Bunge liombe radhi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bunge liombe radhi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Najijua, Apr 14, 2011.

 1. Najijua

  Najijua JF-Expert Member

  #1
  Apr 14, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 1,029
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Wadau nawasilisha hoja barazani la kulitaka bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kutuomba radhi walipa kodi wa nchi hii, wapiga kura wao na wenye maamuzi makubwa dhidi yao kabla hatuhatumia haki yetu ya kikatiba kuwataka wawajibike mbele yetu, nasema hivi kwa sababu zifuatazo,

  1. Kushindwa kutumia hekima na busara kwa kuendesha mijadala wa wapo mjengoni, hii tabia imekithiri na imeanza kuota mizizi, siku hizi ni kawaida sana kusika bungeni wabunge wakizomea, dhihaki michango ya wenzao na hata kuropoka pasipo mpangilio, wanakwenda mbali zaidi hata kupingana na muongozo wa spika

  2. Wabunge siku hizi wanajadili hoja na miswada kwa kufuata ushabiki wa kisiasa wa itikadi wa vyama vyao na si maslahi ya taifa letu, wanaweka maslahi ya chama mbele ya nchi nyuma.

  3. Staha ya kuvaa nayo imepungua na juzi naibu Spika amelalamikia uvaaji hususani waheshimiwa wa jinsia KE

  Haya na mengine yote ambayo sija yataja hapa juu ni uthibitisho wa bunge kutukosea watanzania hivyo wanastahilli kutuomba radhi kabla hatujalazimisha kupewa heshima zetu
   
 2. Muadilifu

  Muadilifu Senior Member

  #2
  Apr 14, 2011
  Joined: Sep 26, 2007
  Messages: 150
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kwa haya nakuunga mkono Bruker. Nilisikitika sana jana, mpaka nikawa siamini macho na masikio yangu, kuwa hili ni bunge au kilabu cha kimpumu. Nadhani Spika inabidi atumie mamlaka yake vema kurudisha nidhamu ya bunge, lakini afanye hivyo baada ya kututaka radhi watanzania.
   
 3. L

  Loloo JF-Expert Member

  #3
  Apr 14, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 214
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  mmmh me nafikiri kuomba radhi sio suluhisho ukweli ni kwamba wamekosa adabu huwa najiuliza hao wanaozomea wana:watoto?,degree?,wake,?waume?, au ni wahuni tu walioingia bungeni kupitia migongo ya wahuni wenzao?manake hata makazini wale walioingia kwa migongo ya watu bila juhudi na sifa zinazotakiwa huwa hawana nidhamu ya kazi manake hawajui uchungu na thamani ya kazi husika nafikiri na bungeni ni hivyo hivyo da natamani Mungu angenyosha mkono wake akatoa fundisho flani,manake mamlaka imekosa adabu
   
 4. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #4
  Apr 14, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Hakuna haja ya kusubiri ama kuwataka wao waombe radhi, nadhani ni wakati mzuri kwetu sisi wananchi kutathimin mwenendo wa matendo yao na kufanya maamuzi magumu. JAMANI WATANZANIA WENZANGU HEBU TUWE SERIOUS, NEXT TIME TUTUMIE HAKI YETU YA KIKATIBA KWA UFASAHA!
   
 5. m

  msambaru JF-Expert Member

  #5
  Apr 14, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 242
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 45
  Acheni woga, ccm bila ligi ya man to man hayaendi haya mangumbaru. CDM MPs msilale mpk kieleweke.
   
 6. I

  ICHONDI JF-Expert Member

  #6
  Apr 14, 2011
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 588
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Hivi ninyi watu mna matatizo gani? Kuomba radhi kwa kosa gani, bungeni si mahala pa mchezo, watu wanakwidana mashati bungeni. Nani alikuambia part affiliation ndani ya bunge inatoweka, US kuna blue na red na hata wanavyokaa wanakaa kichama na hilo lipo kila kona. Kuzomea ni jambo la kawaida, Uk house of commons, wanazomea kila siku Hebu mfanye utafiti kuona mabunge yenye vyama vingi yanakuwaje, tatizo tz watu bado tumelala na inasikitisha. India wanazipiga kial siku, loh
   
