Bunge mzigo namba moja Tanzania

Bunge mzigo namba moja Tanzania

ego

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2013
Posts
1,620
Reaction score
1,408
Kwa tanzania yetu mzigo namba moja unaotunyima maendeleo ni bunge letu. Bunge ndio chombo cha kusimamia na kushauri serikali lakini chombo hiki hakitambui wajibu na mamlaka yake.

Malaka ya bunge juu ya serikali ni sawa na jinsi bodi ya kampuni inavyosimamia utendaji wa kampuni au unavyoweza kuwa unajenga nyumba yako ukamtafuta mtaalamu kusimamia na kumshauri mkandarasi "contractor" kukujengea nyumba yako.kitakuwa ni kituko umemuweka mtaalamu asimamie na kushauri ujenzi wa nyumba yako ukute anamwambia mjenzi kuwa "mimi mweshimiwa injinia nilikuwa nafikiri hapa ukuta mngeunyoosha na simenti msiweke mchanga mwingi lakini mimi naunga mkono ujenzi wenu mia kwa mia"msimamizi sahihi ambaye siyo mzigo wa ujenzi ya nyumba yako kwanza anamuomba mjenzi ampe aina ya vifaa anavyotaka kuvitumia ili aangalie ubora na kutoa ruhusa, wakati wa ujenzi akikuta ukuta umepinda kidogo anamwambia mjenzi bomoa ujenge ulionyooka, sementi kidogo mchanga mwingi anasema hiyo mwaga lazima uweke uwiano unaokubalika.

Bunge letu linaendeshwa kama debate za sekondari "upande unaopinga na upande unaosapoti mada", bado hawajui wanachokifanya maana maana ya bunge haijulikani maana si wawakilishi wa wananchi kusimamia serikali bali limegeuka uwanja wa mabishano wa vyama vya siasa.kama tunataka maendeleo kila mbunge chama chake kibaki mlangoni wabunge wote wanakuwa kambi moja na serikali inayohojiwa kambi nyingine lakini mkubwa pale ni bunge "hapa lijitambue kuwa lina wajibu wa kurekebisha upuuzi wa serikali"mfano kuna tabia ya mawaziri kupeleka fedha za maendeleo katika maeneo kwa upendeleo hasa majimbo yao, kwa mfumo holela tulionao kila atakayeingia atafanya hivyo. Bunge ndio chombo cha kwanza kuondoa upuuzi huu kwa kutumia njia kama hii.

Kwanza mnaagiza serikali kuweka malengo ya kitaifa ya maendeleo kama kufikia mwaka fulani tunataka huduma ya maji mijini kufikia asilimia fulani na vijini kufikia asilimia fulani.sasa takwimu za taifa zima kuangalia kila wilaya imefikia asilimia ngapi ya utekelezaji wa mpango huo wa taifa, vinaaandaliwa vigezo vya utekelezaji mfano kipaumbele kinawekwa kwa wilaya ambazo bado ziko chini na miradi ya kuchochea uchumi kitaifa. Waziri anapoleta bajeti yake ni kuangalia kama yuko katika kutekeleza mpango wa maendeleo wa taifa na fedha anazigawa kwa vigezo.ni upuuzi mtupu kuona mbunge anasiamama na kudai kama kujiji fulani hakitegewi fungu anatoa shilingi wakati huo pengine wilaya yake imevuka lengo na sehemu ambayo wako chini kabisa ya malengo tena hawapewi nafasi kuchangia katika hiyo mada.

Ili kusimamia serikali lazima bunge liwe na sauti moja ya wananchi na sio vyama vya siasa na liwe na kauli moja ya kuwa na nini waziri anatakiwa kufanya na kumpima kwa mapendekezo aliyoyaleta na yale aliyotakiwa kufanya sio kila mmoja huyu anatokea kilabuni, huyu anatokea kwenye biashara zake huyu anatokea sijui wapi wanakutana kujadili hoja za serikali kila mmoja anasema yake na mwisho hawana maamuzi.ni wapumbavu tu wanaoweza kusoma majukumu ya bunge kuwa ni kushauri wakaenda bungeni kusimama na kusema wanayofikiri kuwa kama wabunge wametimiza wajibu wao.

