Bunge la Somalia lakubali tume ya kupitia katiba

Bunge la Somalia lakubali tume ya kupitia katiba

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
27,990
Reaction score
63,859
Bunge la Somalia siku ya Alhamisi (tarehe 19 Juni) liliipitisha kamati mpya iliyoteuliwa ya wajumbe watano wa Tume Huru ya Mapitio na Utekelezaji, kwa mujibu wa Waziri wa Habari.

Tume ilipokea kuungwa mkono kukubwa kutoka bungeni, na wabunge 139 walipiga kura ya kuikubali tume, 9 waliikataa, ilhali 10 hawakushiriki.

Tume imepewa kazi ya kupitia Katiba ya Muda ya Shirikisho

"Serikali ya Shirikisho la Somalia inaamini kwamba mchakato wa kutengeneza katiba lazima uongozwe na kumilikiwa na watu wa Somalia, kitu ambacho ni muhimu sana kwa uhalali na mafanikio ya mwisho ya mchakato huo," Waziri wa Sheria na Mambo ya Katiba Farah Sheikh Abdulkadir Mohamed alisema.

"Serikali inaahidi kutekeleza Dira ya 2016, ikiwa ni pamoja na kupitia katiba za muda, utekelezaji wa mfumo wa shirikisho na mchakato wa kidemokrasia ili kufanya uchaguzi hurur na wa haki ifikapo mwaka 2016," alisema.

Chanzo:Sabahi
 
Back
Top Bottom