 7. M

  Msengapavi JF-Expert Member

  #7
  Apr 14, 2011
  Joined: Oct 23, 2008
  Messages: 4,802
  Likes Received: 2,748
  Trophy Points: 280
  Kanuni na sheria rasmi ziko wazi tu. Makinda alipaswa kurejea kanuni zilizopo kuhusu dress code na mengineyo na kisha kutoa mwongozo. Kanuni ingeazuia kuzomea wasingezomea, ingewazuia kuvaa vimini wasingevaa. Watanzania wanayo haki ya kuhoji mpaka bunge letu liwe makini zaidi kwa kila hali. Katika mabunge mengi sana, hasa la uingereza ambalo nalifahamu vizuri, kuzomeana hilo ni jambo la kawaida. Nafikiri huko ndo tunakoelekea. La msingi ni kwamba inatupasa kwenda na wakati, katika muktadha wa utamaduni wetu.
   
 8. E

  Egyptian Member

  #8
  Apr 14, 2011
  Joined: Apr 1, 2011
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Spika ameshindwa kumanage bunge.Anakua mkali kwenye hoja za msingi za kitaifa kwa kuzizima kibabe.Kama kweli spika anaweza basi wabunge wote wa mipasho wachukuliwe hatua za kinidhamu.Mi kwa maoni yangu bunge la safari hii ni la kihuni tu,na halina tofauti na kijiwe cha mashabiki wa Simba na Yanga au Man U, Arsenal na Chelsea, pumba tupu.
   
 9. L

  Loloo JF-Expert Member

  #9
  Apr 14, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 214
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  kweli we ichondi naona jina lako limekufiti kabisa mkioso kwa hiyo wabunge wa u.s wakianza kuingia uchi bungeni na wa huku waige?wazungu wana tamaduni fikra mtazamo na mienendo yao na siye yetu sio kila upupu tunaiga basi tuwaige kila kt uone
   
 10. K

  KWELIMT Member

  #10
  Apr 14, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 89
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  mmh egpytian ulishawhi kusikia mh waziri/mbunge kujibu au akichangia hoja utasikia.............mh spika........ktk bunge lako tukufu la......................


  Hapo kweny red ni kweli tukufu? kama watu wanalala mle,wanapasha wenzao na kuzomea?
   
 11. H

  Happy mBISE Member

  #11
  Apr 14, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mi nashimdwa kuelewa, huenda hawa wabunge wa CCM wote fani yao ni kuimba taarabu na pale sio mahali pao, na wapo pale kwa sababu wao ni wachakachuaji wa kura zetu siku zote vinginevyo wasingekuwapo mahali pale. Wanaudhi sana na siwapendi. Chadema kaza buti waonyesheni kuwa nyie ni vichwa hampelekwi pelekwi kama wao. Peopleeeeees power.
   
 12. Dr-of-three-Phd

  Dr-of-three-Phd Senior Member

  #12
  Apr 14, 2011
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 194
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mengine yote umesema kweli Bruker ila hili jingine la kusemeana mbovu wenyewe kwa wenyewe hapa spika mwenyewe alipalilia, ule Spika angeondoa ushabiki wa kisiasa akasimamia mwongozo yale yote yasingetokea, kama angekuwa calm kama alivyogundua pale mwishoni akajirudi kwa kuwakemea wote na kuwa wote wangetoka njee na kuahirisha bunge shida kama ile isingetokea. Kwa hili Spika mwenyewe aondoe ushabiki wa kichama na asimamie mwongozo wa bunge.

  Aluta continue !
   
 13. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #13
  Apr 14, 2011
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Lawama zote ziende kwa mama Makinda ambaye anashindwa kuheshimu Kanuni, dharau kwa upinzani, jazba, nk!
   
