Bunge limechakachua Hansard kumuokoa Pinda? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bunge limechakachua Hansard kumuokoa Pinda?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Hamuyu, Mar 20, 2011.

 1. H

  Hamuyu Senior Member

  #1
  Mar 20, 2011
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 119
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Wakuu heshima kwenu,

  Kuna taarifa uthibitisho wa hoja 10 zilizowasilishwa Bungeni na Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema za kuthibitisha uongo wa Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Peter Pinda kulidanganya Bunge na Umma juu ya mauaji ya Arusha, Ofisi ya Bunge imelazimika kuchakachua hansad ambayo ni dhahiri sasa kumbukumbu zinaonesha kwamba inavyosomeka sasa iko tofauti na majibu yaliyotolewa Bungeni wakati Mhe. Waziri Mkuu anatoa majibu juu ya mauaji ya Arusha kufuatia suali aliloulizwa na Kiongozi wa Upinzani Bungeni Mhe. Freeman A. Mbowe juu ya msimamo wa Serikali kuhusu mauaji hayo.

  Ni dhahiri sasa bunge linatapatapa kumuokoa Waziri Mkuu kwa kuwa hoja zote 10 alizozitoa Mhe. Lema ni mzito na zinathibitisha pasipo shaka kwamba Waziri Mkuu amesema uongo na baada ya kupotoshwa na wasaidizi wake.

  Naomba kuwasilisha wana JF.
   
 2. Mzee Wa Rubisi

  Mzee Wa Rubisi JF-Expert Member

  #2
  Mar 20, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,754
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  mkuu source ya HANSARD. Nijuavyo vyovyote vile hansard yeyote inayotolewa bunge ningumu kuibadili.Licha ya kuwepo maandishi pia hipo sauti kwa mfumo ya kitekinoligia,Sasa kama kweli kuna mchezo huo.Bunge linapoteza sifa,
   
 3. Mipangomingi

  Mipangomingi JF-Expert Member

  #3
  Mar 20, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,719
  Likes Received: 980
  Trophy Points: 280
  Ya'rabbi muongoze Ana Makinda!
   
 4. H

  Hamuyu Senior Member

  #4
  Mar 20, 2011
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 119
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mkuu tafuta majibu ya Waziri Mkuu na print hansad kwenye website ya bunge hata leo
   
 5. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #5
  Mar 20, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  hii ni tetesi unauhakika na source yako hata hivyo kwa dunia ya leo watazidi kujimaliza wenyewe kwani tayali vyombo vya habari vili record na kama sikosei niliiona kwenye youtube
   
 6. fangfangjt

  fangfangjt JF-Expert Member

  #6
  Mar 20, 2011
  Joined: Apr 25, 2008
  Messages: 571
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 33
  HAWAWEZI

  Uwongo wa Waziri Mkuu Mizengo Pinda Bungeni

  Uwongo wa Waziri Mkuu Mizengo Pinda Bungeni

  Katika ufunguzi wa kikao cha Bunge 2011, Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliishutumu CHADEMA kwa kusababisha vifo vya watu watatu wasio na hatia kufuatia vurugu zilizotokea baina ya polisi na wapenzi wa chama mjini Arusha. Mhe Pinda alitoa shutuma hizo wakati akijaribu kujibu swali la Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Mhe. Freeman Mbowe, aliyetaka kujua serikali ina msimamo gani kuhusu mauaji hayo yaliyofanywa na Jeshi la Polisi Januari 5, 2011. Mhe Pinda ama kwa makusudi au kutokujua aliendelea kumimina uwongo Bungeni na kudai hata uchaguzi wa meya wa Arusha ambao ndio chanzo cha maandamano na vurugu ulikuwa umefanyika kihalali.

  Yafuatayo ni maelezo ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda Bungeni kama yalivyochapishwa kwenye kumbukumbu rasmi ya mijadala bungeni (hansard)

  10FKF2

  [WAZIRI MKUU]

  Mheshimiwa Spika, naomba nimshukuru Mheshimiwa Umbulla kwa swali lake, hili ni eneo lingine linalosikitisha sana, Baraza la Madiwani la Manispaa ya Arusha kama zilivyo Halmashauri nyingine zilipanga kwamba mkutano wao kwanza ufanyike tarehe 17 mwezi Desemba. Wajumbe walipata taarifa wote wakahudhuria kikao cha tarehe 17, jumla yao wajumbe 31. Katika 31 hawa TLP Mjumbe mmoja, CHADEMA Wajumbe 14, CCM ilikuwa na Wajumbe 16. (Makofi)

