Bunge la bajeti ni mfano hai wa jinsi ambavyo bunge hili haliwezi kuiwajibisha serikali.

DaudiAiko

JF-Expert Member
Dec 2, 2012
302
274
Wanabodi,

Hivi karibuni, bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania lilipitisha bajeti ya waziri mkuu baada ya vikao kadhaa. Majadiliano yali husisha changamoto mbali mbali zilizopo kwenye majimbo ya wabunge na yalifanywa kwa matumaini ya kwamba mbeleni, serikali itaweza kutatua changamoto hizo.

Walio fanikiwa kushuhudia vikao hivi watakubaliana na mimi nikisema kwamba matumizi ya waziri mkuu haya kujadiliwa. Kilicho tokea ni mijadala ya mambo mengi ambayo hayakuwa na uhusiano wa moja kwa moja na fedha zilizopangwa kutumiwa na ofisi ya waziri mkuu kwa mwaka 2022/2023. Unaweza kusema kwamba ilimradi fedha zinapelekwa sehemu husika na kuwa saidia wananchi bila serikali kupata hasara, basi hamna haja sana kwa wabunge kushiriki kikamilifu kwa kutoa maoni ambayo yanaweza kuboresha bajeti iliyopo. Fikra hizo zina batilisha kabisa zoezi la demokrasia na haja ya wananchi kuwa na matumaini na viongozi walio chaguliwa pamoja na kutotilia maanani gharahama ya kuendesha bunge kwa serikali.

Swali la kujiuliza ni "Je matumizi ya serikali yanapangwa na nani?, matumizi haya yanapitia mchakato upi kabla ya kuwasilishwa bungeni?. Je kupitishwa kwa bajeti bungeni ni suala ambalo ni "ceremonial?"
 
Hiki ndio kikao ambacho Jesca Msambatavangu anazungumzia mambo ya wanaume hawapendwi sura?
 
TANZANIA HAKUNA BUNGE KUNA WAJUMBE WA CHAMA TAWALA NDANI YA JENGO LA BUNGE
HUWEZI KUSEMA UNA BUNGE WAKATI HUNA KAMBI RASMI YA UPINZANI HUNA KIONGOZI WA KAMBI HUNA MBADHIMU WA KAMBI HUNA MAWAZIRI VIVULI WA KAMBI HUNA HUTUBA YA KAMBI HUNA HOTUBA ZA MAWAZIRI VIVULI
 
Sidhani kama kuwa na kambi rasmi ya upinzani ingesaidia sana. Kinacho hitajika ni utundu kidogo wa wabunge kufatilia matumizi ya serikali kwa kina au serikali kuwapa taarifa hizo.
 
Back
Top Bottom