Mimi pia nimeliona hilo...
Kisha la ajabu kubwa ni kwamba maswali mengi bungeni hujibiwa na mawaziri kwa kusoma yale waliyo nukuu toka karatasi zao na sii jambo ambalo waziri anatakiwa kufahamu majibu toka kichwani mwake kwa sababu mambo yote yanayoulizwa yapo ktk hatua ya Utekelezaji..Waziri anatakiwa kufahamu kafanya nini na kitu gani kina kwamisha.. Hiindio kazi yake na waziri anatakiwa kufahamu kila hatua ya sera ambazo tayari zipo ktk hatua hii na sii kunukuu vitu kama vile huyu waziri ni mtu alotumwa kujibu kwa niaba ya...
Pili, Majibu ya viongozi wetu wengi hayaridhishi hata kidogo na ajabu ni kwamba sijaona upande wa Upinzani kutoridhika na majibu ya mkato yanayotolewa na mawaziri..Tena ajabu ni kwamba Waziri anaweza kuja na kusema - NILIKUWA SIJUI, hivyo nitaliwakilisha kwa wahusika. Hapa inanichanganya zaidi kwani kama waziri alikuwa hafahamu na bado akapata muda wa kuandika majibu ya hoja iweje asiwe na muda wa kutafuta ukweli wa madai ya mbunge kabla hajaandika majibu yake, hivyo anapopanda jukwaani anakuwa na majibu yanayokwenda na wakati..
Hakika nimeona miujiza mingi tu bungeni na inasikitisha sana kuona wananchi tuna endelea kuwachagua viongozi kama hawa wasioheshimu kabisa Bunge na Spika wake...Jamani hawa watu (wabunge) wanapiga wameligeuza kabisa bunge kuwa kijiwe chao, na sidhani kama utovu huu unafanyika pia ktk mahakamani zetu..