Bungeni: Kubenea apewa siku nne kuthibitisha tuhuma dhidi ya JWTZ

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
17,506
16,004
Habari kutoka bungeni zinathibidisha kuwa Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea amepewa siku nne na Naibu spika kuthibitisha tuhuma dhidi ya JWTZ kuwa ilitoa ardhi kwa kampuni ya Hennang Guiging Industry Investiment kwa ajili ya kufanya ujenzi wa nyumba kwa miaka 40.

Kutokana na madai hayo Waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga Taifa Mh.Mwinyi alimtaka mbunge huyo kuthibitisha madai yake akiahidi ikithibitika atakuwa tayari kujiuzulu Uwaziri vinginevyo Kubenea achukuliwe hatua kali za kinidhamu za Bunge.

Hivyo kubenea kutakiwa kuthibitisha kauli yake hiyo kama Waziri alivyoomba mwongozo.

My take.
Uthibitisho huu utakuwa ni moja ya kithibitisho muhimu kuwa Magazeti ya Kubenea yanaandika ukweli au uongo.Tusubiri huku tukiweka akiba ya maneno.
 
Mwinyi Jr angekuwa wa kujiuzulu angefanya hivyo enzi za milipuko ya mabomu ya mbagala na gomz...
Mwinyi Sr alijiuzulu kwa shinikizo la Mwl JK na si vinginevyo so asitudanganye kuwa eti atafata nyayo za baba.
Kubenea ataleta ushahidi ila utafanyiwa figisu kama wa Lema kwa Pinda!
 
Mwinyi Jr angekuwa wa kujiuzulu angefanya hivyo enzi za milipuko ya mabomu ya mbagala na gomz...
Mwinyi Sr alijiuzulu kwa shinikizo la Mwl JK na si vinginevyo so asitudanganye kuwa eti atafata nyayo za baba.
Kubenea ataleta ushahidi ila utafanyiwa figisu kama wa Lema kwa Pinda!
Hapo kwa mwinyi sr eti alijiuzulu kwa shinikizo la nyerere si kweli
 
Kubenea ni mropokaji kila siku anakuja moto kwa lengo la kujijengea umaarufu kwa muda mfupi, nadhani angekuwa anapata ushauri kwa akina Mnyika kabla hajatamka jambo zito. Na hayo ni madhara ya elimu za ushanga.


Umekosea bwana, mropokajai ni Zitto Kabwe.
 
Ni vema Kubenea athibitishe.Hamna jinsi.Vingenevyo achukuliwe hatua.
 
Nilisema kwa mwaka msimu huu nadhani chadema watakuwa wamepeleka mbunge wa hovyo mno kubenea kuzidi wabunge wote waliowahi kupita chadema,
 
Back
Top Bottom