Bunge letu na itikadi za vyama. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bunge letu na itikadi za vyama.

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by MAGAMBA MATATU, Jul 3, 2011.

 1. MAGAMBA MATATU

  MAGAMBA MATATU JF-Expert Member

  #1
  Jul 3, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 617
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 60
  Kama ilivyo kawaida, bunge la sasa lina wabunge 350, lakini wengi ni kutoka CCM wakichukua robo tatu ya wabunge wote, huku Spika Anne Makinda na Naibu Spika, Job Ndugai wote wakitoka chama hicho tawala.

  Kutokana na wingi wao, bunge limeonekana kuegemea zaidi upande wa chama kimoja likipitisha maamuzi mengi kwa kujali itikadi na matakwa ya CCM sababu zikiwa hazijulikani ni kwanini?
  Mfano mzuri ulijidhihirisha hivi karibuni wakati wa upitishaji wa bajeti ya Serikali ya mwaka 2011/12 ya Sh 13.5 trilioni ambayo ilikosolewa na wadau mbalimbali tangu ilipowasilishwa.

  Kati ya wabunge 315, wabunge 234 walipiga kura ya ndiyo kupitisha bajeti hiyo, huku wengine 81 wanaotoka kambi ya upinzani wakiikataa. Kwa mujibu wa Spika Makinda, wabunge 34 hawakuwamo ukumbini wakati wa wa kupiga kura hiyo. Mbali na upitishwaji huo wa bajeti hiyo, kumekuwa na mijada mingi ambayo imekuwa ikiendeshwa kwa kufuata itikadi. Kwa mfano, mjadala wa posho, ulionekana kuungwa mkono na wabunge wa Chadema huku wale wa CCM wakiupinga na hatimaye bajeti ya serikali yenye posho hizo ikapita,

  1. ni kwanini viongozi wa bunge wanaliendesha bunge letu kwa matakwa ya chama kimoja au kwakuwa
  wapinzani siku zote inabidi wapingwe hata kama hoja zao ni za msingi??

  2. au labda wapinzani ni walopokaji sana bungeni bila kutoa hoja za maana ndo maana makinda, ndugai na simbachawene
  wanaegemea upande wa ccmkwakuwa ndo wanatoa hoja za kimsingi???

  3. labda wabunge wa ccm wako kimaslahi ya chama chao zaidi kuliko wananchi?

  4. au wapinzani bungeni wanaongea sana kwa kujionesha kwenye TV ili wajulikane kama alivyosema Mwanasheria mkuu
  wa serikali ndugu Werema kuwa wanatafuta umaarufu kisiasa.
   
Loading...