Bungeni - Kashfa ya Rada Wenje ailipua upya

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,884
6,885
Wenje(1).jpg

Ezekia Wenje

‘Aibu walarushwa wa rada kuongoza kamati Bunge’

Mzimu wa kashfa ya rushwa ya ununuzi wa rada ya kijeshi ambayo Tanzania iliinunua kutoka Uingereza umeibuka kwa mara nyingine bungeni, baada ya wabunge wa Kambi ya Upinzani kuchachamaa na kutaka waliohusika na ununuzi wa rada watajwe na kuchukuliwa hatua za kisheria.

Wabunge hao walikuwa wakichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa iliyowasilishwa na Waziri Bernard Membe.

Msemaji wa Wizara hiyo, Ezekia Wenje (Chadema-Nyamagana), alihoji: “Tunaendelea kuhoji kwa nini mpaka sasa watuhumiwa wa kashfa hiyo wanaendelea kutembea kifua mbele dhidi ya serikali bila hatua zozote kuchukuliwa?.”

Alisema hadi sasa haieleweki ni kwa sababu gani Tanzania pamoja na kudai kuwa ina uhuru wa kujiamulia mambo yake yenyewe iliamua kuliachia suala hili kufanyiwa kazi na Serikali ya Uingereza, kuanzia uchunguzi hadi kurudishiwa fedha zilizotokana na rushwa ya rada, ambazo kwa sasa zimebatizwa jina tamu la ‘chenji ya rada.’

“Katika hali inayoonesha kuwa baniani mbaya kiatu chake dawa, pamoja na serikali hii kushindwa kufanya uchunguzi na hatimaye kuwashtaki watuhumiwa wa rada, bado ilipobainika mahakamani kuwa tunatakiwa kurudishiwa chenji iliyotokana na rushwa, serikali ilikuwa mstari wa mbele kwelikweli katika kufuatilia chenji ya rada na katika kuipangia matumizi,” alisema na kuongeza:

“Tunashindwa kuelewa umakini wa serikali hii uko wapi kwamba inaweza kuweka msisitizo pekee katika kuhakikisha fedha za rushwa ya rada zinarejeshwa nchini, lakini haiwezi kuthubutu kabisa kushughulikia wale waliosababisha upotevu huo wa fedha za nchi kwa njia ya mikataba.”

Alihoji usikivu wa serikali ambayo pamoja na kelele zote za wananchi walioiweka madarakani kutaka watuhumiwa ufisadi kupimwa kwa kipimo kile kile katika mizani ya sheria na utoaji haki kama wanavyofanyiwa Watanzania wengine wanyonge.

“Bado serikali imetia masikio pamba na kufumba macho yake kwa mikono, kwamba haiwaoni mafisadi hao wala haisikii kelele za wenye nchi. Taarifa mbalimbali zinazotokana na utafiti na uchambuzi wa kina, zimeweka wazi wahusika wa kashfa ya ununuzi wa rada, zikieleza mchakato mzima namna wizi huo ulivyofanyika,” alisema na kuongeza:

“Ukiwahusisha Watanzania wengine wakiwa ni viongozi waandamizi wa serikali ya CCM na sasa Watanzania wanashangaa kuona watuhumiwa hao hao waliopaswa kuwa mikononi mwa sheria, sasa wanachaguliwa kuongoza mhimili muhimu wa Bunge! Kambi Rasmi ya Upinzani tunahoji je, hii ni dalili ya kuwa dola imetekwa na mafisadi?.”

Ingawa Wenje hakuwataja watuhumiwa hao kwa majina, lakini mmoja wa watuhumiwa hao anayeongoza moja ya kamati za Bunge ni Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge, ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi.

Chenge wakati wa mchakato wa ununuzi wa rada hiyo kutoka Kampuni ya BAE Systems mapema miaka ya 2000, alikuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Chenge alikutwa na Dola za Marekani milioni moja katika benki moja iliyoko katika Kisiwa cha Jersey nchini Uingereza.

Hata hivyo, mara kadhaa Change amekuwa akikanusha kuhusika katika wizi wa fedha za rada hiyo na kudai kuwa Taasisi ya Kuchunguza Makosa Makubwa ya Udanganyifu ya Uingereza (SFO) ilishamsafisha.

