Bunge liombe radhi

Bunge liombe radhi

Wadau nawasilisha hoja barazani la kulitaka bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kutuomba radhi walipa kodi wa nchi hii, wapiga kura wao na wenye maamuzi makubwa dhidi yao kabla hatuhatumia haki yetu ya kikatiba kuwataka wawajibike mbele yetu, nasema hivi kwa sababu zifuatazo,

1. Kushindwa kutumia hekima na busara kwa kuendesha mijadala wa wapo mjengoni, hii tabia imekithiri na imeanza kuota mizizi, siku hizi ni kawaida sana kusika bungeni wabunge wakizomea, dhihaki michango ya wenzao na hata kuropoka pasipo mpangilio, wanakwenda mbali zaidi hata kupingana na muongozo wa spika

2. Wabunge siku hizi wanajadili hoja na miswada kwa kufuata ushabiki wa kisiasa wa itikadi wa vyama vyao na si maslahi ya taifa letu, wanaweka maslahi ya chama mbele ya nchi nyuma.

3. Staha ya kuvaa nayo imepungua na juzi naibu Spika amelalamikia uvaaji hususani waheshimiwa wa jinsia KE

Haya na mengine yote ambayo sija yataja hapa juu ni uthibitisho wa bunge kutukosea watanzania hivyo wanastahilli kutuomba radhi kabla hatujalazimisha kupewa heshima zetu

Hapa una mengi lakini ukiisoma KATIBA ya Tanzania kwa uzuri sana imeeleza Bayana kuwa MBUNGE anawakilisha Chama na sio Mpigakura. Sasa kwa mantiki hii ndio maana wanawakilisha mawazo au matakwa ya vyama vyao na sio matakwa ya waliowapigia kura yaani wananchi.

Ndio maana tunasisitiza sana kupata katiba mpya ili mamo kama hayo yaondolewe na MBUNGE awe pale kutetea wapiga kura wake na sio chama chake.
 
Mimi nilishangaa ule mkutano wa kwanza/? mbunge wa ccm mtera alitishia kuwa watapigana bungeni! Na spika, vyombo vya habari nk havikupaza sauti kupinga kauli za hivyo. Huwa najiuliza mbunge wa upinzani angetoa kauli ya vile si tungesikia kile kibwagizo cha uvunjifu wa amani hadi tukome. Matokeo yake jana tena imetoka kauli ya aina ile!! Baadhi ya wananchi wa kanda ya ziwa tumeamua kuwa ccm wakianzisha fujo hizo bungeni, sisi tutawatandika wabunge wao huku mitaani.
 
Back
Top Bottom