  Mkutano umeanza wajumbe wote 31 wakiwepo, zikaanza hoja kwamba sawa, anayetaka kwenda kuapishwa lakini kwanza tunataka ufafanuzi, huyu Mary Chatanda ambaye ni Katibu wa Chama Mkoa pale Arusha na Mbunge Viti Maalum. Anaingiaje kwenye mkutano huu? Na sisi CCM tukasema "Na nyinyi mnaye Rebbeca Mngodo". Yeye hajaapishwa Bungeni, Viti Maalum anaingiaje hapa? (Makofi)

  Ubishi ule tukalazimika sasa pale Manispaa kuielekeza, ombeni ushauri mmoja kutoka Katibu wa Bunge lakini ulizeni na Tume na ikiwezekana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Ufafanuzi ukatoka kwamba Mheshimiwa Rebbeca Mngodo ni Mbunge halali na Mary Chatanda ni Mbunge halali na kwa hiyo ni Wajumbe halali kwenye mkutano huo. Ubishi huu ulichukua siku mzima mpaka jioni hawajaelewana. Lakini kwa sababu ilibidi tufanye mawasiliano hatimaye jioni kabisa ufafanuzi ukawa umepatikana, wakapewa. Kwa hiyo wakakubaliana kwa nia nzuri tu, kwa sababu imeshafika saa 12 na zaidi kidogo kwamba kwa sababu taratibu zinasema saa 12 na bahati mbaya siku ile umeme ukakatika jioni ile wakakubaliana mkutano ule uendelee kesho yake tarehe 18 asubuhi saa 4.30 na kila mjumbe akapewa barua.

  Kwa mujibu wa Sheria ili mkutano ule uwepo ni lazima akidi itimie. Bahati nzuri wote 31 walikuwepo. Kesho yake sasa, saa 4.30 imefika wakawepo wajumbe 17, 16 wa CCM, mmoja TLP. Wajumbe wa CHADEMA wakawa wanakuja lakini wanatoka. Wanakuja kila anaeingia anatoka, aah mkutano ukasema bwana tusipoteze muda tuendelee. Wakaendelea na mkutano ule siku ile kwa sababu ulikuwa umeahirishwa jana yake. Wakapiga kura Meya kutoka Chama Cha Mapinduzi akashinda. Walikuwa wanashindana mmoja wa CHADEMA, mmoja wa CCM. (Makofi)

  Wakaingia awamu ya pili ya kumtafuta Naibu Meya, wakapiga kura, Mjumbe kutoka TLP akashinda, CCM alishindwa hakupata kura hata moja, CHADEMA hawakupata hata kura moja, wakati huo ilikuwa kama saa 7 mchana. Ndipo akaingia Mheshimiwa Mbunge Lema na Wajumbe wengine wawili pale kwenye Ukumbi wa kikao. Kwa maelezo niliyopewa mimi ameingia pale kwa ukali kwamba sasa ni zamu ya CHADEMA kufanya uchaguzi tuweke Meya wetu. Wakamwambia hapana, hatuwezi kufanya hivyo. Kulikuwa na fujo fujo hivi, ikabidi polisi waagizwe kuja kumwondoa. Mkutano baada ya pale ukaona katika mazingira hayo wacha tuahirishe tukapumzike. Mkutano ukaahirishwa mpaka utakapopangwa tena.

  [WAZIRI MKUU]

  Sasa baada ya pale ndipo tukapata hizo taarifa sasa za maandamano ndiyo yalikuja kufanyika na katika taarifa tulizopewa, moja ilikuwa ni kwamba wanapinga matokeo ya uchaguzi wa Meya na Naibu Meya na mambo mengine. Okay lakini tukasema kuna haja gani kama ni maandamano kama jambo hili lilivyo si kwenda tu Mahakamani mkalalamika likaamuliwa likaisha. (Makofi)

  Lakini halikufanyika hivyo. Sasa niseme hivi, Mheshimiwa Spika, yaani hata kwa hesabu tu za kawaida za mtoto wa darasa la kwanza hakuna namna ambavyo kwa hali ilivyokuwa kwamba mna CHADEMA Wajumbe 14, una CCM 16 utashindaje? (Makofi)

  Sasa kwa sababu hoja hii ilikuwa ni kubwa na hakuna namna nyingine ya kuweza kuitatua ikaonekana suluhu labda hiyo ya maandamano na njia nyingine, mimi nasema hazikuwa lazima sana. Sasa kulikuwa na jitihada kwamba wakutane wazungumze. Mimi nikawaambia hapana mtakutana kuzungumza mnazungumza nini? Hili jambo la kisheria tu. Kwa hiyo kama kuna mtu ana tatizo aende Mahakamani alalamike pale Mahakama itaamua tu na wakiamua sisi tutaheshimu kabisa. (Makofi)