Mbunge wa Viti Maalum, Rachel Masishanga (Chadema), aliitaka serikali kueleza ni kina nani waliohusika na kuibia serikali katika kashfa ya rada.

“Tumepata chenji ndio tuwajue ni kina nani waliohusika na kama anawafahamu kwa majina naomba leo hii awaambie Watanzania waliohusika kuiibia serikali katika suala hilo la rada,” alisema.

Mbunge wa Gando, Khalifa Mohamed Khalifa (CUF), alihoji: “Nyie ndio mnatuletea wawekezaji, lakini nyie ndio mnapaswa kuangalia huko nje maslahi ya taifa. Wewe ni mwanadiplomasia namba mbili, wa kwanza ni Rais na wewe mwenyewe uliwahi kufanya kazi katika balozi, hivi kweli unataka kutuambia hujui watu wanaotuibia fedha zetu?” alisema na kusisitiza:

“Kweli hujui, hivi kweli hujui wawekezaji matapeli ukatuambia unaruhusu wanakuja tu hapa kila siku vinasemwa vitu hivi na watu wanafanya utafiti, hii ni aibu kubwa sana, hatuwezi hata siku moja tukavumilia nchi inadhalilishwa na watu na nyie nawajua mnawanyamazia, utakapokuja kufanya majumuisho utawatajia Watanzania,” alisema.

Alisema hata kama yeye (Khalifa) yumo katika orodha ya watu hao waliohusika na rushwa Membe amtaje.

Akijibu katika majumuisho ya hotuba ya Waziri Membe jana jioni, Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe, alisema hakuna mtu yeyote kutoka Tanzania ambaye anaweza kushtakiwa mahakamani kwa mashitaka ya rada.

“Kama kuna mtu yeyote ndani ya Bunge ama nje ya Bunge mwenye ushahidi juu ya mtu yeyote kama walimpiga picha ama mlikuwa naye atuletee huo ushahidi na tutapeleka mahakamani,” alisema.

Alisema jana asubuhi alizungumza na Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP), Eliezer Feleshi pamoja Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk. Edward Hoseah, ambao walisema hakuna kitu kipya na wala hawafanyi uchunguzi kuhusu sakata la rada.

Wiki iliyopita, Rais Kikwete, alisema hakuna mtuhumiwa katika sakata ya rushwa na kwamba walioanzisha suala hilo ni SFO.

Rais alisema baada ya kuwahoji maofisa hao, SFO walirudi Uingereza na kukaa kwa muda mrefu pasipo taarifa yoyote, lakini walishangaa kusikia kwamba kampuni iliyokuwa imetuhumiwa kwa rushwa ya BAE System ikikiri mahakamani kwamba ilifanya makosa ya kutoweka kumbukumbu za kiuhasibu tu, hivyo kuamua kulipa fidia kwa nchi iliyokuwa imefanya nazo biashara ikiwamo Tanzania, Saudi Arabia na Marekani.

“Sasa aliyekuwa anatuhumiwa kwa rushwa amekataa kuhusika na rushwa, amekiri kosa la kiuhasibu la kuweka hesabu vibaya, hapa unamshitaki vipi mtu wakati kampuni yenyewe (BAE) haipo,” alihoji Rais Kikwete na kuongeza:

“Hata jaji (wa Kiingereza) aliyeamua kesi hiyo hakufurahishwa na utaratibu uliotumika.”

Tanzania iliuziwa rada ya bei mbaya ya Sh. bilioni 70 wakati huo na baada ya sekeseke kubwa BAE waliamua kuirejeshea Tanzania Sh. bilioni 72 za fedha zilizobatizwa jina la chenji ya rada, ilhali watu wengine wakisema si chenji ila ni rushwa ya rada.
 
Hawa viongozi hawajui madhara ya kutotenda haki wala kuwajibika! Kama wanataka kujua, ngoja hii vita ya malawi ikolee then waanze kuomba watu wajitolee kwenda kupigana. Yanaua uzalendo, yanaigawa nchi na kuna kipindi baadhi ya sehemu zitaanza kudai fidia ya kuibiwa rasilimali kutokana na serikali kutoziendeleza.
 
