BUnge la Tanzania na Makofi ya kinafiki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

BUnge la Tanzania na Makofi ya kinafiki

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ikimura, Jun 14, 2011.

 1. Ikimura

  Ikimura Member

  #1
  Jun 14, 2011
  Joined: Apr 1, 2011
  Messages: 22
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nimekua ni kifuatilia muda mrefu mijadala inayo endelea ndani ya Bunge na nikaja kubaini kuwa kunakasoro kubwa katika Bunge letu hasa kwa wabunge wa CCM, upigaji makofi wao kidogo unatia shaka!!Mimi ninachokielewa ni kuwa mkusanyiko kama ule wa watu waheshimiwa japo wengine si wasomi ila idadi ya wasomi ni wengi kiasi cha kuwafunika wasiosoma, upigwaji wa makofi uwe wakuikubali hoja nzuri na makini itakayo tolewa na Mbunge wa Chama chochote kile. Ila sasa ndugu zangu wabunge wa CCM hadi wanakera, wanapigia makofi vijembe badala ya point. Sasa, mimi sina uhakika kama huwa wanapata muda wa kupitia tena ile mijadala na kujiridhjisha na kila wanachokuwa wanakipigia makofi na kukishangilia.

  Mi nitoe rai kwa wabunge wote kuwa muda vijembe umekwisha na waungane kwa maswala ya kitaifa na kuwa kitu kimoja, Mfano, leo asubuhi wakati wakichangia mpango wa Taifa wa maendeleo wa miaka mitano, January Makamba ameongea kwa ufasaha sana swala la Elimu pamoja na ajira za Elimu, vilevile ameongelea vizuri sana swala la umeme, Kiasi Mbunge wa CUF aliposimama alisifu alichokiongea kwa sababu kilikua kwa maslai ya Taifa letu na wabunge wote wanapaswa kuwa hivyo. Unganeni kupigania udhalimu, haki sawa na maendeleo ya Taifa letu. Zipo nyakati za vijembe na si bungeni. Mnaopenda vijembe undeeni bendi za vijembe na mpigane hivyo vijembe nje si wakati wa mijadala ya bunge. Ni ninyi mnaochelewesha na kukwamisha maendeleo ya Taifa letu, mnalipwa fedha nyingi na hakuna cha maana mnachokifanya.

  Tafadhali Wabunge wa CCM someni alama za nyakati tumechoshwa na siasa za vijembe tunataka siasa za maendeleo, kwani ukiongea ukweli na ukafukuzwa kwenye chama kuna shida???kama unakubalika na wananchi wako utachaguliwa tu. Sasa nyie kumbatieni kasumba alafu 2015 tuone kama mtarudi Bungeni.
   
 2. kidi kudi

  kidi kudi JF-Expert Member

  #2
  Jun 14, 2011
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 628
  Likes Received: 157
  Trophy Points: 60
  Nina uhakika ushauri wako mzuri umewafikia waheshimiwa huko mjengoni, and i believe they will take it into consideration. hebu nyie wawakilishi wetu tuwe makini kwa yale tuliyo watuma sisi kama wawakilishi wenu na si kurushiana vijembe visivyo na msaada wowote wa kimaendeleo kwetu.MUNGU IBARIKI TANZANIA.....AMEN!!!!!!!!!!!!
   
 3. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #3
  Jun 14, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  CCM sidhani kama watabadilika mbali na ushauri mzuri uliowapa
   
 4. Kinyungu

  Kinyungu JF-Expert Member

  #4
  Jun 14, 2011
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 4,380
  Likes Received: 3,338
  Trophy Points: 280
  Wabunge wa tz hasa wa ccm ni wanafiki mwanzo mwisho..hawana lolote wapo kama mazuzu tu
   
 5. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #5
  Jun 14, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,401
  Likes Received: 736
  Trophy Points: 280
  jitahidi ugombee 2015 ili upunguze makofi mkuu
   
Loading...