figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,658
- 55,487
Mwenyekiti wa Bunge Andrew Chenge, amesitisha shughuli za bunge kwa saa moja, ni baada ya bunge kulalamikia kutooneshwa live Mikutano ya bunge.
Zitto Kabwe (mbunge) aliomba Muongozo wa kuahirisha bunge kwa sababu hawawezi kuendelea kujadili Hotuba ya Rais iliyooneshwa live wakati bunge halipo live. Wanachotaka ni Bunge kuwa live sababu, TBC1 ni mali ya Umma na haijiendeshi kibiashara.
Hivyo Zitto Kabwe, aliomba Muongozo ili Bunge lijadili hatua ya TBC1 kutoonesha Bunge live wakati inapewa ruzuku na Serikali.
Mara ya Kwanza Chenge alikataa kumpa nafasi Zitto ya kuongea, lakini baada ya Kambi ya upinzani kuanza kupiga kelele, akaamua kusitisha bunge kwa saa moja ili kamati ya Uongozi ikae kujadili hilo swala.
Update: 1300HRS
Bunge limeahirishwa hadi jioni;
Bunge limeshindwa kurejea tena baada ya muda wa saa moja, limeahirishwa tena mpaka saa 10 jioni.