Jodoki Kalimilo
JF-Expert Member
- Feb 12, 2012
- 12,671
- 11,339
Tuna wabunge kama sikosei ni 357 kama kila mbunge atakuwa na wasaidizi 4, basi 357 x 4= 1,428. Hii ndiyo idadi watu watakoingia kwenye payroll ya serikali. Jumlisha sasa na gharama za office kwa kila mbunge. Then turudi kwenye hali halisi:
1. Nchi ambayo wagonjwa wanalala wanne kwenye kitanda kimoja na wengine chini, wasaidizi 4 kwa mbunge watasaidia nini?
2. Serikali ina uwezo wa kuwapa chochote (hongo?) wabunge lakini likifika swala la kulipa watu wanaokoa maisha ya raia inasema haina fedha!
3. Watoto wanakalia mawe, ndoo, vitabu hakuna, vyumba vya madarasa havitoshi serikali inaona kipaumbele ni office za wabunge?
4. Kuna shule zingine zina mwalim mmoja tu - wabunge ndio priority?
Hivi vipaumbele vya serikali ya CCM ni vipi? Nchi yoyote isiyowekeza kwa watu wake (rasilimali watu) inajitakia balaa. Nchi jirani zinakazana kuwekeza kwa watoto na umma kwa jumla, elimu bora, huduma nzuri za afya, hapa serikali ya CCM inaona ingelee kuwafurahisha wabunge ili waendelee kupiga makofi na kupitisha bajeti za kipuuzi zinazoishia kwenye mifuko ya wachache.
Kama kweli serikali itaanza kujenga office za bunge kabla ya kumaliza kadhia ya nyumba za walimu nchi nzima, basi walimu wanayo haki ya kuandamana. Huu ni upuuzi.
Wasaidizi wenyewe ni hawa:
- Dereva
- Mpiga chapa
- Karani
- Mhudumu wa ofisi
Mpiga chapa na karani? Kati ya dawa za kuokoa maisha au madawati na mpiga chapa kipi muhimu?
Hii mada ungeweka kwenye status yako ya Facebook ili kutupunguzia gharama ya intaneti(MB) kusoma hii kitu.Mbunge Wa vitimaalum mkoa Wa katavi Anna merystela Malac amemlipua pinda baada ya kuona amejisahaujimboni kwake,Mwenyewe ajitetea bungeni
Tuna wabunge kama sikosei ni 357 kama kila mbunge atakuwa na wasaidizi 4, basi 357 x 4= 1,428. Hii ndiyo idadi watu watakoingia kwenye payroll ya serikali. Jumlisha sasa na gharama za office kwa kila mbunge. Then turudi kwenye hali halisi:
1. Nchi ambayo wagonjwa wanalala wanne kwenye kitanda kimoja na wengine chini, wasaidizi 4 kwa mbunge watasaidia nini?
2. Serikali ina uwezo wa kuwapa chochote (hongo?) wabunge lakini likifika swala la kulipa watu wanaokoa maisha ya raia inasema haina fedha!
3. Watoto wanakalia mawe, ndoo, vitabu hakuna, vyumba vya madarasa havitoshi serikali inaona kipaumbele ni office za wabunge?
4. Kuna shule zingine zina mwalim mmoja tu - wabunge ndio priority?
Hivi vipaumbele vya serikali ya CCM ni vipi? Nchi yoyote isiyowekeza kwa watu wake (rasilimali watu) inajitakia balaa. Nchi jirani zinakazana kuwekeza kwa watoto na umma kwa jumla, elimu bora, huduma nzuri za afya, hapa serikali ya CCM inaona ingelee kuwafurahisha wabunge ili waendelee kupiga makofi na kupitisha bajeti za kipuuzi zinazoishia kwenye mifuko ya wachache.
Kama kweli serikali itaanza kujenga office za bunge kabla ya kumaliza kadhia ya nyumba za walimu nchi nzima, basi walimu wanayo haki ya kuandamana. Huu ni upuuzi.
This is Hilarious
tangu 1961 mpaka sasa tumekuwa na wabunge
wabunge wametekeleza majukumu yao
51 years later ndio tunaleta wasaidizi?
who initiated this?
NI UKWELI?????