Bungeni: Naibu Spika alalamikiwa kumzunguka Spika Ndugai

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,739
32,866
Habari ndio hizo kwenye vikao vya Bunge rasmi na visivyo rasmi,kuwa Naibu Spika ananung'unikiwa kumzunguka Spika katika mambo mengi yanayohusu Bunge na utendaji wake.Hii inatokana na ukweli kuwa Naibu Spika ameonekana kuwa karibu ya Rais na watendaji wa Serikali kuliko kiongozi wake wa Bunge

Naibu Spika amekuwa mtii kwa Serikali kuliko muhimili wake wa Bunge,na mambo mengi Serikali imekuwa ikimtumia kupitisha ndani ya Bunge,moja ya swala ambalo lilianza kuzua utata ni swala la kuwa na matangazo ya moja kwa moja ya Bunge,hili lilizua utata mkubwa sababu ni jambo lililopendekezwa na serikali na kupitishwa kwa naibu Spika na kumfika Spika,mwanzoni Spika hakuona kama ni jambo lenye afya kwa bunge lake,sababu naye alitaka kuwa sehemu ya historia ya Bunge la mfano na lenye kuisimamia serikali na hivyo kuacha historia.

Alizidiwa nguvu baada ya mpango kuwa umeshapangwa na kufikia hatua za kutolewa tamko na Nape Nnauye Bungeni,hali hii haikuwapendeza wabunge wengi wa upinzani na hata chama tawala.Katika vikao vya ndani vya Wabunge wa CCM,wabunge wengi waliipinga hoja hii wakisema ni dalili za Serikali kuingilia uhuru wa vyombo vya habari na uhuru wa bunge na wananchi.Mbunge wa Kilolo wa CCM Mh.Mwamoto alikuwa ni mmoja wa wabunge walioamka na kupinga hoja hii akisaidiwa na Mbunge wa Sumve Mh.Ndassa.Hali hii iliibua mzozo mzito na mwisho wa siku Naibu Spika akishirikiana na Waziri wa Habari wakatoa msimamo kuwa huo ni uamuzi wa chama na si serikali,hivyo wao kama wabunge wa chama wanatakiwa kuafikia na uamuzi huo.Mpaka sasa wabunge wengi wa CCM hawakubaliana na uamuzi huo na wanaona kama ni dalili za kuminywa kwa wao kuwawakilisha wananchi wao

Hali ya Naibu Spika kuwa "mtendaji wa serikali" zaidi ya wa mhimili wa Bunge umeonekana kwenye suala la bunge kutoa hela zake na kuipa serikali.Kitendo hiki kilifanyika bila naibu spika kumpa taarifa spika,na hii ikasababisha spika kuona tu kitendo kimefanyika kwenye "Magroup ya WhatsApp" na mitandao mingine ya kijamii.Naibu Spika ameonekana kujiona yeye ni wa "serikalini" zaidi kuliko wa bungeni na hasa baada ya kuwa yeye ni mteuliwa wa Rais wa moja kwa moja.

Hili la naibu spika limezua malalamiko ya chinichini sana kwa wabunge wa Chama tawala,hali hii ndio ikapelekea wabunge kumpenyezea hoja hiyo Godbless Lema kumfikishia ujumbe naibu spika wakati wa kuchangia bajeti ya Ofisi ya Rais Utawala bora,na hata baada ya Lema kumwambia kuwa Naibu Spika anamzunguka Ndugai na kujiweka karibu na Serikali,naibu spika alikaa kimya,ila wakati wa kuahirisha bunge akatoa tamko kuwa maelezo ya Lema yanataka "kumgombanisha" na Spika.

Kwa mwenendo wa bunge kutoonyeshwa live ni swala linalowaumiza wabunge wote,ila wale wa chama tawala wanaendelea kuongelea Canteen na kwenye sehemu za nje ya ukumbi ili kutokuendana kinyume na msimamo wa chama.Wapo Mawaziri pia ambao walihitaji kuwa live ili wananchi wenye kero mbalimbali wanaozileta kupitia wabunge wawe wanasikia majibu ya matatizo yao moja kwa moja kutoka bungeni,lkn sababu ya msimamo wa chama,nao wameamua kukubaliana na hali hii.

Hizi ndio pata nikupate toka katika viunga vya Bunge weekend hii....Tutaendelea kusikiliza tukibarizi kutoka maeneo ya Nzughuni na Dodoma Carnival...
 
Mie nilikuwa ninashauri hivi, kwa kuwa watu wengi wanatoka kazini saa 10 basi tbc ionyeshe live bunge la jioni kuanzia saa 10 hadi wanapofunga.halafu warushe recorded kuanzia saa tatu usiku kwa ajili ya mijadala iliyofanyika asubuhi. Hili likifanyika watu hawatakuwa na shida sana.nikweli wengi wetu asubuhi tunakua kwenye pilika lakini ile jioni mpaka mapema ya usiku usiozidi saa 4 kamikli jioni/usiku ndo mda mzuri wa kufuatilia.

Kama serikali inania safi basi ichukue huu ushauri kuliko inavyofanyika sasa
 
Huyu Naibu Spika ndivyo alivyo, ninyi mlitaka afanyeje wakati Ubunge alipewa kama Zawadi?

Tena hapa Serikali inajificha kwenye nyumba ya kioo
 
Lawama Za Msingi Ziende Kwanza Ccm Ni Ile Ile
Halafu Watu Kama Naibu Spika Ikiwa Ni Kweli Na Wote Wa Lumumba Buku Saba
 
Jamaa yake alipiga marufuku semina elekezi na akikutwa mtu yeyote anaitoa atalala nae mbele.
 
Back
Top Bottom