Wajibu wa mbunge si kusema anayowaza na kuyahalalisha kwa kutanguliza wananchi wangu wamenituma, bali lazima kuwe na mfumo rasimi wa kitakwimu kuonyesha mwenendo wa maisha ya watanzania na serikali inapanga nini na kutekeleza nini kuhusu maisha haya ya watanzania.hivyo kwa mbunge mambo muhimu ni takwimu za hali maisha ya watanzania, mipango ya maendeleo ya kitaifa, mipango ya mapato na matumizi, utekeleza wa mipango. Na mbunge anapokaa bungeni ni kujadili mambo ya kitaifa kwa maana ya kwamba unakuja na hali iliyoko jimboni kwako, zinalinganishwa na takwimu za kitaifa na hivyo utekelezaji wa serikali lazima ufuate malengo ya kitaifa na hali halisi.serikali inapokuja bungeni lazima kila waziri aambatane na watu muhimu katika wizara yake kila mmoja anajibu maswali katika eneo lake.

Haiwezekani bandarini kuna tatizo waziri hajui chochote yeye ndiye anakaa kujibu maswali hata mambo ya kweli anapinga kujilinda kwa nini mkurugenzi wa bandari asiwe pale na kama anamawazo bora ambayo waziri amekuwa hayapi kipaumbele kwa sababu mkurugenzi hajipendekezi kwake bunge linayapitisha pale pale na kama anamakosa ambayo yanaonekana hayamgusi sana waziri bunge linaagiza awajibishwe.
 
Na mzigo namba moja ni ujinga wa wananchi uliowaweka pale. Zama zile kulikuwa na harakati za kufuta ujinga ambao inaonekana umeamua kutia makao. Hadi ujinga utakapoondoka ndipo mambo yakwenda inavyotakiwa.
 
Mkuu umeongea jambo la maana sana. Ila ni aina moja tu ya ujinga uliotakiwa kufutwa wakati ule, yaani kusoma na kuandika, na si ujinga wa kufikiri.
 
Kuwa mbunge Tanzania nisawa na kujitia uwendawazimu,hii ni hasa pale ukiwa mbunge upande wa kutetea watawala.Hivi watu hawa wanamjua Mungu kweli?wanaishi nasi kweli au wanaishi ulaya na huja bungeni tu?
 
wanatumia maovu kuimarisha vyama maana upande mmoja wakimkemea muovu upande mwingine wanamtetea ili kuvuta wale wanaomsapoti katika chama chao. tutokomeze unafiki huu katika nchi yetu
 
Ama kwa hakika leo kidogo nna furaha,kile ambacho kimekua kikinikera mtoa mada amekizungumza,jaman bunge haliwatendei haki watanzania,wabunge wamesahau wajibu wao,wabunge wameshalizoea lile jengo ndo maana wanafanya upuuz,kwanza najiuliza iweje wabunge kila mwaka wawe wanafanyiwa semina za mambo yaleyale???na mbona mrejesho hawapelek kwa wananchi???,semina zinazoongoza ni za UKIMWI,UTAWALA BORA NA RUSHWA,wabunge kila mwaka wanaenda ughaibun kwenye ziara za mafunzo,jaman wanachojifunza kinatekelezwaje?,me binafsi kwa mtazamo wangu,taasisi hii na wanaounda hii taasisi ni wanyonyaji pia na wala hawapo kwa ajili yetu,inakera sana,tuje kwenye namna ya ujibuji wa maswal ya mawaziri kwa wabunge,nao pia wanajibu kizushi zushi tu,mawaziri wana viburi sana,wabunge kweli wanakubali kupitisha bajet za wizara ya afya na maji kwa ushabiki,au kwakua wao wanatibiwa India???,lakin wanaowapigia kura wanatibiwa huko???mzigo mwingine ni kwamba bunge letu wabunge wake wanalipwa mahela mengi sana ila kazi wanazofanya ni 'KUKAZANA'
 
Unga mkono UKAWA ili tupate katiba inayowakilisha matakwa ya wananchi. Haya yote unayoyazungumzia mwarobaini wake umo katika rasimu ya KATIBA YA WANANCHI ile iliyowasilishwa na Tume ya Warioba. Lakini CCM wana rasimu ya KATIBA YA KIKWETE inayotetea mambo yale yale, watu wale wale, ufisadi ule ule, nk
 
tukifanikiwa kuendelea na mchakato wa katiba inabidi tuubadili mfumo mzima wa bunge, ili liwe watch dog mzuri kwa serikali, tuunde mfumo wa bunge imara mathubuti, tufocus miaka 200 ijayo

