Bunge letu halijadili mambo ya msingi katika Ustawi wa Taifa letu

Bunge letu halijadili mambo ya msingi katika Ustawi wa Taifa letu

Jamani kwema humu ndani?

Leo nimeona niliongelee Bunge letu pamoja na madudu yake.

Yaani Bunge la kipindi hiki ni bunge la ajabu kuwahi kutokea katika historia ya nchi yetu.
Wabunge badala ya kuongelea mambo ya msingi kwa ajili ya usitawi wa Taifa letu, wengi wao wamekuwa wakijikita kwa mambo ya hovyo yasiyo na kichwa wala miguu.

Huenda hali hii imechagizwa na wengi wao kuwa na elimu za kuunga unga na wengine kujipachika vi-PhD vya kununua, lakini Kichwani hamna kitu!

Nachelea kusema zaidi ya 50% ya wabunge wote wa bunge hili, hawatarudi bunge lijalo. Maana sisi wananchi tupo macho kuwaangalia tena kwa umakini sana na michango yenu ambayo mingi haiko kwa maslahi ya Taifa.

Eti, baadhi yao nao walikuwa wanashangaa lile roboti Eunice kwamba ni la kiwango duni ilhali wengi wao hawana tofauti na hilo dude!

Jiandaeni kisaikolojia, pepeto linakuja 2025.
Samia alishasema mkimchagua au msipomchagua atashinda tu, maananyake CCM wana uwezo wa kugeuza natokeo, kwa hiyo wewe ndiye wa kujiandaa kwa maumivu
 
Nakusahihisha.

Ni uwongo kusema hilo ni bunge letu. Hayo majizi ya mamlaka ya wananchi kuwachagua wawakilishi wanaowataka, unayaita ni wabunge wetu?

Haya ni majizi, haya ni maporaji ya mamlaka ya wananchi. Yalistahili kufukuzwa kutoka kwenye jengo hilo. Na wale walioyatangaza kuwa ni wabunge walitakiwa kukamatwa na kushtakiwa.

Jengo la bunge kwa sasa limejaza majambazi ya mchakato wa uchaguzi.
 
Kama Musukuma anamwambia Profesor Janabi kuwa hata yeye ni Dr unategemea nini?

Bunge linasubiri tukio kwenye magazeti na forums ndio wapeleke bungeni
 
Yale madude yalirushwa kutoka Iran kuelekea Israel ilifaa limoja likosee njia lielekee pale dom mjengoni jirani na chuo cha cbe...tuanze upyaa kuliko ilivyo sasa hv!.
 
Kwa bahati nzuri muda wa ubunge ni miaka mi5 kwa hiyo kama wananchi hawaridhiki na utendaji wao hawatawachagua. Hii nchi ya demokrasia
 
Nakusahihisha.

Ni uwongo kusema hilo ni bunge letu. Hayo majizi ya mamlaka ya wananchi kuwachagua wawakilishi wanaowataka, unayaita ni wabunge wetu?

Haya ni majizi, haya ni maporaji ya mamlaka ya wananchi. Yalistahili kufukuzwa kutoka kwenye jengo hilo. Na wale walioyatangaza kuwa ni wabunge walitakiwa kukamatwa na kushtakiwa.

Jengo la bunge kwa sasa limejaza majambazi ya mchakato wa uchaguzi.
Mkuu hiyo "heading" ni ya "Moderators" wa JF.
Kichwa changu cha habari kilikuwa; HILI BUNGE LA SASA NI BARAZA LA MADIWANI LILILOCHANGAMKA!
Hii ni kwa vile sioni kama lina hadhi ya kuitwa Bunge Letu.
 
Back
Top Bottom