Bunge la ccm ni leo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bunge la ccm ni leo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mzee wa inshu, Feb 8, 2011.

 1. m

  mzee wa inshu Member

  #1
  Feb 8, 2011
  Joined: Jan 25, 2011
  Messages: 49
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Bunge la jamuhuri ya muungano wa tanzania likiwa linatarajiwa kuanza leo, bado kuna utata kutokana na kuacha maswali mengi yasiyo na majibu.

  Nathubutu kuliita bunge la ccm kutokana na ukweli kwamba hoja zenye nguvu ambazo zimetokea kuwagusa sana watanzania walio makini na wenye mapenzi na nchi yao tayari zimetupwa kapuni.

  Nilitarajia hoja kama ya Katiba na Dowans zingepewa kipaumbele cha kwanza kutokana na ukweli kwamba hali ya nchi ambayo inayumbayumba kwa sasa ni kutokana miongoni mwa mambo hayo mawili, hivo ingelikuwa mahali sawia kwa serikali kutoa mapendekezo yake lakini pia kupokea mapendekezo mbali mbali kutoka kwa wabunge wa kambi ya upinzani na chama tawala ili kuona namna ya kufikia suluhu ya matatizo haya.

  Hii ni dhahiri kuwa serikai haina uwazi, badala yake inafanya madudu mengi gizani na kuwatwika watanzania mizigo mizito mambo yakisha haribika.

  Lazima tujue kuwa hapa sio bure, lazima pana mambo ya gizani ambayo serikali kwa vyovyote vile serikali haingependa yawekwe kwenye mwanga na kuiumbua mbele tya macho ya watanzania ikifahamu fika kuwa hatua hiyo siajabu ikapelekea yale ambayo yanatokea Tunisia na Misri.

  Niwazi kabisa serikali ya ccm haipo kutetea masilahi ya wananchi bali kulindsa masilahi ya mafisadi ambao wanaliangamiza taifa kwakutumia jasho na damu za watanzania wenzao bila hata chembe ya huruma.

  Ikumbukwe kwamba watanzania wa leo nitofauti sana na wa miaka ile! Kizazi hikina masikio ya kusikia, kina macho ya kuona na midomo ya kuongea na mioyo yakufikiri na kutafakari.

  Tukumbuke kuwa haya ytote yana mwisho wake!

  I cry for my coutry, I cry for my people!
   
Loading...