1. tuwe na mabunge mawili bunge dogo(tanganyika) na bunge kubwa(tanzania)

2. waziri mkuu au raisi au gavana wa (tanganyika )vyovyote tutakavyomuita atawajibika bungeni
kwenye bunge dogo(congress)

3. makamu wa raisi wa tanzania ikibidi kama kuna issue nyeti raisi wa tanganyika atawajibika kwenye bunge kuu la Tanzania yaani (senete)

4. bunge kuu senete likae mara 2 kwa mwaka isipokuwa wakati wa dharula

5 bunge dogo (congress)likae mara 3 kwa mwaka isipokuwa wakati wa dharulla

4, tukubali tuwe na bunge ambalo ni kuu kuliko mihimili mingine yaan ( paliamentary supreme)

5.bunge likae mara tatu kwa mwaka lakini muda upunguzwe kuliko hivi sasa- kuwe na bunge la bajet pamoja na feedback ya utekelezaji wa bajet iliyopita tu bila maswali wala miswada - kuwe na bunge la kupitisha miswada ya sheria, kuuliza na kujibu maswali ya wananchi tu pamoja na hoja binafsi- kuwe na bunge maalumu la kubuni mikakati mikubwa ya kiuchumi na kisiasa na kuipangia serikali dira na malengo ya taifa tu. na kwa ajili ya utekelezaji tu,

-kwa mfano bunge likae mahususi, kujadili na kupanga mikakati ya ya kuhakikisha vyanzo yva mapato vinapatikana ili bajeti ijitosheleze bila ya kutegemea misaada

-bunge maalum linakaa kujadili jinsi ya kupata mkopo mkubwa kwa ajili ya kutandaza treni za umeme nchi nzima na njia njia za juu na chini ya aridhi

- bunge likanakaa kujadili uanzishwaji wa mradi mkubwa wa nuclear power plant kwa ajili ya kuzalisha umeme il kuuza nchi zote za kusini mwa afrika

katika bunge hili maalum wabunge wanaweza kuja ubunifu wa miradi mipango, mikakati mbali mbali wakifanikiwa kulishawishi bunge, likaridhia serilkali haina jinsi ni kutekeleza tu.

ingawa bunge ndio muhimili mkuu utashirikiana na serikali na mahakama vizuri, kiasi kwamba kama mfumo huu unatekelezwa si rahisi kujua ni muhimili gani ni supreme kwa kuwa mihimil yote ni kama kitu kimoja na interest yao no maendeleo ya nchi na si vininevyo
 
nadhani haya ni mawazo mazuri na vilevile kuna haja ya kuliwezesha bunge kufanya kazi yake vizuri. kimsingi bunge kwanza linawakilisha wananchi lakini pia linawajibu wa kufanya kazi za kupitia mapendekezo ya serikali. mitizamo hii miwili ni vigumu kuipata kwa pamoja hivyo kila bunge ni vema likawa na sura mbili. sura ya kwanza ni uwakilishi wa wananchi kwa maana ya watu kuchaguliwa katika majimbo yao. hapa ni vigumu kupata uwakilishi unaojumuisha utaalamu wa kuchambua mapendekezo ya serikali hivyo tunalazima kuweka ubunge wa aina ya pili wa ubunge wa kisekta. ni vema michakato ya kimaisha tukaigawanya katika sekta mbalimbali na kila sekta kuwa na wabunge wataalamu waliobobea na vijana ili kuchambua mapendekezo ya serikali na hao ndio wanakuwa mstari wa mbele kuwahoji wizara kuhusiana na mipango na utekelezaji wa kiufundi huku wawakilishi wa majimbo wao wakichangia kwa kuangalia yanayotekelezwa katika majimbo. Swala la kuweka wataalamu bungeni ni muhimu kuliko swala la jinsia tunalolikimbilia maana kama tuna kuwa na wanawake sawa na wanaume sawa bungeni huku madini, gesi, wanyama, misitu vikiendelea kuvunwa bila taifa kufaidika inatusaidia nini? tatizo kubwa la bunge hawajui wafanye nini ? mtu anafanya biashara ya nguo au ni mwalimu unampeleka ajadili muswada wa madini unategemea nini?
tukifanikiwa kuendelea na mchakato wa katiba inabidi tuubadili mfumo mzima wa bunge, ili liwe watch dog mzuri kwa serikali, tuunde mfumo wa bunge imara mathubuti, tufocus miaka 200 ijayo

