john agrey
JF-Expert Member
- Jan 24, 2015
- 1,280
- 2,079
Wakati wa bunge la katiba kulijitokeza makundi mawili tanzania kwanza na umoja wa katiba ya wananchi. Haya yalikuwa matokeo ya kile kilichotokea ndani ya bunge na misimamo ya vyama vya siasa, leo hii tunashuhudia demokrasia ikipigwa mateke kwa kisingizio cha hapa kazi tu,wabunge wanatimuliwa bungeni,mikutano ya siasa marufuku na cha kusikitisha ni kwamba hata makongamano sasa ni marufuku. Kitu ambacho viongozi wetu hawa hawajui nu kwamba hiki kitu baadae kitakuja kusumbua utawala, ukawa imeisumbua sana ccm hata kama hawasemi hadharani, leo wapo wanaosema ukawa imekufa lakini bado hawa watu wanashirikiana 90% sio wa kupuuzwa.
Yanayotokea leo hii kwenye mfumo wa vyama vingi ccm waombe zitto na ukawa wasije kuungana na kushirikiana kwenye huu unyonyaji maana sioni mwisho mzuri kwa ccm hii.
Kina Lissu, Mnyika, Mdee, wengi wanawaona kama wamepotea kwenye siasa lakini wanapaswa kutazamwa kwa jicho la tatu, wanazichanga wakirudi kuna upande utatamani vyama vya siasa vifutwe.
Ahsante