Maneno yako mazito,umeandika ukiwa na Hisia kali..mi nipo natetemeka hapa nilipo....!
"vox populi,vox dei"
 
Kiukweli inaumiza sana....viongozi wanapojifanya kuwa ni Nyeupe wakati watanzania tunaona ni Nyeusi
 
Udhaifu wa serikali yetu kiasi hicyo umezidi kiwango. Kama hakukuna na makosa katika bidhaa ya kununua rada serikali ya Uingereza imesimamia wapi kuishtaki kampuni iliyouza rada?

Kamanda Lema yuko kule sasa anafuatilia, ameonana na meya wa jiji, atakaporudi na kuanza mikutano ya hadhara serikali sijui itaficha wapi maovu yako.
 
Safi sanaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!

Mafisadi wanajifanya ndio viongozi,hakika mwisho wao waja!
 
Huu ni ushahidi mwingine kuwa ima serikali ya Kikwete ni ya kifisadi au iko mifukoni mwa mafisadi. Ni aibu kwa watu kama Chenge na Lowassa kuwa wenyeviti wa kamati za bunge. Wana udhu na jipya gani la kuwatendea wananchi iwapo tamaa yao imeuponza umma wetu? Je haya ndiyo matokeo ya uswahiba wa Kikwete na Lowassa au mchango wa Chenge kuasisi na kuidhinisha wizi wa EPA uliomweka madarakani Kikwete? Shame on you all! Hata hivyo kwa bunge lenye kujaa wabunge wanafiki na wala rushwa tutegemee nini?
 
Naona watawala wetu hawasomi hata historia!Kweli wamaikumbuka empire ya Songhai?
 
Wenje(1).jpg

Ezekia Wenje

‘Aibu walarushwa wa rada kuongoza kamati Bunge’

Mzimu wa kashfa ya rushwa ya ununuzi wa rada ya kijeshi ambayo Tanzania iliinunua kutoka Uingereza umeibuka kwa mara nyingine bungeni, baada ya wabunge wa Kambi ya Upinzani kuchachamaa na kutaka waliohusika na ununuzi wa rada watajwe na kuchukuliwa hatua za kisheria.

Wabunge hao walikuwa wakichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa iliyowasilishwa na Waziri Bernard Membe.

Msemaji wa Wizara hiyo, Ezekia Wenje (Chadema-Nyamagana), alihoji: “Tunaendelea kuhoji kwa nini mpaka sasa watuhumiwa wa kashfa hiyo wanaendelea kutembea kifua mbele dhidi ya serikali bila hatua zozote kuchukuliwa?.”

Alisema hadi sasa haieleweki ni kwa sababu gani Tanzania pamoja na kudai kuwa ina uhuru wa kujiamulia mambo yake yenyewe iliamua kuliachia suala hili kufanyiwa kazi na Serikali ya Uingereza, kuanzia uchunguzi hadi kurudishiwa fedha zilizotokana na rushwa ya rada, ambazo kwa sasa zimebatizwa jina tamu la ‘chenji ya rada.’

“Katika hali inayoonesha kuwa baniani mbaya kiatu chake dawa, pamoja na serikali hii kushindwa kufanya uchunguzi na hatimaye kuwashtaki watuhumiwa wa rada, bado ilipobainika mahakamani kuwa tunatakiwa kurudishiwa chenji iliyotokana na rushwa, serikali ilikuwa mstari wa mbele kwelikweli katika kufuatilia chenji ya rada na katika kuipangia matumizi,” alisema na kuongeza:

“Tunashindwa kuelewa umakini wa serikali hii uko wapi kwamba inaweza kuweka msisitizo pekee katika kuhakikisha fedha za rushwa ya rada zinarejeshwa nchini, lakini haiwezi kuthubutu kabisa kushughulikia wale waliosababisha upotevu huo wa fedha za nchi kwa njia ya mikataba.”

Alihoji usikivu wa serikali ambayo pamoja na kelele zote za wananchi walioiweka madarakani kutaka watuhumiwa ufisadi kupimwa kwa kipimo kile kile katika mizani ya sheria na utoaji haki kama wanavyofanyiwa Watanzania wengine wanyonge.

