Bungeni Dodoma: Gari kuukuu lazusha tafrani bungeni

Bungeni Dodoma: Gari kuukuu lazusha tafrani bungeni

Mandla Jr.

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2013
Posts
3,098
Reaction score
631
Maofisa usalama wa Bunge wakishirikiana na Jeshi la Polisi jana saa 3:40 asubuhi walilizingira gari moja la Serikali lililokuwa limeegeshwa ndani ya eneo la Bunge.
Gari hilo ambalo linaonekana kuwa chakavu kiasi, aina ya Toyota Prado lilizingirwa na maofisa hao ambao walilizungushia kamba maalumu za njano zenye maandishi ‘Crime Scene' yakimaanisha ni eneo la tukio la jinai.

Kamba hizo zimekuwa zikitumiwa na Jeshi la Polisi kuzuia watu wasiohusika na masuala ya kiusalama kusogelea eneo hilo ili kutoa fursa kwa wataalamu kufanya uchunguzi ikiwamo kuchukua sampuli.

Mwandishi wetu aliwashuhudia maofisa hao wakitumia mbwa weusi kulikagua gari hilo.

Hata hivyo, haijafahamika ilikuwaje gari hilo kuwa eneo hilo ambalo hutumika kwa maegesho ya magari binafsi ya wabunge na viongozi na huduma za kibiashara.Kwa utaratibu, magari yote yanayoingia ndani ya viwanja vya Bunge hufanyiwa ukaguzi maalumu na mitambo iliyopo katika mageti.

Wakati wa ukaguzi huo, maofisa hao walianza kutoa amri kwa watu waliokuwa karibu na eneo hilo, wakiwamo wanahabari kuondoka.

"Tunawaomba muondoke eneo hili kwa sababu kuna shughuli maalumu tunaifanya," alisema ofisa mmoja.

Habari ambazo hazijathibitishwa zilieleza wakati wa ukaguzi huo, maofisa hao waliokota kitu kisichojukana na kukichukua kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma ambaye pia alikuwa katika eneo la tukio, David Misime alisema baadaye kuwa hajui chochote kuhusu jambo hilo.

Source: Mwananchi.

Mandla.
 
Kamanda wa Polisi anapokuwa muoga....
 
Hivi vikundi vya kiislam vimekuwa hatari kwa dunia kutokuwa mahala salama pa kuishi
 
waliokota kitu kisicho julikana hii policcm inatabu.
 
wapeleke kile kikosi cha kuvunja matofali jamani
 
huyo mwandishi weni alishindwa kulipiga hata picha au alikuwa na simu ya nokia tochi
 
....wakati wa ukaguzi huo,
maofisa hao waliokota kitu
kisichojukana na kukichukua
kwa ajili ya uchunguzi zaidi....
wakati huo mwandishi akishuhumia. picha?
 
uoga tu unawasumbua,kwanza wabunge wetu hawa wa mipasho hata wakiripukiwa na kiripuzi sidhani kama taifa litakuwa limepata hasara kwani tutapeleka majembe mengine yenye uchungu na nchi yetu!
 
Hivi vikundi vya kiislam vimekuwa hatari kwa dunia kutokuwa mahala salama pa kuishi

Vikundi vya kiislamu vinahusika vipi na hilo gari chakavu hapo Dodoma?
Mijitu mengine ubongo wao umeungana ni mishipa ya mavi!
 
Wapo kwenye maandalizi ya kupandikizia mtu, chama cha siasa au viongozi wa kisiasa kesi za uzushi na kutafuta sababu kuweka wazushiwa vizuizin.
 
Hivi vikundi vya kiislam vimekuwa hatari kwa dunia kutokuwa mahala salama pa kuishi

Wewe kichwa lako ni sawa na ng'ombe, haliwazi mambo ya msingi wewe kila kinachoandikwa humu jf comment zako ni waislamu tu, pumbafu sana wewe
 
Kweli vikundi vya kiislam vina shida sana. Ona wanavyopeleka mabomu makanisani mbona hatusikii kuhusu misikitini?Ila ingekuwa vema wakalipue bunge la katiba hapo nitawapongeza mno!
 
Back
Top Bottom