Bunge la Tanzania linawajibika kwa Rais

Kkimondoa

JF-Expert Member
May 31, 2014
4,453
4,933
Ninasema hivyo kwa uhakika kabisa kuwa bunge linawajibika kwa rais

Mf. sheria yeyote ambayo Rais akiitaka ibadilishwe huwa haina kipingamizi ikifika bungeni wabunge hasa wa CCM watapitisha kwa nguvu zote hata kama ni sheria ya kipumbavu na Italitia hasara taifa itapita tu. Na hawana jeuri ya kupinga huu ni ushahidi wa wazi kabisa kwamba bunge linawajibika kwa rais.

WABUNGE WENGI ELIMU KICHWANI HAKUNA HII PIA NI SABABU.

Hili la sheria ya madini hili kwakweli CCM kwa ujinga na elimu ndogo ya wabunge wenu mnalipoteza taifa kabisaa.

CCM Ndio chanzo cha umasikini Tanzania kwa 100% sheria nyingi za hovyo zinapitia mikononi mwao huku wao wakishangilia na kupiga makofi.

HATUNA BUNGE TANZANIA TUNA WALA POSHO.
 
Nakumbuka wabunge wa upinzani walilia Sana wakisema sheria ile inampa mamlaka makubwa Sana Mkulu juu ya rasilimali zetu.... Nadhan kuna siku tutawaelewa hawa wapinzani
wabunge wa ccm hawaja soma na.hawana elimu ni mambumbumbu sana ndio maana nasema tena kwa sauti kuu BUNGE LINAWAJIBIKA KWA RAIS na bunge hili halina maana kabisa
 
Musukuma, Kibajaji lkn pia hata ukiwa umesoma, ukishaingia tu kwenye chama kile unaharibikiwa. Mfano ni maprofesa waliokuwa bungeni wakati wa sheria ya madini ikipitishwa
lakin kungekuwa na wenye elimu kidogo uafadhari ungekuwepo kubwa ya wabunge darasa la saba hatari sana hii, halafu huyo ndio amepewa mamlaka ya kutunga sheria za nchi.
 
Ninasema hivyo kwa uhakika kabisa kuwa bunge linawajibika kwa rais

Mf. sheria yeyote ambayo Rais akiitaka ibadilishwe huwa haina kipingamizi ikifika bungeni wabunge hasa wa CCM watapitisha kwa nguvu zote hata kama ni sheria ya kipumbavu na Italitia hasara taifa itapita tu. Na hawana jeuri ya kupinga huu ni ushahidi wa wazi kabisa kwamba bunge linawajibika kwa rais.

WABUNGE WENGI ELIMU KICHWANI HAKUNA HII PIA NI SABABU.

Hili la sheria ya madini hili kwakweli CCM kwa ujinga na elimu ndogo ya wabunge wenu mnalipoteza taifa kabisaa.

CCM Ndio chanzo cha umasikini Tanzania kwa 100% sheria nyingi za hovyo zinapitia mikononi mwao huku wao wakishangilia na kupiga makofi.

HATUNA BUNGE TANZANIA TUNA WALA POSHO.

Mkuu mimi unanifurahisha sana unavyozidi kujitambua maana ulikuwa uvccm kindakindaki sasa unaikosoa ccm na Serikali yake waziwazi, hongera sana kwa kuitendea haki nchi yako
 
Mada kama hizi huwezi kuona wale pisi wakikatiza,wanapita tu wanasoma kimya kimya
 
Kibajaji yeye ni comedian pale bungeni,ni Mzee wa kuaribu move ambazo zinakuwa na mwelekeo na tija pale bungeni.
 
Ukweli mchungu,siku yoyote utaitwa kwenye kamati ya maadili.
Rais ni mkuu wa serikali na CHAMA ,ukilita fyoko bungeni ana uwezo wa kuamua lolote kwa spika na hata wabunge wanaotokana na chama chake
 
Lkn ukija kwa Msukuma yeye ni mtu mwenye uwezo mkubwa sana wa kuelewa na kumeza kwa mfano km una insue nyeti na ina mashiko, msomeshe msukuma kisha akikisha amekuelewa, basi apo atasimamia na kuitetea mpaka kieleweke, na uyu jamaa na la Saba lake lkn anaelewa mapema sana, juzi tu sakata la waajiriwa wenye darasa la Saba walisimamishwa kazi jamaaa amelisimamia mpaka limeeleweka
Ni tofauti sana na kibajaji.
 
Pamoja na hayo lkn lazima tuwe na katiba itakayohakikisha checks and balance ya mihimili yote mitatu tofauti na sasa ambapo mihimili mingine miwili ni sawa tu na idara za serikali.

Rais akiwa na function fulani, wakuu wa mihimili hiyo mingine huagizwa sambamba na mawaziri kwenda ikulu kuhudhuria! Hiki ni kuwadhalikisha wakuu wa mihimili hii kwani kihaki mihimili yote iko sawa mbele ya sheria.

Na mara nyingi tu bunge hudhibitiwa na serikali na mahakama pia mara kadhaa huingiliwa utendaji wake na serikali hasa kwenye zile kesi za kubumba za kisiasa. Tunahitaji katiba mpya itakayotenganisha mamlaka ya hii mihimili.
 
Pia hili swala la kuunganisha mifuko ya Bima kuna kitu kipo nyuma ya hili hasa kuweza kufahamu total collections balance.......
 
Mkuu mimi ninauliza tu; hivi Bunge "linawajibika" au ulimaanisha "linatumika"?
 
Mkuu mimi ninauliza tu; hivi Bunge "linawajibika" au ulimaanisha "linatumika "?
Bunge la awamu ya tano linatumika na halijawahi kuwajibika sio kama bunge tu bali hata kwa wananchi waliowachagua! Kwa ujumla ni bunge lililosahau au halijui wajibu wake kikatiba! Soma majukumu ya mbunge na kazi zake kama utaona kipengele cha kuisifia serikali na rais! Yaani linafanya mambo ya aibu kiasi kwamba ile heshima waliyokuwa wanapewa mtaani imetoweka! Wajitathmini kabisa kwani hadhi yao imepotea na wanadharaulika mno!
 
Back
Top Bottom