“Bado serikali imetia masikio pamba na kufumba macho yake kwa mikono, kwamba haiwaoni mafisadi hao wala haisikii kelele za wenye nchi. Taarifa mbalimbali zinazotokana na utafiti na uchambuzi wa kina, zimeweka wazi wahusika wa kashfa ya ununuzi wa rada, zikieleza mchakato mzima namna wizi huo ulivyofanyika,” alisema na kuongeza:

“Ukiwahusisha Watanzania wengine wakiwa ni viongozi waandamizi wa serikali ya CCM na sasa Watanzania wanashangaa kuona watuhumiwa hao hao waliopaswa kuwa mikononi mwa sheria, sasa wanachaguliwa kuongoza mhimili muhimu wa Bunge! Kambi Rasmi ya Upinzani tunahoji je, hii ni dalili ya kuwa dola imetekwa na mafisadi?.”

Ingawa Wenje hakuwataja watuhumiwa hao kwa majina, lakini mmoja wa watuhumiwa hao anayeongoza moja ya kamati za Bunge ni Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge, ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi.

Chenge wakati wa mchakato wa ununuzi wa rada hiyo kutoka Kampuni ya BAE Systems mapema miaka ya 2000, alikuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Chenge alikutwa na Dola za Marekani milioni moja katika benki moja iliyoko katika Kisiwa cha Jersey nchini Uingereza.

Hata hivyo, mara kadhaa Change amekuwa akikanusha kuhusika katika wizi wa fedha za rada hiyo na kudai kuwa Taasisi ya Kuchunguza Makosa Makubwa ya Udanganyifu ya Uingereza (SFO) ilishamsafisha.

Mbunge wa Viti Maalum, Rachel Masishanga (Chadema), aliitaka serikali kueleza ni kina nani waliohusika na kuibia serikali katika kashfa ya rada.

“Tumepata chenji ndio tuwajue ni kina nani waliohusika na kama anawafahamu kwa majina naomba leo hii awaambie Watanzania waliohusika kuiibia serikali katika suala hilo la rada,” alisema.

Mbunge wa Gando, Khalifa Mohamed Khalifa (CUF), alihoji: “Nyie ndio mnatuletea wawekezaji, lakini nyie ndio mnapaswa kuangalia huko nje maslahi ya taifa. Wewe ni mwanadiplomasia namba mbili, wa kwanza ni Rais na wewe mwenyewe uliwahi kufanya kazi katika balozi, hivi kweli unataka kutuambia hujui watu wanaotuibia fedha zetu?” alisema na kusisitiza:

“Kweli hujui, hivi kweli hujui wawekezaji matapeli ukatuambia unaruhusu wanakuja tu hapa kila siku vinasemwa vitu hivi na watu wanafanya utafiti, hii ni aibu kubwa sana, hatuwezi hata siku moja tukavumilia nchi inadhalilishwa na watu na nyie nawajua mnawanyamazia, utakapokuja kufanya majumuisho utawatajia Watanzania,” alisema.

Alisema hata kama yeye (Khalifa) yumo katika orodha ya watu hao waliohusika na rushwa Membe amtaje.

Akijibu katika majumuisho ya hotuba ya Waziri Membe jana jioni, Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe, alisema hakuna mtu yeyote kutoka Tanzania ambaye anaweza kushtakiwa mahakamani kwa mashitaka ya rada.

“Kama kuna mtu yeyote ndani ya Bunge ama nje ya Bunge mwenye ushahidi juu ya mtu yeyote kama walimpiga picha ama mlikuwa naye atuletee huo ushahidi na tutapeleka mahakamani,” alisema.

Alisema jana asubuhi alizungumza na Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP), Eliezer Feleshi pamoja Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk. Edward Hoseah, ambao walisema hakuna kitu kipya na wala hawafanyi uchunguzi kuhusu sakata la rada.

Wiki iliyopita, Rais Kikwete, alisema hakuna mtuhumiwa katika sakata ya rushwa na kwamba walioanzisha suala hilo ni SFO.

Rais alisema baada ya kuwahoji maofisa hao, SFO walirudi Uingereza na kukaa kwa muda mrefu pasipo taarifa yoyote, lakini walishangaa kusikia kwamba kampuni iliyokuwa imetuhumiwa kwa rushwa ya BAE System ikikiri mahakamani kwamba ilifanya makosa ya kutoweka kumbukumbu za kiuhasibu tu, hivyo kuamua kulipa fidia kwa nchi iliyokuwa imefanya nazo biashara ikiwamo Tanzania, Saudi Arabia na Marekani.

