Bunge labana matumizi na kuokoa Bilioni 6/-. Zitatumika kutengenezea madawati

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Sep 4, 2013
37,907
43,821
Nasikia zimeshakabidhiwa kwa JPM ikulu. Hatuwezi kuendelea kuacha wanafunzi wakae chini wakati pesa ilikuwa inachezewa hovyo.

Bunge.png

Rais Magufuli ameipongeza ofisi ya Bunge kwa kubana matumizi na kufanikiwa kuokoa shilingi Bilioni 6, ambazo zitatumika kutengeneza madawati ya wanafunzi wa shule na amezitaka ofisi na taasisi nyingine za serikali kuiga mfano huo.

Ameagiza fedha hizo zipelekwe Idara ya Magereza na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ili vyombo hivyo vifanye kazi ya kutengeneza madawati yanayotarajiwa kuwa zaidi ya 120,000 ambayo yatasambazwa katika shule ili kukabiliana na tatizo la wanafunzi wanaokaa chini kwa kukosa madawati.

Hundi Kifani ya fedha hizo imekabidhiwa kwa Mheshimiwa Rais na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Akson, ambaye amesema Ofisi ya Bunge imetekeleza wito wa serikali wa kubana matumizi ambapo kiasi hicho cha shilingi Bilioni 6 kimepatikana kwa kipindi kifupi cha takribani nusu mwaka.

Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashilila ametaja maeneo ambayo Bunge limebana matumizi kuwa ni Safari za nje ya nchi, Mafunzo nje ya nchi, Machapisho na ununuzi wa majarida, Shajala, Chakula na Viburudisho, Mtandao, Malazi hotelini, Matibabu ya wabunge na familia zao nje ya nchi, Umeme, Maji, Simu na Uendeshaji wa Mitambo.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
11 Aprili, 2016

mboj2.jpg

Muonekano wa Madawati ambayo yanatarajiwa kutengenezwa na yaliyoidhinishwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kama yanavyoonekana katika picha.​
 
Rais Magufuli aziagiza Idara ya Magereza na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kutengeneza madawati 120,000 kwa kutumia fedha (Zaidi ya Bilioni 50) zinazookolewa kutokana na watumishi hewa.

Amesema Kati ya shilingi Bilioni 583 ambazo serikali imekuwa ikitumia kila mwezi kwa ajili kulipa mishahara, kati ya shilingi Bilioni 53 na 54 zimekuwa zikipotea kutokana na kulipa mishahara ya watumishi hewa.

Rais Magufuli ameipongeza ofisi ya Bunge kwa kubana matumizi na kufanikiwa kuokoa shilingi Bilioni 6, ambazo zitatumika kutengeneza madawati ya wanafunzi wa shule na amezitaka ofisi na taasisi nyingine za serikali kuiga mfano huo.
 
Ila kuna viti fulani vya chuma na kama
mbao zitumike juu kwenye kuandikia na sehem ya kukalia tu kupunguza matumizi ya mbao na uharibifu wa mazingira.... viti na meza za chuma ni imara na vinadumu sana... serikali ikibidi iondoe ushuru kwenye materials za chuma watakazo tumia ili tuondokane na mbao ambazo madawati yake hayadumu....
 
Haya ndio matumizi sahihi ya pesa za wananchi,kwa sasa kila mtu angalau anaonja keki ya taifa kupitia huduma kama si wewe basi mwanao au mjukuu wako.Nawaonya wale wabunge walitumwa na mafisadi kuhoji uhalali wa raisi kupanga matumizi ya pesa anazookowa kisa walitaka kujineemesha na biashara ya fulana na maji wakome na huyo anayewatuma tulishamkemea alipojaribu kuongelea suala hilo.Katiba ya JMT kifungu 137 inampa raisi mamlaka na sisi wananchi tulio wengi tunaunga mkono.
 
Ila kuna viti fulani vya chuma na kama
mbao zitumike juu kwenye kuandikia na sehem ya kukalia tu kupunguza matumizi ya mbao na uharibifu wa mazingira.... viti na meza za chuma ni imara na vinadumu sana... serikali ikibidi iondoe ushuru kwenye materials za chuma watakazo tumia ili tuondokane na mbao ambazo madawati yake hayadumu....
Wazo zuri na la kizalendo.
 
Dkt. Thomas Kashilila ametaja maeneo ambayo Bunge limebana matumizi kuwa ni Safari za nje ya nchi, Mafunzo nje ya nchi, Machapisho na ununuzi wa majarida, Shajala, Chakula na Viburudisho, Mtandao, Malazi hotelini, Matibabu ya wabunge na familia zao nje ya nchi, Umeme, Maji, Simu na Uendeshaji wa Mitambo.

HII IMEWAFANYA WAOKOE 6 BILIONI
 
Ushauri mzuri sana
 
Wengine 2020 hamuwaoni kugombea tena
 
Back
Top Bottom