Tanzania Railways Corp
JF-Expert Member
- Mar 23, 2018
- 274
- 646
Waziri wa Uchukuzi Mhe. Profesa Makame Mbarawa, ameliarifu Bunge namna serikali inavyonufaika na fursa zake za kijiografia kwa kubuni na kukamilisha miradi mikubwa ya kimkakati ili nchi iweze kunufaika zaidi na fursa hizo.
Waziri wa Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa, ameliarifu hayo Bunge wakati akiwasilisha bungeni mpango wa makadirio ya mapato na matumizi ya fedha kwa mwaka wa fedha 2025/26, ambapo amesema mnano Januari 29, 2025 kupitia Shirika la Reli Tanzania (TRC), imesaini mkataba wa ujenzi wa Reli ya SGR kipande cha Uvinza (Kigoma) - Musongati (Burundi) km 240.
Aidha Profesa Mbarawa ameongeza kusema kuwa kusainiwa kwa mkataba huo ni matokeo ya ya ushirikiano kati ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Burundi na kwamba kukamilika kwa kwa Reli hiyo kutaunganisha nchi ya Burundi na Bandari ya Dar es Salaam sambamba na kuifungua Tanzania kikanda kwa kurahisisha ufanyaji biashara kati ya nchi mbili hizo.