Bunge la budget 2012/2013 na kauli hizi..! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bunge la budget 2012/2013 na kauli hizi..!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BJEVI, Jul 10, 2012.

 1. BJEVI

  BJEVI JF-Expert Member

  #1
  Jul 10, 2012
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 1,360
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  [FONT=&quot]WADAU HEBU PIMENI MANENO HAYA NA MWIITIKIO WA JAMII.

  1.LIWALO NA LIWE-Mh.waziri mkuu.-Jamii bado ina mtazamo hasi kwani kauli hii ilitolewa wakati mgomo wa madaktari unaendela pia kutekwa na kuumizwa vibaya kwa DK.ulimboka ---kauli hii haikukubalika na hata sasa ipo midomoni kwa wanajamii wengi.Na kwa taarifa tu imefanya jamii ioneshe dharau kwa watawala hasa mtoaji wa kauli hii....habari ndo hiyo....dadisi ujue nisemalo......

  2.MWENYE UCHUNGU AKAZAE-Mh.said -mbunge wa sikonge---Kauli hii ilizua mambo mengi kwenye jamii hata ya kumfananisha mropokaji sawa na mchawi....kama huamini fuatilia....Ni kauli yenye mtazamo usiyokizana na maadili na utamaduni wa mtanzania ,hata sasa kauli hii imechukuwa sura tofauti miongoni mwa wananchi wa kada mbalimbali wasomi na wasio wasomi.Ni kauli maudhui tata wanasema wenyewe raia.....

  3.DHAIFU-MH.J.J MNYIKA-MBUNGE WA UBUNGO-KAULI hii ilishika kasi ,ilizua mengi,ilianika uozo wa kila aina ndani ya serikali ya JK.NA HATA SASA hili neno linaendelea kutumika na lina mitazamo yote miwili hasi na chanya.Na kwa taarifa za chini ya capeti aliyetoa kauli hii amepanda chati kwa kiasi fulani kwenye medani za siasa za bongo.Na anaendelea kupata umaarufu kadri siku zinavyohesabika-huwezi amini na si ushabiki lakini wataalamu wa uchambuzi wa mambo mbalimbali ndani ya jamii watakualiana nami kwani kauli hii imebeba dhana nzima ya uwajibikaji wa serikali iliyopo madarakani....dadisi ujue nisemalo......

  4.HITLER-MH.STELLA MANYANYA-MBUNGE NA MKUU WA MKOA WA RUKWA...Ni kauli iliyotolewa wakati watanzania wengi wenye hamu ya kuona haki ikitendeka hasa kuhusiana na unyama aliofanyiwa DK.ULIMBOKA...Ni kauli isiyozingatia maadili,ina walakini na uteuzi wa viongozi wetu,ina mtazamo hasi kabisa ndani ya jamii hata sasa inajadiliwa mno mno mno mno mno na hata kumfananisha mtoaji wa kauli hii na mlevi ndani ya kanisa au msikiti.Huwezi amini ingia ndani ya jamii.....dadisi ujue nisemalo......

  UNAWASHWAWASHWA.--Mh.silvester malumbo-mwenyekiti wa BUNGE-Imefananishwa na kauli zinazotolewa na watu walevi,watu wenye jazba,waliyokosa hoja ,wasio na hekima,wasiyojua dhana nzima ya kuwa kiongozi,wasiyojali hadhira wala mandhari ya kutoa kauli kama hizi,WATU WENYE TABIA ZA UDIKTETA,wasiopenda kukosolewa,watu wenye nidhamu za uoga na mengine yanayofanana na hayo....Ina mtazamo hasi ndani ya jamii hata imefikia wanajamii kutaka kujua viongozi wa bunge huwa wanapatikana vipi....Imepelekea kumkumbuka MH.SITA -THE EX-SPIKER.Amini usiamini habari ndo hiyo ndani ya jamii...dadisi ujue nisemalo......

  INGAWA KUNA WENGI WAMEFUNGUKA NA KUYAELEWA MENGI KUHUSU VIONGOZI WETU BAADA YA KAULI HIZI.BADO WAPO NJIA PANDA KWAMBA ,NANI ALAUMIWE KWA KAULI KAMA HIZI?.JE! ZINAENDANA NA MAADILI YA MTU ANAYEIWAKILISHA JAMII KWENYE VYOMBO VYA MAAMUZI KAMA BUNGE?

  [/FONT]
   
Loading...