Bunge Lijadili Hoja ya Dharura kuhusu Mgomo wa Madaktari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bunge Lijadili Hoja ya Dharura kuhusu Mgomo wa Madaktari

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kitila Mkumbo, Jan 31, 2012.

 1. Kitila Mkumbo

  Kitila Mkumbo Verified User

  #1
  Jan 31, 2012
  Joined: Feb 25, 2006
  Messages: 3,347
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Nchi yetu ipo katika hali ya dharura kutokana na kutaabika kwa wagonjwa mahospitalini bila msaada kufuatia mgomo unaoendelea wa madaktari.

  Itakuwa ni aibu kwa Bunge kuanza kikao chake leo kama vile mambo ni kama kawaida. Hata wabunge wenye hoja binafsi wangeziweka pembeni kwanza ili mojawao aombe kuwasilisha hoja ya dharura kuhusu hili la mgomo kama alivyofanya Wenje kuhusu umeme Mwanza katika kikao kilichopita. Tayari tunaonekana kituko, hili la mgomo wa madaktari litafanya baadhi ya binadamu wenzetu katika nchi zingine waanze kushuku ubinadamu wetu! Na huu utamaduni wa kuamini kwamba ubabe wa fukuzafukuza ni suluhisho la migogoro linazidi kutudhoofisha kifikra na kutufanya tuonekane ndondocha.

  Na wabunge wanapojadili hili la mgomo, kama kweli watajadili, watambue kwamba kitendo chao cha kushinikiza na hatimaye kuidhinishiwa posho zisizo na tija, kimehalalisha na kuimarisha zaidi madai ya madaktari. Ujumbe wa posho za wabunge ni mmoja tu, nao ni kwamba kumbe serikali yetu ina uwezo wa kutekeleza madai yote ya madaktari. Kumbe basi tatizo sio uwezo, bali nia na mgomo ni njia mwafaka zaidi katika kushinikiza watawala kubadili nia.

  Lakini je kuna mtu anasikiliza, na wakisikia wanajali?
   
 2. Nyami2010

  Nyami2010 JF-Expert Member

  #2
  Jan 31, 2012
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 227
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Big up Kaka yangu Kitila Mkumbo! Kikao kinaanza saa tatu asubuhi hii...Mhe. Dr. Kigwangala, Mhe. Mnyika...pick it up!
   
 3. Technician

  Technician JF-Expert Member

  #3
  Jan 31, 2012
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Umesikika mkuu, nakuamini kwa ushauri. Nadhani mwenye akili atagundua ushauri wa busara na aufuate.
  Lakini naini wa kusikiliza?

  Mwenyewe yuko bize na Wizara ya Mambo ya Nje.
   
 4. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #4
  Jan 31, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Wasiwasi wangu ni hata kama itatolewa hoja ya dharura kuhusu mgomo wa madaktari, ni waziri gani atakayetoa majibu ya kuaminika na yenye kuleta suluhu ya matatizo yaliyopo? Nani mwenye busara za kutatua mgogoro uliopo na wakati huu ambapo hata waziri mkuu ameshakuwa mtu wa jazba badala ya hoja?

  Kwa mfano ikitokea mbunge akatoa hoja ya kutaka serikali ikashughulike na kutatua tatizo la madaktari kwanza na kusitisha shughuli za bunge, wabunge wako tayari kwa hilo au watajali posho?
   
 5. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #5
  Jan 31, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Vikao vya bunge vimeanza
   
 6. Bukanga

  Bukanga JF-Expert Member

  #6
  Jan 31, 2012
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 2,863
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  Nimeona asbh wanajadili mkonge na pango, watashtuka kweli hawa jamaa wanotibiwa Apollo? Okey lets wait and see but I guess Dodoma inaweza kuwa biznes as usual.....
   
 7. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #7
  Jan 31, 2012
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,927
  Likes Received: 2,080
  Trophy Points: 280
  Kwa kuwa PM ameshatoa msimamo wake/maamuzi yake suala hili ni very likely likajadiliwa kiushabiki.....itakuwa vigumu kwa wabunge wa CCM "kumuangusha" waziri mkuu!

  Hata hivyo sio wazo baya....wabunge wanaweza kujaribu......lakini linaweza kwenda vizuri zaidi bungeni kama hoja hiyo ya dharura italetwa na mbunge wa CCM.
   
 8. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #8
  Jan 31, 2012
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,315
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Hiyo imenipita, nani waliokuwa wanajadili?
   
 9. M

  Molemo JF-Expert Member

  #9
  Jan 31, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Mkuu Kitila.Tuko pamoja.Umenena vema wabunge wetu wasikie kilio cha watanzania.Nadhani Tundu Lissu,Mnyika,Lema,Zitto na kiongozi wao Mbowe wamesikia
   
 10. only83

  only83 JF-Expert Member

  #10
  Jan 31, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Umenene Dr..nategemea uzalendo na utaifa kwanza kwa hawa wawakilishi wetu,japo kwangu wamekwisha poteza mvuto muda mrefu.
   
