Bunge live 'limeanza'!

Jamaa umeona umetoa bonge hoja mwenyewe...
 
Serikali haijakataza bunge kuoneshwa live huu ni upotoshaji tu.

Serikali imejitoa kuonesha bunge live kupitia shirika lake la utangazaji TBC kwa sababu ilizozitoa.

Aliyezuia vikao vya bunge kuoneshwa live kwa vyombo binafsi ni bunge lenyewe baada ya TBC kujitoa kurusha matangazo hayo.

Kwa hiyo kulaumu serikali hasa rais kwa maamuzi ya mhimili mwingine ni upumbavu tu,rais alaumiwe kwa kujitoa kwa TBC basi lakini hata akiamua TBC irudishe utaratibu wa zamani wakuonesha live,uongozi wa bunge tayari umezuia kamera yoyote kuingizwa kwenye ukumbi wa bunge kwa ajili ya kurusha live.

Haya yote yanatokea sababu hatuna upinzani imara nchi hii.
 
Kichwa cha habari na yaliyomo tofauti kabisa.ccm bwana ni shida.sasa kijana kama huyu usikute kule ccm ndo msomi kuliko wengine.
 
Yaan ilibidi watanzania wote tuwepo pale bungeni, tushiriki moja kwa moja, tuulize maswali, tusikilize hoja na kupitisha baadhi ya mambo sasa kwa kuwa hilo haliwezekani ndio maana tumechagua wawakilishi wakawasilishe matakwa yetu. Sasa kama kushiriki moja kwa moja imeshindikana basi tuna haki ya angalau kuona uwakilishwaji wetu huko bungeni. Tuone live bila kuchuja chochote kama hilo limeshindikana basi waongeze ukubwa wa bunge ili watanzania wote zaidi ya milion 45 tukutane pale bungeni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…