Bunge Limeisha - CHADEMA Tuhamie Igunga

Bunge Limeisha - CHADEMA Tuhamie Igunga

Ndallo

JF-Expert Member
Joined
Oct 1, 2010
Posts
7,619
Reaction score
4,303
Kwa wale wakereketwa wa chama makini cha Chadema tusipoteze muda hapo Dodoma baada ya kufuatilia kwa umakini vikao vya bajeti ya 2011-2012 japokua baadhi ya bajeti zimepitishwa kisanii!

sasa naowaomba tusipoteze muda tuhamie Igunga tukalichukue hili jimbo japoku wao wanapesa! Sisi tuna Mungu! Ninavyopost thread hii ndio niko mbioni kuelekea Igunga asanteni na nawatakia weekend njema hakika tutashinda.
 
Ushindi ni mikakati na hoja,Jenga hoja CHADEMA ,tetea hoja CHADEMA,Elezea Ilani yako CHADEMA.Umoja uwepo CHADEMA.....haya yakiwepo hakika CCM watajuta kuwaona CHADEMA kule IGUNGA.INAWEZEKANA....Kwa CHADEMA HIIII......
 
Nikipanga mambo yangu yakapangika nitaenda tena kwa gharama zangu ili kuhakikisha hakuna uhuni utaofanyika huko na lazima chadema kipande ushindi maana wamezoea kukaba mpaka penalt
 
Msipohamia Igunga
1. mamluki watapiga kura (Chini ya ulinzi mkali)
2. vitambulisho vya kura vitanunuliwa
3. Kura zitabadilishwa, tena masanduku kabisa (Chini ya ilinzi mkali)
4. Kura zitachakachuliwa (Chini ya ulinzi mkali na madonge manono kwa mawakala)
 
Naungo hoja 100% tukalinde kura pamoja na kuelimisha raia wa huko wajue wajibu na haki zao.
hakuna kulala hadi kieleweke
 
Back
Top Bottom