“Sasa aliyekuwa anatuhumiwa kwa rushwa amekataa kuhusika na rushwa, amekiri kosa la kiuhasibu la kuweka hesabu vibaya, hapa unamshitaki vipi mtu wakati kampuni yenyewe (BAE) haipo,” alihoji Rais Kikwete na kuongeza:

“Hata jaji (wa Kiingereza) aliyeamua kesi hiyo hakufurahishwa na utaratibu uliotumika.”

Tanzania iliuziwa rada ya bei mbaya ya Sh. bilioni 70 wakati huo na baada ya sekeseke kubwa BAE waliamua kuirejeshea Tanzania Sh. bilioni 72 za fedha zilizobatizwa jina la chenji ya rada, ilhali watu wengine wakisema si
Tz wamelipa 70bil. Chenji ya 72bil.hapo sijakuelewa kwanin ivo
 
Haya haya mambo yao ndo yametuondolea mood wetu wa kuwa wazalendo, tunashindwa kulitetea taifa letu kwa mambo ya umimi.
 
Hivi visingizio vya namna hii vitatumika mpaka lini?
Serikali inategemea mahesabu yaliyopigwa na mtu mmoja? na baada ya huyo mtu mmoja serikali ikaenda na hiyo hesabu na kufanya matumizi ya bilioni 70? Kwa mahesabu ya mhasibu mmoja? Hii kitu hainiingii akilini.
Ile EPA pia alikuwa huyo huyo mhasibu mmoja? Jina lake nani huyu mhasibu ili utakapopatikana mwanya wa kumhoji aweze kuuambia umma ukweli wa hili jambo. Maana inavyoelekea alipewa maagizo siyo kwamba alikosea?

Watuwekee hadharani huo mkataba na hizo hesabu tuwafahamu walioweka sahihi ya kuidhinisha ununuzi huo. Haiwezekani ikawa ni mhasibu tu! Hapa yalitolewa maagizo ya nguvu kutoka juu kabisa.
Ili nchi iamue kutumia bilioni 70 ni lazima baraza zima la mawaziri lihusishwe pamoja na makatibu wakuu wote na waweka hazina, na Gavana. Kama haikutokea hivyo basi huu haukua ununuzi wa kiserikali ila ni wakubwa wachache waliamua kufanya "shopping" kwa makusudi.

Na hivi ndivyo tutaelewa sababu za kuwepo mamilioni ya dola yaliyofichwa Uswiss.
 
Maneno yako mazito,umeandika ukiwa na Hisia kali..mi nipo natetemeka hapa nilipo....!
"vox populi,vox dei"
Mkuu, viongozi wetu bado wako miaka 30 nyuma ya wakati tulionao sasa! Wanakera sana na hata wakifanya zile ziara sijui wanaenda kunywa pombe tu na kurudi. Kwa ufupi wanatumia vibaya madaraka. Watu tuko tayari kwa mabadiliko ya kiuchumi, kielimu na hata kitechnolojia lakini viongozi wanatuchelewesha. Anyway, tutaendelea kuwa soko la bidhaa, wateja wa technolojia na wafuata upepo tu.
 
Wenje NMB wanakukumbuka we acha tu! Turudi kwenye mada ujue tatizo letu wa bongo (na mimi nimo) we have our eyes wide open on issues but our hands are off! Ila kiundani hakuna mtu anechukua hatua, tunavizia nani atatuokoa!

Dawa ni kila mtu kuchukua hatua kwa wakati mmoja, mfano kwenye uchaguzi mkuu we unaona ndungu, jamaa hawaendi kupiga kura unaacha tu unaenda kupiga mwenyewe, sasa ndo matokeo, ikifika 2015 kila mtu akague, ahakikishe na kuchimba biti yeyote alie na umri wa kupiga kura aende, na unahakikisha mgombea unaemkubali unamsaidia campeni kwa wale watu undecided unawachota wote, namna hiyo hata wabunge wataogopa kutuvuta sharubu zetu
 
Njia pekee ya kujinasua na huu uongozi dhalim mno ni kutoa elimu kwa umma kwa kuwapa taarifa zote hizi jinsi serikali ya CCM inavyorudisha wananchi nyuma na kutuacha tuteseka kiasi hiki. Elimu hii iambatane na umuhimu wa kujiandikisha na kupiga kura mapema kabla ya 2015 ili muda ukiwadia wananchi tuwe tayari kuwaondoa CCM madarakani kwa njia ya kura. Viongozi gani hawa wasiokuwa na aibu kutuhadaa kiasi hik?
 
