Bunge laingilia mgomo wa madaktari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bunge laingilia mgomo wa madaktari

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Saint Ivuga, Feb 3, 2012.

 1. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #1
  Feb 3, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,515
  Likes Received: 19,934
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"]Bunge laingilia mgomo wa madaktari[/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Thursday, 02 February 2012 21:35[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]
  0digg
  Waandishi wetu Dar na mikoani
  HATIMAYE Bunge limeingilia kati mgomo wa madaktari kwa kuitaka Serikali kulitolea tamko tatizo hilo leo bungeni, vinginevyo ratiba ya shughuli zake itavurugwa na baadhi ya wabunge wanaotaka suala hilo lijadiliwe.

  Naibu Spika, Job Ndugai alitoa agizo hilo jana wakati anaahirisha kikao cha mchana akisema: "Serikali haina budi kujipanga ili leo itoe kauli kuhusu suala hilo."

  Ndugai alisema Misri kulikuwa kuna mchezo wa mpira, kukatokea fujo uwanjani na kusababisha vifo vya watu mbalimbali, Bunge lilikuwa likizo lakini limeitwa kwa dharura kujadili suala hilo.

  Ndugai aliongeza; “Hapa nyumbani (Tanzania) kuna mgomo wa madaktari unaendelea, asubuhi wamesimama wabunge kuleta hoja ya dharura lakini haikuungwa mkono. Litakuwa jambo lisiloeleweka kama kesho (leo) kauli ya Serikali haitatoka, wakisimama wabunge ratiba yetu inaweza kutibuka.”

  Awali, baada ya kipindi cha maswali na majibu, Mbunge wa Kigamboni, Dk Faustine Ndungulile (CCM), alisimama kwa kutumia kanuni namba 47 (i) na kutaka Bunge lijadili mgomo wa madaktari unaoendelea nchini.

  Hoja hiyo ambayo baadaye iliungwa mkono na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (Chadema), lakini ilitupwa na Ndugai kwa madai kuwa haikuungwa mkono na wabunge wengine.

  Viongozi wa dini

  Viongozi wa dini wa Kikristo na Kiislam jana walianza juhudi za kusaka suluhu ya mgogoro huo katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC ya mjini Moshi.

  Viongozi wa dini walioshiriki kikao hicho ni mkuu wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Dk Alex Malasusa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya hospitali hiyo, Askofu wa KKKT Dayosisi ya kaskazini Dk Martin Shao, Katibu wa Baraza la Waislamu (Bakwata) Mkoa wa Kilimanjaro, Rashid Malya, Msaidizi wa askofu jimbo katoliki Deodatus Matika na Mkuu wa wilaya ya Moshi Musa Samizi aliyemwakilisha Mkuu wa mkoa huo, Leonidas Gama.

  Akizungumzia majadiliano Dk Alex Malasusa alisema:” Ulikuwa mkutano wa kawaida uliokuwa na lengo la kuhimiza na kushauriana juu ya madai ya madktari na tumewakumbusha wajibu wao na kuzingatia viapo vyao”, alisema.

  Katibu wa Bakwata, Shehe Mallya aliungana na viongozi wengine kutoa wito kwa madaktari waliogoma kurudi kuwahudumia wagonjwa ambo kwa sasa wanaendelea kukosa huduma mbalimbali za afya.

  Muhimbili
  Madaktari bingwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), wameungana na kamati ya madaktari inayosimamia mgomo na kuitaka Serikali kujibu hoja za zilizowasilisha kwake haraka ili kumaliza tatizo hilo.
  Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kikao cha pamoja kati ya kamati hiyo na viongozi wa jumuiya ya madaktari, Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Dk Stephen Ulimboka alisema wamekubaliana kuwa masuala yote yanayohusu mgogoro huo na maslahi ya madaktari yafanywe na kamati iliyoteuliwa na madaktari.[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #2
  Feb 3, 2012
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,079
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Yaani hadi waige kutoka misri... Hehe hawa watu bana .. kwa hiyo misri wasingeita kikao cha dharura na wao wasingejadili
   
 3. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #3
  Feb 3, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,515
  Likes Received: 19,934
  Trophy Points: 280
  basi ndio ingekula kwetu.
   
Loading...