Bunge la JMT lifanyie marekebisho Katiba ya NChi ilikupunguza Ma RC kudharau bunge.

Civilian Coin

JF-Expert Member
Dec 2, 2012
2,305
4,379
Salaaam ndugu zangu wapendwa,

Heshima kuu iende kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa siku ya leo napenda kutoa maoni yangu kuwa,

Mawaziri na manaibu Waziri wote wanaapishwa na Rais na wanachaguliwa na Rais na hivyo wanawajibika kwa Rais.

Makatibu Wakuu wa Wizara na Watendaji wengine wa wizara wanateuliwa na Rais na wanaapishwa na Rais na hivyo wanawajibika kwa Rais.

Wakuu wa Mikoa wote wanateuliwa na Rais na wanaapishwa na Rais na hivyo wanawajibika kwa Rais.

Mtengano huu ndio unaofanya Wakuu wa Mikoa kuweza kulidharau bunge letu tukufu.

Lakini cha kushangaza Wakuu wa Wilaya wanateuliwa na Rais lakini wanaapishwa na Wakuu wa Mkioa kwa niaba ya Rais.

Natamani siku moja niwe Waziri wa Mambo ya Ndani iliniisafishe NChi kuondokana na upuuzi huu wa kulidharau bunge na mahakama. Mwisho wa siku tutajikuta tunaingia kwenye Vita ya sisi kwa sisi bila kujijua.

Mamlaka yana mipaka yake hata kama umeteuliwa na Rais.

Deogratius Nalimi Kisandu
Mtemi Kiongozi wa Chama cha ACA tarajiwa.
5 Januari 2017.
 
Bro kwa hili nakubaliana na wewe 100%. Kila mhimili uwe na heshima kwa mhimili mwingine. Inapotokea mtendaji kutoka mhimili mmoja kudharau mhimili mwingine Katiba na Sheria za Nchi zieleze bayana hatua za kuchukua tena kwa haraka bila kusubuiri hisani ya mamlaka ya uteuzi. Mgawanyo wa madaraka kati ya mihimili ya nchi ni muhimu sio tu kwa usalama wa nchi bali pia kwa utangamano wa kitaifa.
 
Ili tufike tunahitaji uelewa.
 
Sikutegemea unaweza kumwaga point kiasi hiki. Endelea hivyohivyo utapata wafuasi wa chama chako.
 
dawa ya aliyelaaniwa ni kuombewa tu...angalao akutane na huruma ya MUNGU abadilike.
 
Mkuu wabunge wa siku hizi wanadharaulika na watu wengi kwa kuwa ni vilaz.
Hilo halijalishi ni rc, dc, machinga au muuza vitunguu kule matombo!
 
Kwahiyo wasiambiwe ukweli kisa wao ni wabunge? Watu wanashinda wanalala na wakiwa macho wanatetea wauza unga... mnataka tukae kimya
 
Back
Top Bottom