SERIKALI imeelezwa kuwa imeamua kutofungua mashtaka dhidi ya vigogo wanaodaiwa kuhusika katika kashfa ya ununuzi wa rada kwa madai kuwa kesi hiyo ingemgusa mmoja wa marais wastaafu, na watu wa karibu wa Rais Jakaya Kikwete, imefahamika.
Taarifa kwamba serikali imekacha kufungua mashitaka kwa lengo la kuwalinda vigogo, mara ya kwanza iliibuliwa na mtandao maarufu wa Wikileaks, ambao umekuwa ukifichua siri nzito katika duru za kiserikali, kidiplomasia na kisiasa katika nchi nyingi duniani. Mchakato wa ununuzi wa rada hiyo iliyouzwa kwa bei ya kuruka ya sh bilioni 40, uliwahusisha watu wa madaraka na kada mbalimbali ambao ni pamoja na aliyekuwa Waziri Mkuu wa Uingereza, Tony Blair.

Blair anatajwa kuwa ndiye aliyemshawishi aliyekuwa Rais wa Tanzania wakati huo, Benjamin Mkapa, kununua rada hiyo kutoka Kampuni ya kutengeneza silaha ya Uingereza, BAE-Systems wakati aliyekuwa Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa, Clare Short, alikataa katakata, na hata kumshauri Rais Mkapa kwamba Tanzania ni moja kati ya nchi masikini duniani, isingekuwa busara kutumia sh bilioni 40 kununua rada katikati ya umasikini unaonuka.

Mwingine anayetajwa kuishauri vibaya Serikali ni Mbunge wa Bariadi Mashariki, Andrew Chenge (CCM), ambaye kwa muda mrefu amekuwa akitajwa ndani na nje ya chama chake kuhusika na kashfa ya ununuzi wa rada kutoka Kampuni ya BAE- System ya nchini Uingereza.

Chenge, ambaye kwa sasa ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Fedha na Uchumi, anatajwa kuhusika kutoa ushauri wa kisheria wakati huo akiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, ushauri ambao unatajwa kuzingatiwa katika hatua za uamuzi.
Mwingine anayehusishwa na kashfa hiyo ni aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu (BoT), Dk. Idriss Rashid.

Pamoja na hao, wanatajwa wafanyabiashara wenye asili ya India, lakini ambao wanaishi/walipata kuishi Tanzania, Tanil Somaiya, ambaye alikuwa akimiliki kampuni ya uwakala wa simu ya Shivacom na Sailesh (Shailesh) Vithlani kuwa watu wa kati wa biashara hiyo.

