Bunge lamjadili Masaburi

Masuburi ana maana gani kuongea maneno mazito kama hayo,inawezekana kukawa na jambo kati yao masuburi na wabunge,si bure.
 
duh huyu bwana kwa kweli the fact kwamba mpaka muda huu yupo ofisini nina mashaka na 'waliotukanwa' kama nao wako serious
 
Kimsingi Masaburi aliongea tamasali ya usemi akiwa na maana kwamba, wabunge wa Dar hawana akili. Kama jambo waliloamua ni jambo lisilo na manufaa kwa nchi na linaloonesha kiburi cha viongozi hawa alikuwa na uhalali wa kutumia tamathali hii ili kufikisha ujumbe kwamba hawana akili kabisa. Na kwa jinsi naovyowafahamu viongozi wetu, nadhani ni bora wangemezea mate tu, kumjadili na kumpa adhabu kutampa masaburi umaarufu zaidi na kimsingi kwake ni faida kwani ni mwanasiasa.
 
Uki google MASABURI utapata hii




Hata kama ningekuwa mimi ndio mbunge ningemshughulikia huyu meya yaani wabunge wanawaza kupitia hii kitu? Aisee acha wakae vikao vya kumjadili na waongezewe posho kwa kipindi hiki cha kumjadili
 
Kauli ile ilikua na chembe nyingi tu za ukweli
 

Nadhani Hizi kamati za bunge kuna shida ya kukosa kazi na wakati mwingine kutokuwa na mipaka ya madaraka yao kiasi cha kufikia kuwa chombo cha kutoa adhabu. kitu ambacho sidhani kama ndiyo haswa jukumu lake,
 
1.Didas huyu huyu ANA miliki shule ya Dkt Didas huko Dar es Salaam.
2. Didas huyu huyu alishakuwa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki.
3. Didas Huyu huyu ni diwani na Meya wa Jiji la Darisalama.
4. Didas huyu huyu anahusishwa na uuzawji wa UDA kwa Kapuya.
5. Didas huyu huyu.......... waweza kuongezea unavyomfahamu Didas wa Masaburi!
 
Kujadili na kuchukua hatua ni vitu viwili tofauti. Tumeona managapi yamejadiliwa na kuekewea mapendekezo lakini mpaka leo kimya ! Tunataka bunge lenye meno sio hili la blah blah.

Kweli mkuu kujadiliwa siyo suluhisho, bali maamuzi yatakayotolewa kufanyiwa kazi kwa vitendo ndiyo tutaona umuhimu wa kikao hicho
 
Lakini BUNGE na KAMATI YA BUNGE ni vitu viwili tofauti sana!
Mathematically,Kamati ya Bunge ni seti ndogo ya Bunge (Sub set).
Ki utawala Kamati ya Bunge imekasimishwa(deligated) madaraka na bunge katika masuala mbalimbali kuyatekeleza kwa niaba ya Bunge ,hata hivyo inapashwa iripoti kwenye Bunge juu ya kazi zake na bunge litathibitisha(approve) au vinginevyo kazi hiyo.
From Utawala bora Bunge limekasimisha majukukumu si wajibu("You can deligate power but not responsibility").
Hivyo Bunge haliwezi kukwepa sifa au lawama dhidi ya kamati yake.
 
Akipatikana na hatia watamfanyaje?
 
Mi nashangaa watu wazima wanaweka masaburi chini na kulipana posho kumjadili mtu, kweli acha awatukane i wish na hii kamati aipe msemo mwingine mkali zaidi. Labda wanafikiria na kumjadili mtu kwa ku2mia m....o
 

masaburi yuko sahihi namuunga mkono kwani ukiangalia ata kitendo cha yeye kujadiliwa bungeni si cha maana, yaani Bunge lilishindwa kujadili mgomo wa madaktari watanzania wakafa pasipo na idadi sasa wanatumia muda vibaya kujadili kauli ya masaburi.

Masaburi yuko sahihi namimi namuunga mkono na naongezea sio wabunge wa Dar es salaam pekee bali ni wabunge wote wanafikiri kwa kutumia masaburi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…