Bungeni: Joseph Musukuma asema ana majina ya wabunge wa upinzani waliohongwa kuitetea ACACIA

ZionTZ

JF-Expert Member
Oct 6, 2009
1,283
541
Kwa kipindi kifupi kilichopita bunge letu lilianza kurudi kwenye misingi ya kizalendo, ila tokea hii budget ya madini ianzwe kusomwa vijembe,majigambo,maneno ya kuudhi,kejeli zimerejea mahali pake.

Leo kwa mara nyingine mbunge wa Geita, mh Msukuma aliomba dakika za nyongeza kutoka kwa Hawa Ghasia na kuwashambulia wabunge wa upinzani badala ya kuzungumza hoja. Mh. Msukuma alisema wapinzani wamehongwa na anawajua ingawa hakuwataja, pia akasema Msigwa anamiliki nyanya,kuku na mbwa hawezi jua mambo ya madini kama vile haitoshi akamrudia Mnyika kwamba anamiliki mchanga wa matofali.

Tizama mwenyewe.

 
naunga mkono hoja,chadema walisaini miktaba ya kipuuzi sana na wameiweka nchi yetu pabaya sana sasa wanatokea wabunge wazalendo,wapambanaji wenye IQ kubwa kama kasjeku msukuma wanapambana ili tufaidike na rasilimali zetu zilizouzwa na chadema halafu akili ndogo kama za lissu na mnyika zinabisha
 
Kwa kipindi kifupi kilichopita bunge letu lilianza kurudi kwenye misingi ya kizalendo, ila tokea hii budget ya madini ianzwe kusomwa vijembe,majigambo,maneno ya kuudhi,kejeli zimerejea mahali pake...leo kwa mara nyingine mbunge wa geita mh msukuma aliomba dakika za nyongeza kutoka kwa hawa ghasia, na cha akapatiwa dk 10 ndipo alipoanza kuattack wabunge wa upinzani badala ya kuzungumza hoja, mh. msukuma alisema wapinzani wamehongwa na anawajua ingawa hakuwataja, pia akasema msigwa anamiliki nyanya,kuku na mbwa hawezi jua mambo ya madini kama vile haitoshi akamrudia mnyika kwamba anamiliki mchanga wa matofali...tizama mwenyewe.


Mbona umeiandika kishabiki?
 
Mchungaji Msigwa akiwa katika umiliki wa NYANYA. Halafu inabidi achukuliwe hatua kwa kuvunja sheria za nchi. Hao watoto anaowatumikisha inabidi wawe shule na sio kuwa cheap labour.

1479932444478.jpg
 
naunga mkono hoja,chadema walisaini miktaba ya kipuuzi sana na wameiweka nchi yetu pabaya sana sasa wanatokea wabunge wazalendo,wapambanaji wenye IQ kubwa kama kasjeku msukuma wanapambana ili tufaidike na rasilimali zetu zilizouzwa na chadema halafu akili ndogo kama za lissu na mnyika zinabisha
dongo hilo au???
 
Hili jambo ccm wanalichukulia kwa mzaha kama walivyofanya kusaini mikata kwa mzaha. Huu ndio wakati ambao ccm wanapaswa kuungana na wapinzan ili waangalie namna ya kujitoa ktk makucha ya unyonyaji wa mali zetu. Lakin jambo la kushangaza haohao ccm wanaamin upnzan wamehongwa wakat wapinzan wanakosoa approach mbovu znazotumiwa kutatua tatzo lenye kuleta matatzo makubwa.
 
Back
Top Bottom