1. tuwe na mabunge mawili bunge dogo(tanganyika) na bunge kubwa(tanzania)

2. waziri mkuu au raisi au gavana wa (tanganyika )vyovyote tutakavyomuita atawajibika bungeni
kwenye bunge dogo(congress)

3. makamu wa raisi wa tanzania ikibidi kama kuna issue nyeti raisi wa tanganyika atawajibika kwenye bunge kuu la Tanzania yaani (senete)

4. bunge kuu senete likae mara 2 kwa mwaka isipokuwa wakati wa dharula

5 bunge dogo (congress)likae mara 3 kwa mwaka isipokuwa wakati wa dharulla

4, tukubali tuwe na bunge ambalo ni kuu kuliko mihimili mingine yaan ( paliamentary supreme)

5.bunge likae mara tatu kwa mwaka lakini muda upunguzwe kuliko hivi sasa- kuwe na bunge la bajet pamoja na feedback ya utekelezaji wa bajet iliyopita tu bila maswali wala miswada - kuwe na bunge la kupitisha miswada ya sheria, kuuliza na kujibu maswali ya wananchi tu pamoja na hoja binafsi- kuwe na bunge maalumu la kubuni mikakati mikubwa ya kiuchumi na kisiasa na kuipangia serikali dira na malengo ya taifa tu. na kwa ajili ya utekelezaji tu,

-kwa mfano bunge likae mahususi, kujadili na kupanga mikakati ya ya kuhakikisha vyanzo yva mapato vinapatikana ili bajeti ijitosheleze bila ya kutegemea misaada

-bunge maalum linakaa kujadili jinsi ya kupata mkopo mkubwa kwa ajili ya kutandaza treni za umeme nchi nzima na njia njia za juu na chini ya aridhi

- bunge likanakaa kujadili uanzishwaji wa mradi mkubwa wa nuclear power plant kwa ajili ya kuzalisha umeme il kuuza nchi zote za kusini mwa afrika

katika bunge hili maalum wabunge wanaweza kuja ubunifu wa miradi mipango, mikakati mbali mbali wakifanikiwa kulishawishi bunge, likaridhia serilkali haina jinsi ni kutekeleza tu.

ingawa bunge ndio muhimili mkuu utashirikiana na serikali na mahakama vizuri, kiasi kwamba kama mfumo huu unatekelezwa si rahisi kujua ni muhimili gani ni supreme kwa kuwa mihimil yote ni kama kitu kimoja na interest yao no maendeleo ya nchi na si vininevyo
 
Kwa tanzania yetu mzigo namba moja unaotunyima maendeleo ni bunge letu. Bunge ndio chombo cha kusimamia na kushauri serikali lakini chombo hiki hakitambui wajibu na mamlaka yake.

Malaka ya bunge juu ya serikali ni sawa na jinsi bodi ya kampuni inavyosimamia utendaji wa kampuni au unavyoweza kuwa unajenga nyumba yako ukamtafuta mtaalamu kusimamia na kumshauri mkandarasi "contractor" kukujengea nyumba yako.kitakuwa ni kituko umemuweka mtaalamu asimamie na kushauri ujenzi wa nyumba yako ukute anamwambia mjenzi kuwa "mimi mweshimiwa injinia nilikuwa nafikiri hapa ukuta mngeunyoosha na simenti msiweke mchanga mwingi lakini mimi naunga mkono ujenzi wenu mia kwa mia"msimamizi sahihi ambaye siyo mzigo wa ujenzi ya nyumba yako kwanza anamuomba mjenzi ampe aina ya vifaa anavyotaka kuvitumia ili aangalie ubora na kutoa ruhusa, wakati wa ujenzi akikuta ukuta umepinda kidogo anamwambia mjenzi bomoa ujenge ulionyooka, sementi kidogo mchanga mwingi anasema hiyo mwaga lazima uweke uwiano unaokubalika.

