BUNGENI, DODOMA: Tanzania Bara hakuna uhaba wa Sukari! Ushuru wa 100% wa sukari kutoka nje unasababisha ipande bei

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Aug 22, 2012
2,036
3,929
Waziri wa viwanda, biashara na uwekezaji Charles Mwijage, amesema leo Bungeni kuwa kwa vigezo vyovyote vya kupima uhaba wa bidhaa sokoni, Tanzania bara hakuna uhaba wa sukari

Aidha ameeleza kuhusu tofauti ya bei ya sukari katika pande mbili za muungano kuwa ni zaidi ya 53% ya sukari itumikayo Zanzibar huagizwa kutoka nje kwenje vyanzo ambavyo gharama zake ni nafuu ukilinganisha na 29% zinazoagizwa kwa upande waa bara kujaza mapungufu ya uzalishaji

Kwa Upande wa bara na nchi nyingine za Afrika Mashariki hutozwa ushuru wa 100% ili kulinda viwanda vya ndani. Kutokana na sababu hizo bei ya sukari huweza kutofautiana

Serikali imechukua hatua ya kusimamia kampuni kubwa nne zinazozalisha sukari ili ziwekupanua mashamba na uzalishaji, zoezi ambalo linakwenda vizuri ambapo Kilombero sugar wameongeza uzalishaji maradufu kwa kuwekeza dola milioni 200

Mtibwa sugar kwa kuwekeza Tsh. Bilioni 75 wataongeza uzalishaji kwa kipindi cha miaka mitano kutoka tani 30,000 na kufikia tani 100,000. Kagera sugar wanawekeza Tsh. Bilioni 360 ili kwa kipindi cha miaka mitano waongeze uzalishaji kutoka tani 75,000 mpaka tani 175,000

Aidha Waziri Mwijage amesema serikali kwa nyakati tofauti imekuwa ikishusha ushuru au kutoa kabisa ushuru ili kutoa nafuu ya bei kwa watumiaji sukari, kuanzia mwezi Machi mpaka Juni mwaka huu serikali imetoa vibali kwa wadau mbalimbali kuagiza sukari kwa kutoa ushuru wa 25% badala ya 100%

Waziri Mwijage amesema hayo wakati akijibu swali linaulizwa na Mhe. Jaku Hashim Ayoub Mbunge wa baraza la Wawakilishi. Alilouliza Kuna tatizo gani linalofanya sukari iweze kuuzwa bei ya juu kwa tanzania bara na serikali inachukua utaratibu gani kuweza kuwasaidi wananchi katika upatikanaji wa bidaa hiyo

Hata hivyo Spika wa Bunge ameyakataa majibu ya Waziri Mwijage na kusema Bunge linahitaji majibu ya uhakika hivyo swali hilo kuhusu Sukari litaulizwa wiki ijayo ili Serikali ije na majibu ya Uhakika
 
Majibu ya hawa watu sometimes ukiwasikiliza unapata hasira.
Sema basi tu unavumilia kwakuwa hakuna namna hata uvimbe upasuke hawajali ukivimba sana wanakutumia polisi.
 
Back
Top Bottom