BUNGENI, DODOMA: Gesi asilia kuanza kutumika majumbani kuanzia mwezi Julai mwaka huu

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,253
BUNGE LA 11 LA JAMHURI YA MUUNGANO
MKUTANO WA SABA-KIKAO CHA PILI
MASWALI NA MAJIBU

Swali:
Ni lini ujenzi wa chujio na usambazaji wa maji katika mji wa Mgumu utakamilika?

Majibu:
Utakamilika ifikapo mwezi Juni 2017

Swali: Serikali ina mpango gani kuhakikisha miradi ya maji inayojengwa katika wilaya ya sengerema inakamilika kwa wakati?

Majibu: Miradi bado inaendelea na punde itakapokamilika itahudumia wananchi wengi wa vijiji vya wilaya hiyo.

Swali: Je ni lini serikali itasitisha usafirishaji wa gesi toka Mtwara kwenda Kinyerezi?

Majibu: Sera ya gesi inalenga kutoa fursa kwa watanzania wote. Kwa sasa TPDC inaunganisha gesi hii majumbani pia inaunganisha, imefikia makubaliano na kiwanda cha Dangote kuunganisha gesi hii. Aidha TPDC ipo katika mazungumzo ili kuunganisha katika kiwanda cha Lindi.

Aidha serikali kupitia TPDC iko katika mazungumzo ya kuunganisha gesi katika kiwanda cha mbolea cha Mtwara. Pia TPDC ipo katika mchakato wa kuunnganisha gesi majumbani kwa wakazi wa Dar na Mtwara.

Swali: Tatizo ni nini kukatika kwa umeme katika mikoa ya Mtwara na Lindi?

Majibu: Unatokana na ubovu wa jenereta moja kati ya 9. Pia ubovu wa njia ya kusafirisha umeme.
Aidha serikali inaboresha mtambo wa kuzalisha umeme ili kukabiliana na tatizo hili.
TANESCO itanunua majenereta sita ili kukabiliana na tatzio hili.

Swali: Serikali haioni ipo haja kodi ya PAYE na ya kampuni zote za zanzibar zikusanywe na serikali ya Muungano kama serikali walivyokubaliana?

Majibu: Kodi za kampuni zinakusanywa na serikali ya Muungano.

Swali: Ni lini mradi wa umwagiliaji ya Ikwea utakamilika?

Majibu: Serikali ilitenga milioni 435.6 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo. Hata hivyo kulikuwa na marekebisho ambayo yalihitaji kufanyiwa kazi.

Bado serikali haiwezi kutoa jibu la moja kwa moja kwamba ni lini mradi huo utakamilika ila mradi utaanza mwezi nne. Na katika kipindi cha miezi kumi na mbili mradi kasoro zilizokuwepo zitakuwa zimerekebishwa.

Swali la nyongeza: Serikali ina mpango gani wa kuwachukulia hatua waliofanya ubadirifu miradi?

Majibu: Serikali inakagua miradi yote na ikibainika kuna ubadirifu wowote, hatua stahiki zitachukuliwa

Swali: Wakala wa misitu wamehamisha vijiji vilivyokuwepo toka mwaka 1974 katika hifadhi ya Gheita, serikali inatoa kauli gani?

Majibu: Mwaka 1974 serikali ilifanya mapitio ya mpaka wa msitu, na iligundulika kuwa mpaka huo umepita katikati ya vijiji. Mpaka sasa serikali ipo katika mjadala wa kuangalia namna ya kutatua mgogoro huu bila kuleta athari kwa walengwa.

Suala hilo limefikishwa katika kamati ya ushauri ya mkoa na jambo hili bado lipo katika mazungumzo. Aidha serikali inawataka wananchi wa maeneo hayo kuondoa mifugo katika eneo hilo kabla serikali haijachukua hatua za kisheria stahiki.

Serikali imetoa taarifa kuwa gesi asilia itaanza kutumika kwa matumiazi ya majumbani kuanzi mwezi Julai mwaka huu.
 
Mi sijui nina matatizo ya macho au lakini naona majibu yapo sawa na maswali yalii ulizwa.. Sasa sijui maswali magumu na majibu maraisi yapojee
 
Kutoka Bungeni mjini Dodoma Serikali imetoa taarifa kuwa gesi asilia itaanza kutumika kwa matumiazi ya majumbani kuanzi mwezi Julai mwaka huu.
 
Kweli! Mwanzoni tuliambiwa gesi ya Songosonga ilikuwa ni suluhisho la kila kitu na baadaye tukaambiwa ikifika ya Msimbati umeme utashuka kwa 50%! Bado tupo tunang'aa ng'aa macho.
 
Back
Top Bottom