Bunge lashindwa kwa mara ya tatu kumchagua Rais wa Iraq

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,500
9,279
Wabunge wa Iraq wameshindwa kwa mara ya tatu kumchagua rais mpya wa nchi hiyo, kutokana na ukosefu wa idadi ya kutosha bungeni. Hatua hiyo imerefusha hali ya mkwamo wa kisiasa katika nchi hiyo iliyoharibiwa kwa vita.

Kitengo cha habari cha bunge kimesema bila kutangaza tarehe mpya kuwa bunge liliahirisha kikao hicho hadi wakati usiojulikana.

Chanzo cha bunge kimeliambia shirika la habari la AFP kuwa ni wabunge 178 pekee kati ya 329 waliokuwepo ikiwa ni idadi isiyofika theluthi mbili inayohitajika kwa kura hiyo kupigwa.

Wabunge lazima kwanza wamchague mkuu wa nchi, na kwa mujibu wa mapatano atoke katika jamii ya Wakurdi, kwa kupata angalau theluthi mbili ya kura zote. Rais kisha atamteuwa mkuu wa serikali, wadhifa ambao sasa unashikiliwa na Mustafa al-Khademi.
 
Back
Top Bottom