 11. j

  jigoku JF-Expert Member

  #11
  Jan 31, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,347
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  Bunge linaendelea naona watu wanaendelea na maswali na majibu tu,sioni kama kuna dalili ya kuleta hoja kujadili jambo la dharura.lakini to be honest hili ni wazo zuri sana maana kwa taarifa nilizo nazo hali si nzuri huko mahospitalini tayari watu wanaendelea kupoteza maisha kila muda unavyokwenda.jamani hata wabunge wa CDM hamtaliona hili kama ni jambo la muhimu sana?
   
 12. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #12
  Jan 31, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Mkuu, umenikumbusha jamaa yangu mmoja aliniambia kwamba waziri husika wa mambo ya nje hana kazi sasa hivi. kazi yake ni kufanya appointments na bookings za mkulu.

  So, sad.
   
 13. babayah67

  babayah67 JF-Expert Member

  #13
  Jan 31, 2012
  Joined: Mar 28, 2008
  Messages: 493
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Kaka Kitila, Hoja yako ni ya msingi saana, hata mimi nilitarajia hasa vyama vya upinzani kulisimamia hili, maana ni kete nzuri saana kisiasa. Lakini nashangaa SI CHADEMA WALA TLP waliotamka neno in a very STRONG TERMS. Heri yao NCCR waliojitamkia on behalf of serikali kwa kuwaomba Madaktari kurudi kwanza kazini then madai yao ndio yajadiliwe. Hata hivyo kaka mkumbo nakutumia message binafsi uisome tafadhari!!!
   
 14. M

  Molemo JF-Expert Member

  #14
  Jan 31, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Wazo zuri sana.Wabunge wa Chadema ambao ndio watetezi pekee wa watanzania wafanyie kazi hili swala
   
 15. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #15
  Jan 31, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Dr, honestly, labda kama serikali itakuwa imegundua kwamba imechemka in the first place. Approach yake kwenye hili swala through katibu mkuu wa wizara husika and later PM Pinda was wrong in all aspects.

  Otherwise, majibu ya serikali yanatolewa na waziri mkuu ambae ndiye aliyechemka zaidi, sasa tutatarajia majibu tofauti? Tukizingatia kwamba tayari Wabunge wa CCM wameshafanya kikao na kuonyesha kuchukizwa na mwenzao Kigwangala kwa ushiriki wake katika mgomo (I don't believe kwamba ameshiriki katika kiwango cha kuwashawishi madaktari anyway)
   
 16. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #16
  Jan 31, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,125
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Wana muda hao watetea matumbo?
   
 17. n

  nderingosha JF-Expert Member

  #17
  Jan 31, 2012
  Joined: Mar 20, 2011
  Messages: 3,527
  Likes Received: 1,314
  Trophy Points: 280
  Kweli Dr...this needs to be done ASAP......inauma sana....wish i had power in this country(bahati mbaya mi si mwanasiasa na wala sipendi siasa)....ningewaswaga hawa washenzi mithili ya Sokoine(na labda labda zaidi yake)....nchi gani hii inayoongozwa na manyang'au na mafisi!!.....TZ ni nchi tajiri sana na haikutakiwa iwe hapa ilipo....lakini tunaongozwa na manyang'au hawa......raia wa Tanzania ni wapole sana...they don't deceive this....hata dunia inalijua hili......only time will tell......
   
 18. W

  We know next JF-Expert Member

  #18
  Jan 31, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 664
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nadhani ni kipimo kwa Wabunge wote leo. Ingawa nasikia Wabunge wa CCM wamekaa kama kamati ya chama na kuwatisha na hata kutaka kuwafukuza wengine uanachama, sasa hiyo ndiyo kawaida ya janja ya serikali na ccm, lakini kwa hili hawana ujanja, Suala hili la madaktari ni tete.
   
 19. nashy

  nashy JF-Expert Member

  #19
  Jan 31, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 679
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Dr kinachouna zaidi ni pale matatizo yanatokea mwenye nchi yuko huko kwenye vikao na mikutano ambayo siku zote amehudhuria na hakuna positive changes kwa taifa. Watu wanakufa, Pinda anasema hakuna pesa kwa madaktari at the same time anawaambia wabunge Rais kapitisha posho nao wanashangilia ujinga wakati watu wanakufa kwa kukosa tiba. Viongozi wamelewa madaraka na kusahau mambo ya muhimu kwa nchi. Ila nadhani Mungu anataka kuwaonesha kitu watanzania. Maana hata biblia inasema ukiona mambo yote hayo ujue mwisho umekaribia, ole wao watakaokata tamaa. Naamini mwisho wa ccm umefika
   
 20. Gwalihenzi

  Gwalihenzi JF-Expert Member

  #20
  Jan 31, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 5,117
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Ndugu yangu DR. Kitila, wabunge wa CCM hawapo tayari kwa hilo. Kama umesoma gazeti la Mwananchi la tarehe 31/1/2012 utaona walivyomuweka kiti moto mbunge mwenzo Dr Kigwangala kwa kosa la kuwaunga mkono madaktari wanaogoma. Kwenye kamati yao ya wabunge wa CCM walimpongeza sana mh.sana mtoto wa mkulima wa sumbawanga kwa wa ganga wa jadi kwa hatua nzuri alizochukua dhidi ya 'madaktari watukutu' wanaogoma !
   
Loading...