Pamoja na wahusika walioliingiza mkenge taifa kujulikana, Rais Kikwete na Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe kwa nyakati tofauti wametoa msimamo wa serikali.
Rais Kikwete katika mkutano wake na wahariri wa vyombo vya habari, alisema kuwa serikali yake haiwezi kumfikisha mahakamani mtu yeyote kwa vile hakuna rushwa katika ununuzi huo, na badala yake kulikuwa na makosa ya uchapaji katika kuweka kumbukumbu za fedha na mahesabu.
Waziri Chikawe juzi na jana alisema serikali haiwezi kumfikisha mtu yeyote mahakamani katika kesi ya rada, kwani hakuna ushahidi hasa baada ya Serikali ya Uingereza kukataa kuja kutoa ushahidi.
Akijibu swali la Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (CHADEMA) jana bungeni, Chikawe alisisitiza kuwa serikali haina ushahidi wa kumshitaki mtu yeyote mahakamani kwa kashfa ya ununuzi wa rada.
Alisema kutokana na hali hiyo, iwapo kuna mtu yeyote mwenye ushahidi wa kuaminika ndani au nje ya nchi auwasilishe na kwamba wataweza kwenda mahakamani wakati wowote.
"Hili la rada, sina ushahidi, nilisema jana na nasema tena leo ndani ya Bunge hili kama yupo mtu, nje ya Bunge hili mwenye ushahidi ambao ni ‘credible' wa kumshitaki mtu yeyote ambaye ni Mtanzania, tutamchukua mtu huyo na kwenda naye mahakamani kesho," alisema Waziri Chikawe.
Katika swali lake la msingi, Mnyika alisema kwa kuwa kampuni ya Uingereza ya silaha za kivita (BAE Systems) ilishakiri makosa ya kutoweka kumbukumbu za fedha na mahesabu katika mchakato wa mauzo ya rada kwa Serikali ya Tanzania, ni dhahiri kuna makosa yalifanyika ya kimanunuzi kati ya pande zote mbili, hali iliyosababisha kuwapo kwa tozo ya pauni milioni 29.5 kama fedha zilizochukuliwa na BAE Systems, hivyo wahusika wachukuliwe hatua.
Pia alihoji serikali imewachukulia hatua gani waliohusika na mchakato wa ununuzi huo kwa upande wa Tanzania.
"Katika hali kama hii tukichukua mtu na kumpeleka tutapata wapi ushahidi na tunaowategemea ni BAE na SFO ambao sasa kule hata kumtaja mtu hauruhusuwi. Na katika ushahidi ni lazima kuwapo na mtoaji na mpokeaji," alisema.
Wakati serikali ikisema Uingereza imekataa kutoa ushahidi kwa vile hakuna rushwa, Bunge la nchi hiyo hiyo liliwahi kuitaka Serikali ya Tanzania iwafikishe mahakamani wote walioshiriki katika ununuzi wake na kuiingiza nchi katika hasara ya mabilioni ya fedha.
Kupitia kamati yake ya Maendeleo ya Kimataifa, Bunge hilo limesema lingependa kuona watu wote walioshiriki katika mchakato wa ununuzi wa rada hiyo wakifikishwa mahakamani kujibu tuhuma za ufisadi.
Taarifa ya kamati hiyo iliyonukuliwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), ilieleza kwamba wajumbe wake ambao ni wabunge kutoka vyama mbalimbali nchini humo, walisema watatoa ushirikiano wa dhati kwa Tanzania iwapo itaamua kuwashtaki watuhumiwa hao nchini Tanzania au Uingereza.
Kwa mujibu wa BBC, wabunge hao wamesema, mbali na kurudishiwa fedha iliyozidi kwenye ununuzi huo unaosemekana ulitawaliwa na rushwa, Serikali ya Tanzania inapaswa kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wote haraka iwezekanavyo ili haki itendeke.
Namna walivyochota mamilioni
Kwa mujibu wa rasimu ya ripoti ya SFO (Taasisi ya Uchunguzi Makosa ya Jinai ya Uingereza), Chenge alipokea malipo ya jumla ya dola za Marekani milioni 1.5 (zaidi ya sh bilioni 1.5) kati ya Juni 1997 na Aprili 1998 kutoka Benki ya Barclays, tawi la Frankfurt.
Fedha hizo zililipwa katika benki ya Barclays huko Jersey - Uingereza, katika akaunti inayomilikiwa na kampuni iliyotajwa kwa jina la Franton Investment Limited. Kampuni hiyo imetajwa kumilikiwa na Chenge, ikiwa ni maalumu kwa ajili ya uhamishaji fedha kiasi cha dola za Marekani 600,000 (zaidi ya sh milioni 600).
Dola hizo 600,000 za Marekani zilihamishwa kutoka kwenye akaunti ya kampuni ya Chenge kwenda kwenye akaunti nyingine, inayomilikiwa na Kampuni ya Langley Investments Ltd, iliyokuwa ikiendeshwa na Dk. Idriss (aliyewahi pia kuwa Mkurugenzi wa TANESCO).
Septemba 20, mwaka 1999, Chenge binafsi aliidhinisha uhamishaji wa dola za Marekani milioni 1.2 (zaidi ya sh bilioni 1.2) kutoka akaunti ya Kampuni (yake) ya Franton kwenda Royal Bank of Scotland International, huko Jersey.
 
Kwakuangalia vitu kama hivi, basi itakuwa ngumu kujitoa kwenye lindi la UFISADI. Ninaimani udhaifu huu si wa KIKATIBA, bali ni watendaji wetu wanaogopa na wao watakapotoka madarakani wafanyiwe favour kama hizi. Katika SERIKALI safi, maslahi ya TAIFA ndiyo huwa nguzo ya kila kitu.
 
Mbaya zaidi Mkuu wa nchi badala ya kuwachukulia hatua anawatetea wezi, eti kwa sababu kuna maswahiba! hii inamaana hata yeye anahusika kwa sehemu kubwa!
 
Back
Top Bottom