaaa!!!!!!!!

  Sidhani kama kuna kiongozi yeyote Hapa Tanzania anayeweza hata kufikia Robo ya Uwezo wa Utendaji aliokuwa nao Sokoine.

  Kwa kweli anastahili Heshima zote na kukumbukwa Daima katika Historia ya Tanzania.

  Ningefarijika kama SErikali ingeamua kumkumbuka hata kwa kuanzisha taasisi ya kumuenzi kiongozi huyu, ili viongozi wetu waige mfano wake katika kupanmbana na Rushwa na ubadhirifu wa mali za Umma / uhujumu Uchumi.

  Nakumbuka Vita ya Wahujumu Uchumi ilikuwa vita kali sana, kwani Mafisadi wa enzi zile walihaha!!!  MIZAMBWA
  NABII MTARAJIWA!!!
   
 5. buhange

  buhange JF-Expert Member

  #5
  Apr 12, 2012
  Joined: Oct 23, 2011
  Messages: 494
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Ni kweli ndugu yangu Mizambwa, Leo nimesikia kupitia kituo kimoja cha habari kwamba kumbe hata Eneo walipoweka Mnara wa kumbukumbu ya ajali ya Hayati Moringe hapafanyiwi usafi kabisa na ingawa ni barabarani kabisa ktk barabara ya Dodoma-Dar, lakin viongozi wetu huwa hawana hata habari na eneo hilo kabisa, shame enough serikali hii, Sipati mantiki ya swala hili
   
 6. M-mbabe

  M-mbabe JF-Expert Member

  #6
  Apr 12, 2012
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 4,992
  Likes Received: 3,741
  Trophy Points: 280
  .....very sad.
  hatuombei..... lakini ngoja itokee aje kufa (akiwa mstaafu tayari) mkulu wa sasa pale magogoni. wasanii wote (clouds, bongo flavour, etc) wataifanya tarehe ya kifo chake kuwa ni one big annual countrywide event, ikiambatana na zile pati za kufa mtu!
   
 7. Mchochezi

  Mchochezi JF-Expert Member

  #7
  Apr 12, 2012
  Joined: Feb 29, 2012
  Messages: 6,953
  Likes Received: 1,155
  Trophy Points: 280
  yaan inasikitisha sana jembe kama hili kusahaulika kiasi hiki!
  Huwa napenda sana Kusoma Kitabu kiitwacho Morani ambacho husomwa A-level, hadithi ya mule ndani inamzungumzia sokoine mwanzo mwisho!
  R.I.P Edward Moringe Sokoine!
   
 8. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #8
  Apr 12, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Kweli mkuu hvyo vi-media ulivyovitaja vimeanza kujadili eti tarahe aliyokufa msanii maarufu iwe na maadhimisho yake kila mwaka!

  Nani anajua kitatokea nini tarehe hyo mwakani??

  Tungekuwa taifa la maana leo ilitakiwa iwe siku kubwa sana, tena huu ungekuwa mda muafaka kuweka kumbukumbu sawa juu ya kifo chake!
   
 9. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #9
  Apr 12, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,333
  Likes Received: 1,796
  Trophy Points: 280
  RIP Moringe Sokoine. This I think was the man with the pill to cure our diseases...uvivu, rushwa, uongo, wizi wa mali ya umma,udini etc
   
 10. S

  Skype JF-Expert Member

  #10
  Apr 13, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 7,284
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135

  Sokoine University of Agriculture (SUA) kwa mawazo yangu ni taasisi mojawapo au wadau mnasemaje?
   
 11. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #11
  Apr 13, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 569
  Trophy Points: 280

  Ni vizuri kama tukiwaenzi viongozi hawa maarufu wa Taifa letu kutokana na mambo au matukio waliyoyafanya kwa Taifa hili. Tutekeleze kwa vitendo si isiwe tu kwa kuongea.

  TUWAENZI KIVITENDO. matendo yao mema tuyafuate na ushauri wao mzuri tuuzingatie ili Taifa letu liweze kufanikiwa.

  Ukisikiliza kipindi cha "WOSIA WA BABA WA TAIFA" katika Redio na kama yale maneno mazuri tungeyafuata, au viongozi wetu wasasa wakiyazingatia. nafikiri kuna baadhi ya majanga unayokutana na yo leo hii kama si kuyaepuka basi yangelipungua kasi.

  Lakini nani anayajali hayo maneno ya Mwalimu Nyerere. Kuna maneno aliyasema miaka ya sabini lakini leo utadhani kama yupo jukwaani anaongea kutokana na matukio yaliyopo.

  RUSHWA, UBADHIRIFU WA MALI ZA UMMA, ULANGUZI, UHUJUMU UCHUMI ulikuwepo toka enzi za marehemu Sokoine, na ni vita ambayo aliianzisha miaka ya Themanini kabla ya kifo chake.

  Leo hii yote tunayo tene kwa kasi zaidi, nguvu zaidi na tunayaangalia pasipo kuyapatia ufumbuzi yakinifu.

  Hivi vyuo tulivyovipatia majina ya viongozi wetu Mf. Mwl. Nyerere, SUA, NElson Mandela University. Ni heri viwaenzi kwa vitendo. Wasomi wanaotoka katika vyuo hivi wamuenzi vilivyo na siyo kwenda pale kwa ajili ya kupata elimu tu. Na masomo yawe muhimu kwa ajili ya kulienzi jina la Chuo husika.

  TUSIPOBADILIKA TAIFA LITAANGAMIA!!!  MIZAMBWA
  NABII MTARAJIWA!!!
   
Loading...