 14. Jeremiah

  Jeremiah JF-Expert Member

  #14
  Apr 14, 2011
  Joined: Feb 17, 2009
  Messages: 641
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Je nuliza . Ushahidi wa PM kudanganya bunge kuhusu yaliyotokea Arusha ni lini utasomwa? Je Kuhusu Msukuma Ngereja ni lini atasasambuliwa na lisi
   
 15. Mwalimu

  Mwalimu JF-Expert Member

  #15
  Apr 14, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,475
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Spika anawalea wabunge wa CCM wakifanya mambo ya kihuni...wanazomea hovyo, wanaongea hovyo hovyo bila kuruhusiwa n.k....kwake hiyo haoni ni ukosefu wa adabu! Mbunge wa CDM akiongea ghafla anakuwa mkali na kuanza kufoka kama anaongea na wanae nyumbani....\

  Huu ni unafiki mkubwawa Spika kwa sababu amekuwa anawalea CCM ndio maana hali imefika hapa...na bado mpaka wachapane ngumi labda ndio wataanza kuheshimiana!
   
 16. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #16
  Apr 14, 2011
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,650
  Likes Received: 21,865
  Trophy Points: 280
  Mnajua Wabunge wa CCM na spika wao wanadhani walichotumwa na wananchi Bungeni ni kwenda kupambana na Chadema. Hata hoja iwe ya msingi na manufaa kwa taifa madamu imetolewa na Mbunge wa Chadema basi itapingwa na kuzomewa kijinga jinga. Huu ni upumbavu ambao wabunge wa Chadema sasa unaanza kuwachosha na kufikia kusema "funga milango zipigwe"
  Makinda angesimamia haki na kuacha ushabiki wake safari hii kungekuwa na Bunge zuri sana kuliko yote yaliyopita kwa kuangalia uwiano kati ya wabunge kivyama,damu mpya,uelewa mpana nk. Fikiri Bunge hili lingekuwa chini ya Sita ingekuwaje kwa Mawaziri? lazima blabla zingeisha.
  Wananchi tumewaona wabunge wetu wa CCM na tumejua wamo mle wakiwakilisha nini badala ya kutuwakilisha sisi. Huwezi kukubali ulipanga foleni masaa kadhaa kumchagua mtu anayeleta mizaha na kuzomea wengine wenye kutoa hoja zenye mishiko. Huyo hafai na lazima nasi wakirudi majimboni tuwaambie hatukuwatuma hayo na ujinga hatutaki maana ndio unaotufanya tushindwe kutengana na umasikini.
   
 17. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #17
  Apr 14, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Yaani bunge linaendeshwa kiushabiki zaidi, kilichotokea jana ni kama kwenye kilabu cha pombe.
   
 18. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #18
  Apr 14, 2011
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Hii ni wazi Spika Bunge limemshinda haliwezi kabisa Bunge la mwaka huu! yuko kichama zaidi kuliko maslahi ya Taifa anajisahau kuwa kile ni chombo cha Taifa na sio chao cha Magamba! iko siku ngumi zitalika kule bungeni, kama jana jioni nilikuwa naangalia taarifa ya habari kupitia mlimani tv nilijionea vituko hasa nikajiuliza bunge letu limekuwa nila vijembe kama waimbaji taarab au....!

  Makinda asipojiangalia vizuri nae atavuliwa magamba!
   
 19. Mpiga Nyoka

  Mpiga Nyoka JF-Expert Member

  #19
  Apr 14, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 283
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 45
  Mimi naona bunge liende hivi hivi mpaka pale kanuni zitakavoanza kufuatwa na yule mama lasivyo ccm wanaona kama bunge ni mali yao. Siku hizi waziri akidanganya anaambiwa hapo hapo kwa sababu amna haja ya kuwa na bunge la makondoo linalopitisha miswada kwa maslahi ya chama..Peoples power mpk kielewekeee
   
 20. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #20
  Apr 14, 2011
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Letu ni bunge la watanzania kwahiyo kunaumuhimu wa kuheshimu kanuni zilizowekwa za kuliendesha bunge letu; kusema kuwa kwa vile wabunge wa uingereza wanazomeana na sisi pia tuige tabia hiyo si sahihi kwani uzomeaji ni ukosefu wa adabu na hufanywa na wale wasio kuwa na hoja za nguvu. Ni vizuri tukaiga yale tu mazuri yanayofanywa na mabunge ya nchi nyingine pasipo kuiga hovyo hovyo tu ilimradi mabunge mengine yanafanya hivyo!!
   
Loading...