Lady Whistledown
JF-Expert Member
- Aug 2, 2021
- 1,031
- 1,648
Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii imewasilisha taarifa yake kuhusu mahojiano iliyofanya na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) baada ya Waziri Wa Elimu, Prof. Adolf Mkenda, Novemba 2, 2022, kudai Bungeni kuwa Bodi hiyo inamkwamisha
Akiwasilisha taarifa hiyo kwa niaba ya Mwenyekiti wa Kamati, Mbunge wa Singida Mjini (CCM), Mussa Sima amesema kikubwa walichobaini ni mawasiliano hafifu kati ya Wizara ya Elimu na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu
Akichangia ndani ya Bunge, Profesa Mkenda amekanusha hajawahi kulalamika ndani ya Bunge kwa kuwa anaimudu kamati hiyo, pia hajawahi kusema kama bodi inamkwamisha, kauli ambayo iliwaibua baadhi ya Wabunge kumuombea mwongozo kwa madai alitoa kauli hiyo na ndiyo sababu ya Spika kuteua Moja ya Kamati ikapate uhakika
Chanzo: Mwananchi