Bunge lapata Wenyeviti na Wawakilishi Wapya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bunge lapata Wenyeviti na Wawakilishi Wapya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Apr 15, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Apr 15, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  na Mwandishi wetu

  HATIMAYE Bunge la Muungano limepata wenyeviti watakaomsaidia Spika kuendesha shughuli za Bunge.

  Waliochaguliwa kushika nafasi hiyo ni pamoja na Mbunge wa Peramiho, Jenister Mhagama, Sylvesther Masele Mabumba (Dole) na George Simbachawene.

  Wabunge hao walipita bila kupingwa baada ya wabunge wengine watatu kukosa sifa na Kamati ya Uongozi ya Bunge kuamua kupitisha majina matatu ambayo hata hivyo hayakuwa tena na sababu ya kupigiwa kuwa.
  Katika hatua nyingine, Bunge la Muungano limepata wabunge watano waliochaguliwa kuingia katika Bunge la Afrika akiwemo Mbunge wa Shinyanga, Steven Macele wa Shinyanga Mjini (CCM), aliyeibuka na kura 185.

  Wabunge wengine waliotangazwa kuingia kwenye Bunge la Afrika na kura zao kwenye mabano ni Bernadetta Mshashu (Viti Maalum 143), Mbunge wa Kikwajuni, Hamad Yusuf Masaun (275), Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina (151) na Mbunge wa Khalifa Suleiman Khamis (CUF) ameshinda kiti hicho kupitia kambi ya upinzani kwa kura 283.
  Katika nafasi hiyo, Khalifa alikuwa akichuana na Moses Mchali (NCCR Mageuzi) na John Shibuda (CHADEMA) ambaye baadaye alitangaza kujitoa.

  Kwa upande wa Bunge la SADC, Mbunge wa Viti Maalum, Stella Manyanya, ndiye aliyepita bila kupingwa kuliwakilisha Bunge la Muungano katika Bunge hilo. Kwa upande wa wabunge wanaowakilisha kwenye Bodi ya Mpango wa Tathmini ya Utawala Bora Afrika (APRM), walioshinda ni Matha Umbula na John Shibuda.
   
Loading...