Bunge letu linaendeshwa kama debate za sekondari "upande unaopinga na upande unaosapoti mada", bado hawajui wanachokifanya maana maana ya bunge haijulikani maana si wawakilishi wa wananchi kusimamia serikali bali limegeuka uwanja wa mabishano wa vyama vya siasa.kama tunataka maendeleo kila mbunge chama chake kibaki mlangoni wabunge wote wanakuwa kambi moja na serikali inayohojiwa kambi nyingine lakini mkubwa pale ni bunge "hapa lijitambue kuwa lina wajibu wa kurekebisha upuuzi wa serikali"mfano kuna tabia ya mawaziri kupeleka fedha za maendeleo katika maeneo kwa upendeleo hasa majimbo yao, kwa mfumo holela tulionao kila atakayeingia atafanya hivyo. Bunge ndio chombo cha kwanza kuondoa upuuzi huu kwa kutumia njia kama hii.

Kwanza mnaagiza serikali kuweka malengo ya kitaifa ya maendeleo kama kufikia mwaka fulani tunataka huduma ya maji mijini kufikia asilimia fulani na vijini kufikia asilimia fulani.sasa takwimu za taifa zima kuangalia kila wilaya imefikia asilimia ngapi ya utekelezaji wa mpango huo wa taifa, vinaaandaliwa vigezo vya utekelezaji mfano kipaumbele kinawekwa kwa wilaya ambazo bado ziko chini na miradi ya kuchochea uchumi kitaifa. Waziri anapoleta bajeti yake ni kuangalia kama yuko katika kutekeleza mpango wa maendeleo wa taifa na fedha anazigawa kwa vigezo.ni upuuzi mtupu kuona mbunge anasiamama na kudai kama kujiji fulani hakitegewi fungu anatoa shilingi wakati huo pengine wilaya yake imevuka lengo na sehemu ambayo wako chini kabisa ya malengo tena hawapewi nafasi kuchangia katika hiyo mada.

Ili kusimamia serikali lazima bunge liwe na sauti moja ya wananchi na sio vyama vya siasa na liwe na kauli moja ya kuwa na nini waziri anatakiwa kufanya na kumpima kwa mapendekezo aliyoyaleta na yale aliyotakiwa kufanya sio kila mmoja huyu anatokea kilabuni, huyu anatokea kwenye biashara zake huyu anatokea sijui wapi wanakutana kujadili hoja za serikali kila mmoja anasema yake na mwisho hawana maamuzi.ni wapumbavu tu wanaoweza kusoma majukumu ya bunge kuwa ni kushauri wakaenda bungeni kusimama na kusema wanayofikiri kuwa kama wabunge wametimiza wajibu wao.

Wajibu wa mbunge si kusema anayowaza na kuyahalalisha kwa kutanguliza wananchi wangu wamenituma, bali lazima kuwe na mfumo rasimi wa kitakwimu kuonyesha mwenendo wa maisha ya watanzania na serikali inapanga nini na kutekeleza nini kuhusu maisha haya ya watanzania.hivyo kwa mbunge mambo muhimu ni takwimu za hali maisha ya watanzania, mipango ya maendeleo ya kitaifa, mipango ya mapato na matumizi, utekeleza wa mipango. Na mbunge anapokaa bungeni ni kujadili mambo ya kitaifa kwa maana ya kwamba unakuja na hali iliyoko jimboni kwako, zinalinganishwa na takwimu za kitaifa na hivyo utekelezaji wa serikali lazima ufuate malengo ya kitaifa na hali halisi.serikali inapokuja bungeni lazima kila waziri aambatane na watu muhimu katika wizara yake kila mmoja anajibu maswali katika eneo lake.

Haiwezekani bandarini kuna tatizo waziri hajui chochote yeye ndiye anakaa kujibu maswali hata mambo ya kweli anapinga kujilinda kwa nini mkurugenzi wa bandari asiwe pale na kama anamawazo bora ambayo waziri amekuwa hayapi kipaumbele kwa sababu mkurugenzi hajipendekezi kwake bunge linayapitisha pale pale na kama anamakosa ambayo yanaonekana hayamgusi sana waziri bunge linaagiza awajibishwe.

Utafiti unaonesha bunge hilo,tangu uhuru ndo bunge atleast lililoonesha kujali matatizo ya wananchi na pia kuwa bubge machachari zaidi kwa kujenga na kutetea hoja
 
Back
Top Bottom