Bungeni sio darasani- Azan | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bungeni sio darasani- Azan

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Dopas, Sep 24, 2010.

 1. D

  Dopas JF-Expert Member

  #1
  Sep 24, 2010
  Joined: Aug 14, 2010
  Messages: 1,151
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  WanaJF nimeikuta hii kali ya Idd Azzan-mgombea ubunge wa Kinondoni-CCM katika Majira ya leo 24/09/10 "Jamani hivi watu wanadhani bungeni ni kama darasani ambapo kila mtu anaongea anavyotaka, kule kuna utaratibu maalumu siyo unasimama bila mpangilio na kuzungumza unavyotaka," alisema Bw. Azzan.

  Huyo mheshimiwa alituhumiwa na wapinzani wenzake kuwa hachangii hoja yoyote bungeni, hivyo ndivyo anavyojitetea kwa wananchi wake.

  Swali 1. Ni kweli darasani kila mtu anaongea anavyotaka?

  Ninavyofahamu darasani maswali na michango ya wanafunzi pamoja ya majibu ya walimu hufanywa kwa mipango. Pia napenda kuamini kuwa bunge ni zaidi ya darasa kwa sababu kila moja akijua wajibu alionao kwa niaba ya waliomtuma na kwa faida ya nchi yake lazima azungumze, tofauti na darasani kama somo limeeleweka hakuna haja ya michango zaidi au maswali zaidi.

  2. Kuna kazi gani nyingine bungeni kama sio kwenda kuongea kwa niaba ya waliokutuma?
  Ninavyofahamu bungeni ni nafasi nzuri zaidi ya kuongea kwani hakuna kuandika notes, wala nini. Kila kitu wanaandaliwa. Ni kuzipitia tu hoja na kuzungumza hata kama hapati nafasi kila siku. Lakini ipite siku... wiki... mwaka ..... na baada ya miaka mitano anajitetea kuwa sio lazima kuzungumza, unaweza kuandika karatasi ikawakilisha hoja yako. Huo ni utaratibu unaofahamika.

  3. Kwa miaka yote mitano Mbunge anaandika kikaratasi cha kuwakilisha hoja zake?
  Kama kila mara alituma hoja, michango yake nadhani wananchi wake wangefahamu.
  Kwa maoni yangu wananchi wa Kinondoni wawe macho, huyo mtu hawafai, ni mkwamishaji wa maendeleo yenu na ya Taifa kwa ujumla, asijitetee uwongo. Kama kuna mtu mbadala kutoka chama cha upinzani mpeni kura mwaka huu.
   
 2. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #2
  Sep 24, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,840
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  Look the guy is too nervous.He is unfit to represent today's tanzanians taking into account that today the world is sorrounded by science and IT alongside.Hajui kama anakula kodi zetu, hatuko tayari kulipa mazezeta wa siasa, eti tu kwa sababu anfanya biashara ya kusafiri sana nje.Hata wauza unga wanasafiri bado they are termed as destractors of human lives.
  Piga china zezeta hilo
  You kinondoni voters;Keep him aside
   
 3. SILENT WHISPER

  SILENT WHISPER JF-Expert Member

  #3
  Sep 24, 2010
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 2,231
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  ni aibu kubwa ..KINONDONI KWA WAJANJA kuwa na mbunge kama huyu..!

  mie nadhani KARATU , KIGOMA KASKAZINI, KYELA kuna wajanja zaidi ya kinondoni , kwa vipimo vya kutoa wabunge wanaolisadia TAIFA. BILA KUSAHAU LOLYA KWA WANAMUME ...!

  ILALA , IGUNGA NA TABORA MJINI ndo hooooovyooo kabisa..! mnachangia kuliua taifa hili kwa kutuchagulia MAKAPI...! WAKE UP.
   
 4. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #4
  Sep 24, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,938
  Likes Received: 2,088
  Trophy Points: 280
  Wajanja si wako Sinza jamani?
   
 5. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #5
  Sep 24, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,938
  Likes Received: 2,088
  Trophy Points: 280
  Tatizo amefanya diploma ya Sound Air na kutengeneza madege ya JWTZ! Profile yake hii hapa Parliament of Tanzania
   
 6. p

  pierre JF-Expert Member

  #6
  Sep 24, 2010
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 211
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Msimlaumu ndio upeo wake.Msimtwike mzigo wa kumzidi nguvu.
   
Loading...