  Kwa hiyo, nataka tu nimalizie kwa kusema ukiniuliza mimi na kwa kuwa nilikuwa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, utaratibu uliofuatwa ulikuwa sahihi kabisa, haukukosewa kitu chochote. Meya ni halali kabisa, alipatikana kihalali kabisa. Baadaye ndipo Naibu Meya alikuja akasema kwenye vyombo vya habari kwamba amejitoa. Lakini sisi hatujapata taarifa yoyote ya maandishi kwamba kajitoa. Matumaini yangu ni kwamba atafika mahali ata-register kwa maandishi ili tuweze sasa kuchukua hatua nyingine ya kutangaza nafasi hiyo iweze kufanyika.

  Kwa kifupi Mheshimiwa Spika, naweza nikasema ndiyo maelezo niliyonayo. (Makofi)

  MHE. MARTHA J. UMBULLA: Swali dogo tu Mheshimiwa Spika. Kwanza nimshukuru sana Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa kuwa sasa suala hili limeeleweka kwa upana zaidi. Lakini kwa kuwa tunaelewa kwamba suala hili kwa sehemu kubwa liko Mahakamani, lakini tumelielewa kwamba kuna sababu iliyopelekea vurugu hizo na hata kupoteza maisha kwa baadhi ya vijana wetu. Je, Serikali sasa inachukua hatua gani kwa chama kilichohusika cha CHADEMA kuwaadhibu ili tukio kama hilo lisirudie katika chaguzi za nchi yetu?

  WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, mimi nadhani hili nadhani wala si suala pengine la kusema ichukue hatua dhidi ya CHADEMA hapana. CHADEMA ina Wajumbe watu wazima, wasomi wazuri. Mimi nadhani kubwa ni wao tu kufika mahali waone kwamba wanalo jukumu la kujenga chama cha kuaminika. Chama ambacho hata kikikabidhiwa madaraka mwaka kesho watasema tumewapa watu ambao wanaweza wakaongoza nchi vizuri. (Makofi)

  [WAZIRI MKUU]

  Kwa hiyo mimi nataka niwasihi sana, hata haya matokeo mengine yote kususia kwenda kwenye matokeo ya uchaguzi pale, kususia kuja kwenye hotuba. Juzi hapa wameshindwa kwenye agenda ni kushindwa tu, wametoka nje. Behaviour hii haiwezi kuwa ndiyo ya kujenga chama kizuri. Nataka niwaombe sana, hili hatuwezi kama Serikali tukasema tutaichukulia hatua CHADEMA, kikubwa ni kwamba wananchi wenyewe wataendelea kuona chama kinavyokwenda na hatua wanazochukua. Halafu wataamua tu. (Makofi)

  MHE. HAMAD RASHID MOHAMED: Ahsante sana Mheshimiwa Spika. Mheshimiwa Waziri Mkuu juzi tulipata briefing juu ya hali chakula nchini, lakini vile vile tumeona katika taarifa mbalimbali kwamba hali ya chakula duniani siyo nzuri. Lakini leo tumepata taarifa nyingine ya kutisha zaidi kwamba hata hali ya chakula wazalishaji wakubwa kama Saudi Arabia hali yao siyo nzuri na wakubwa wanaanza kufikiria kwamba kutakuwa na tatizo kubwa la nishati. Serikali inachukua hatua gani za dharura kuona tunaikabili hali hiyo ili kupunguza ukali wa maisha ya wananchi?

  WAZIRI MKUU: Mhesihmiwa Spika, ni kweli kabisa anachokisema Mheshimiwa Hamad Rasahid Mohamed juu ya kupanda kwa gharama kwa ujumla tu za maisha kutokana na mambo fulani fulani na of course ni hili la mafuta na bei ya mafuta sasa hivi kwa metric tone ni karibu dola 730 kwa kidogo iko juu. Sasa na hiyo ita-trigger bei za bei za vyakula vile vile duniani kupanda, ukichanganya na matatizo sasa ya mabadiliko ya tabia nchi tatizo linakuwa kubwa zaidi.

