ndiyomkuusana
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 668
- 426
NI ajabu kama tumefikia hatua ya watunga sheria waliokula kiapo cha kuilinda, kuitetea na kuihifadhi Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kugeuka na kutaka kuivunja.
Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashililah, amesema kuwa wanaandaa utaratibu wa kusitisha kurusha vikao vya Bunge moja kwa moja katika vyombo vya habari ili kuzuia purukushani za wabunge zisionekane kwa wananchi.
Hofu ya Dk. Kashililaha, Spika Anne Makinda na Naibu wake, Job Ndungai, kutaka kuwanyima wananchi haki yao ya kikatiba ya kupata habari ni kwamba baadhi ya wabunge wanavunja kanuni na kufanya vurugu ili kutafuta umaarufu.
Bunge linajipanga kufanya utaratibu wa kukaa na Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA) kuliwezesha Shirika la Utangazaji la Taifa na televisheni nyingine namna ya kurusha shughuli za Bunge.
Kashililah alisema kuwa wanataka kukaa na TCRA, TBC, vituo vingine vya televisheni na waandishi wa magazeti kuangalia namna ya kuweka maadili ya kazi sababu hata TBC wakati mwingine haifuati maadili.
Tumemsikia Kashililah lakini hatumwelewi kama msimamo huo ni wake binafsi, Spika, Naibu Spika au ametumwa kuwasemea wananchi waliowachagua wawakilishi hao anaodai wanafanya vurugu kwa kukiuka kanuni.
Tunasema hatumwelewi Kashililah kwa kuwa kile alichokisema kama ndiyo msimamo wa Bunge zima basi ni aibu na fedheha kwa wabunge wetu kukubali kuivunja Katiba waliyoapa kuilinda na kuitetea.
Bunge linataka kujadili mambo yake gizani. Kashililah na wenzake wanataka kuturudisha kwenye enzi ya zama za ujima wakati sasa dunia imepanuka na kuwa kama kijiji.
Haya mawazo mgando yanatoka katika vichwa vya namna gani? Bunge linataka lisionwe linajadili nini wakati wabunge wanategemea wananchi hao hao wanaotaka wasiwaone wawapigie kura za kuwapeleka bungeni.
Spika na wasaidizi wake wanapaswa kuacha kuogopa vivuli vyao. Haiwezekani mjadala wa wasomi wa kariba kama ya wabunge uendeshwe kwa wote kuwa na mawazo yanayofanana.
Wajibu wa kiti hapa si kuahirisha Bunge kwa jazba na vitisho kama tulivyoshuhudia akifanya Spika na naibu wake bali ni kujikita kusimamia kanuni na kuwabana wanaozivunja.
Mathalani tumeshuhudia mahakamani mawakili wakivutana na kulumbana kwa hoja na maneno makali, lakini hatujawahi kusikia wala kuona hakimu au jaji kaahirisha kesi kwa sababu ya malumbano ya hoja, sasa woga wa Bunge letu unatoka wapi?
Spika na wenzake wanafahamu kuwa ibara ya 18 ya Katiba ya nchi inatoa uhuru kwa wananchi kupata habari; sasa walipokaa na kufikia hatua ya kutaka kuishawishi TCRA iwaruhusu wazuie matangazo ya moja kwa moja kutoka bungeni wana ajenda gani ya siri?
Vinginevyo tuambiwe kuwa wanataka kuzui wananchi wasione udhaifu wa mawaziri kushindwa kujibu hoja; hawataki tuone wabunge na mawaziri wanaosinzia muda wote; na wanakwepa kujue ni kina nani wanatumia muda wa Bunge kutangatanga ukumbini wakati wenzao wanajenga hoja nzito.
Bora ikawekwa bayana kuwa wanataka Bunge lenye wawakilishi wa kusema ndiyooooooo kwa kila hoja inayoletwa bungeni vinginevyo msigano haukwepeki hata kidogo, hivyo kuzuia matangazo ya moja kwa moja ni kuvunja Katiba.
source: tanzania daima