Bunge linavuja

iringa

Member
Joined
Feb 5, 2012
Posts
66
Reaction score
33
Leo Bungeni jioni Mh Mjungaji Peter Msigwa kaomba mwongozo wa spika kuhusu usalama wa wabunge kwani bunge linavuja maji. Je kama bunge ambalo ni sehemu nyeti na muhimu sana Tanzania linavuja hali ikoje kwingineko? Kama vile majengo ya shule, Vyuo vikuu, hospitali, na mahakama, barabara, polisi na nyumba za watumishi wa kawaida.

Kiwango cha uchakachuaji wakati wa ujenzi kimefikia hali mbaya sasa. Wana JF toeni ushahidi wa maeneo yenu mlipo na semeni kama kuna haja ya kuendelea kubaki na mfumo wa kiutawala tulio nao kwa zaidi ya miaka 50 ya uhuru na bado tunategemea maendeleo halisi?
 
si wanawaamini wachina zaidi ya watz wazalendo..wakome
 
si wanawaamini wachina zaidi ya watz wazalendo..wakome
Wachina tenda zao za bei rahisi, na si unajua wabongo tunavyopenda vitu cheap. Wabongo nao ni kama wachina tu. Competency yao ni ya kuvizia tu. Kama kuna sehamu ambayo mimi ningekuwa kiongozi ningeiboresha ilikuwa ni JKT. Huko kulipaswa kuwe na wataalamu wa kila aina na mitambo ya aina zote. Tenda zote za serikali zingekuwa zinachukuliwa na hawa watu. Lakini sasa ubunifu bongo ni zero.
 
Indonesia huko mafuriko yalifika hadi Ikulu mwezi uliopita, na kuamua kuliondoa tatizon hilo jumla kwa kutoa tender ya ujenzi wa tunnel la 26km kudrain maji

labda na sisi tutaondoa tatizo la mifumo mibovu ya usimamizi wa majengo ya umma s
 
Indonesia huko mafuriko yalifika hadi Ikulu mwezi uliopita, na kuamua kuliondoa tatizon hilo jumla kwa kutoa tender ya ujenzi wa tunnel la 26km kudrain maji

labda na sisi tutaondoa tatizo la mifumo mibovu ya usimamizi wa majengo ya umma s

Ee baba wa imani epushia mbali jengo hili lisije kuwa kaburi la wawakilishi wetu.
 
posho ya siku moja tu kwa wabunge inaweza kulimaliza tatizo hilo !
 
Six alikuwa anajitapa mzee wa Standard and speed vipi? Hakuangalia viwango? MaCCM bana...
 
Jamani kama jengo la bunge linavuja baada mda mchache kiasi hiki, sijui kama nitakosea kuamini kuwa kuna ufisadi katika ujenzi wake?
 
Jamani kama jengo la bunge linavuja baada mda mchache kiasi hiki, sijui kama nitakosea kuamini kuwa kuna ufisadi katika ujenzi wake?

Uko sahihi mkuu. Hakuna mradi wo wote mkubwa katika hii nchi ambao hauhusishi ufisadi.
 
Hii Nchi inavituko kwelikweli! Niliona ajabu nilipopanda basi likawa linavuja tulipofika kwa trafiki akauliza 'ndugu abiria kuna tatizo lolote?' wengi katika abiria wakajibu 'hakunaa!!' tukachapa mwendo huku tukiendelea kuwalalamikia wahusika wa gari, kumbe hata jengo la Bunge linavuja? This is too much kwakweli!!:A S 114:
 
unampa mchina tenda? atawaangushia paa lote na mfie huko, mpe mjerumani bhana, angalia majengo ya COET yalivyosimama imara hata miaka 100 yatafika bila tatizo, lakini bunge letu utaambiwa linavuja sana, wanataka jingine
 
UDOM ndio usiseme kila jengo linavuja, chezea wachina na mambo ya 10 % wewe! Chukua Chako Mapema ndio habari ya mujini.
 
Hakuna hata mwenye picha jamani akatupia hapa.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Daaah kweli kabisa hata taifa zima linavuja!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…