  Hapa Tanzania tunayo bahati kidogo tu kwa sababu msimu uliopita hali ya hewa ilikuwa nzuri zaidi. Angalau tuliweza kuzalisha chakula cha kutosha, tunayo akiba angalau ya kuweza kutusukuma kwa miezi kadhaa bila matatizo yoyote. Lakinii bado haitupi matumaini makubwa sana na ninalisema hili kwa sababu kwa maoteo ya kitaalam kutoka Idara ya Hewa inaonekana kama Taifa mvua zetu zitakuwa chini ya wastani kwa maeneo mengi. Kitu hicho kidogo si kizuri sana. Tutakuwa na maeneo machache ambayo yanaweza kufanya vizuri. Kwa hiyo nilichofanya baada ya kupata ile taarifa, pamoja ilikuwa ni kuwapelekea Wakuu wa Mikoa taarifa yote ili kila Mkuu wa Mkoa aone mkoa wake uko katika kifungu kipi na kusukuma juhudi za kilimo kwa nguvu zaidi.

  Kwa hiyo Mikoa kama Nyanda za Juu Kusini, upande wa Magharibi kule Kigoma wamefanya vizuri sana. Ni bahati mbaya tu kwamba sasa ukame kidogo umejitokeza tokeza. Lakini hali ya chakula tunaamini bado itakuwa nzuri. Kwa hiyo, hiyo ni moja ya matumaini ambayo tunayapata. Lakini kwa upande mwingine ni kuwaomba Watanzania katika mazingira haya kutumia chakula kwa uangalifu mkubwa. Tutajitahidi sana kujaribu kupeleka mbegu katika mvua zitakazofuata zitakazodumu kwa muda mfupi ili tuweze kujihakikishia kwamba tuna akiba ya kutosha ya chakula. Kwa hiyo nadhani tumejipanga vizuri nafikiri tutakwenda vizuri.

  MHE. HAMAD RASHID MOHAMED: Mheshimiwa Spika nashukuru. Mheshimiwa Waziri unakumbuka kwamba katika suala langu hili niliulizia suala zima la nishati na unakumbuka kwamba katika Bunge hili tuliamua tutaipitisha Sheria ya kwamba sasa tuweze kufanya ile bulck purchases ya mafuta. Sasa sina hakika kama Serikali imetekeleza hilo ili kuweza kupunguza tatizo hili la bei ya mafuta pale ambapo watu wataona kuna shortage ili waweze kuuza mafuta. Je ununuaji wa mafuta wa jumla umefikia wapi mpaka sasa.

  WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa swali lake hilo la nyongeza. Ni kweli tulifanya ule uamzi na Serikali ukauchukua, ukawasilishwa kwenye Cabinet tukalizungumza tukalikubali kwamba ni vizuri tuanze mfumo sasa wa ununuzi wa mafuta kwa kutumia mfumo huo. Lakini kulikuwa na taratibu ambazo ilibidi zikamilishwe ili uweze ku-function vizuri. Kwa hiyo taratibu hizo mpaka tunakwenda kwenye uchaguzi ndiyo zilikuwa zinashughulikiwa ili zikamilike. Matumaini yangu ni kwamba kwa sasa inawezekana zimeshakamilika. Lakini nitacheki, lakini pili upande mwingine tulikuwa vile vile bado kama kawaida kigugumizi hasa kutoka kwa wafanyabiashara kujaribu kukutana nao tumewaeleza faida zake. Lakini bado baadhi yao bado wanaona kama haitawanufaisha sana.

  Sasa naweza nikaelewa sababu, maana sielewi kwenye vyanzo wanavyopata, wanapata kwa namna gani. Lakini bado sisi kama Serikali msimamo wetu ni pale pale. Ni lazima tufike mahali tuyaagize kwa pamoja ili tuweze kupata tija inayotakiwa. Kwa hiyo nina hakika tutaifanyia kazi tukamilishe ili tuanze.

  SPIKA: Mheshimiwa Waziri Mkuu ahsante sana. (Makofi)

  MWONGOZO WA SPIKA

  MBUNGE FULANI: Mwongozo wa Spika

  SPIKA: Ninaongea mimi. Naomba ukae. Waheshimiwa Wabunge tuna nafasi kubwa ya kumshukuru sana Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa uma kwa umakini wa kuweza kujibu maswali mazito ambayo kwa kipindi kilichopita yalituletea wasiwasi na mashaka makubwa kabisa ndani ya nchi. Sasa tunashukuru sana kwa wale waliouliza maswali, tunashukuru sana na mwenyewe uliyejibu maswali kwa sababu angalau Watanzania sasa waelewe kiini na mambo yaliyofanyika. Lakini kikubwa Watanzania tutunze amani yetu. (Makofi)

  Haya kuhusu utaratibu.

  MHE. GODBLESS J. LEMA: Mheshimiwa Spika, Kifungu cha 68(7) ninaomba kupata ufafanuzi kwamba Mbunge anaweza akachukua hatua gani kama anaona mtu mwenye nafasi kubwa katika nchi kama Waziri Mkuu analidanganya Taifa na kulidanganya Bunge. Ahsante.

  SPIKA: Mheshimiwa Mbunge, Bunge hili lazima liwe na adabu inayostahili. Kwa hiyo kama tutafanya Bunge letu hili ikawa ni mahali, sasa unataka kusema Waziri Mkuu kwa ahadi aliyoweka ndani ya Bunge hili anadanganya? Kama anadanganya naomba ukaiandike vizuri kabisa kuhusu kudanganya kwake, halafu nitakuambia tufanye nini. (Makofi)
   
 7. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #7
  Mar 20, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,828
  Likes Received: 10,140
  Trophy Points: 280
  KAZI YA DADA ADELLA HIYO, si ndio maana Mjomba Mpoto akamwambia anyooshe tena kidole amrekebishe???

  bUT in reality haiwezekani kuna ushahidi wa video na sauti, je hizo nazo itakuaje au watazipeleka Loliondo??
   
 8. a

  asakuta same JF-Expert Member

  #8
  Mar 20, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 15,065
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 0
  haiwezekani mkuu kwasababu hansad haiwezi kuchakachuliwa na hutoka kesho yake baada ya kikao..
   
 9. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #9
  Mar 20, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,959
  Likes Received: 1,284
  Trophy Points: 280
  JK onya jamaa zako hao, akiwapo na huyo mama mvivu wa kufikiri jasiri wa jazba na kukurupuka. Hatudanganyiki
   
 10. MartinDavid

  MartinDavid JF-Expert Member

  #10
  Mar 20, 2011
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 876
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  Waziri mkuu amelidanganganya bunge... Ila ukweli utajulikana tu iko siku.

  Pia nasubiri sana kuona tamko wa spika kuhusu hili suala la arusha..
   
 11. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #11
  Mar 20, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Hadi hapa hali ilipofikia Anne Makinda is a Looser...!!
   
 12. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #12
  Mar 20, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Ukweli unajulikana mkuu, labda tusubili hatua watakazo chukua wa husika Makida na Pinda...na mimi nakuhakikishia hili swala ni zito chukulia siku hukumu inatoka huku haki ikiwa imetendeka CDM wakashinda nini kitafata au kama sheri itapindishwa kama wengi tunavyo amini tukaambiwa chadema wameshindwa hakika tegemea maafa mengine vyovyote vile iwe ushindi ama kushindwa...
   
 13. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #13
  Mar 20, 2011
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Hata ukiwa msafi kiasi gani ndani ya ccm lazima utachemsha kwa sababu chama kimejengwa katika misingi ya uongo na kulindana hata mtu akikosea kwa kuwa ana title sheria ipindishwe ili tu aonekane amefanya sawa.

  Shame on them.
   
 14. Zegreaty

  Zegreaty JF-Expert Member

  #14
  Mar 20, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 638
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  kazi kwao,Kikao kijacho sijui watatueleza nini?lazima ile kwao serikali na spika wao wa kubandika
   
 15. j

  junior2008 JF-Expert Member

  #15
  Mar 21, 2011
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 528
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sikubaliani na kauli ya viongozi kupotoshwa na wasaidizi wao ila ni kwamba wao wenyewe hawako makini na ni vilaza pia!!
   
 16. n

  niweze JF-Expert Member

  #16
  Mar 21, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 1,008
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Chadema hakuna ku-back down, tuhakikishe tunatoa mfano kwa Pinda not to ever repeat stupid comments like that. Pia hawa wote wakina Sophia na Kikwete.
  We will make sure the world know what kind of propagandas ccm is running in Tanzania.
   
 17. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #17
  Mar 21, 2011
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  CHADEMA tuache uongo na kuzua mambo kwani hili suala unalolieleza hapa ni suala la kitaaluma zaidi lakini wewe unajaribu kuleta porojo.

  Kitu unachoongea ni kitu ambacho hakiwezekani kabisa kwani pamoja na Hansad ku record na kuweka kwenye maandishi lakini vile vile na vyombo vya habari vilirecord pia.

  Kumbuka kila kitu kwenye Hansad kila kitu kinakuwa recorded na time na date na any modification ina kuwa recorded time na date yake. Hakuna njia yoyote ile inayoweza kufanya ili isionekana.

  lakini hata hivyo na vyombo vya habari(radio na TV) waliomrecord nayo atachakachua.

  Acha uongo na uzandiki. Simama kwenye ukweli.
   
Loading...