Kikao cha bunge kinachoendelea mjini Dodoma kimekuwa ni sumu kwa CHADEMA kwa vile wananchi wamepata fursa adimu ya kuwaelewa aina ya viongozi na chama kwa ujumla kilivyo. Wabunge wa CHADEMA wamekuwa mashuhuri kwa kuibua hoja zisizo na mshiko kwa wapiga kura na taifa kwa ujumla hivyo wananchi wamepata nafasi ya kuwajua kiundani viongozi wa CHADEMA wasivyo na uelewa na ufahamu wa kuongoza nchi. Mbowe akiwa ni Kiongozi Mkuu wa Upinzani Bungeni amezidi kupoteza umaarufu kutokana na tabia za yake ya kuwaachia wabunge wasio na haiba ya uongozi kama vile Sugu, Wenje na Msigwa kuandaa na kusoma hotuba zisizo na manufaa kwa taifa. Yote kwa yote kikao cha bunge kimekuwa ni KABURI la CHADEMA kwa vile watanzania wamepata nafasi ya kuwachambua viongozi wa CHADEMA.
Nimefanya utafiti mikoa ya Lindi, Mtwara, Pwani na Tanga nimegundua wananchi kwa kupitia bunge wamejiridhisha kuwa chama cha CHADEMA hakina sifa ya kuongoza nchi kwa sababu viongozi wake ni vinara wa fujo na kuleta uchochezi wenye dalili ya kuharibu AMANI nchi mwetu iliyojengwa kwa zaidi ya miaka 50.
Wanazi wa CHADEMA pokeeni hoja hii pasipo matusi ili chama chenu kibadilike kwa manufaa ya nchi yetu
Ni nchi hii peke yake ambapo ukiwa mpumbavu unakuwa shujaa. Ni ukweli usiopingika ni kazi ya upinzani kutoa mawazo mbadala namna ya kuendesha serikali. Lakini sasa badala ya kuyachukua CCM ambacho ni chama tawala mmekuwa mabingwa wa kupinga kila kinachosemwa na upinzani. Kiufupi CCM ni "
chama cha upinzani wa wapinzani" na bila aibu mwenyekiti wa CCM alimsifia na kumpandisha cheo Mh MWIGULU kwa kuchana bajeti ya upinzani. Mko very busy kukosoa yanayofanywa na upinzani badala ya kuelekeza nguvu zenu kwenye kuelezea malengo yenu, ilani yenu na kuchapa kazi. Mmejisahau kuwa nyie ni chama tawala na mna wajibu mkubwa wa kuonyesha njia na upinzani upo kwa ajili ya kuwakosoa pale mnapokosea.
Kila mmoja ana wajibu wake na ndio maana mnakula kodi zetu na hatutegemei kuwa na mpinzani ambaye ana kaa tuu na kusema sawa mzee, huyo hile ni jasho letu na tunafurahi pale mnaposhikana mashati kutetea ya kwetu. na hii ndio mfumo wa vyama vingi.
CCM mna ndoto za chama kushika hatamu na mnatamani sana mbaki wenyewe bila ya upinzaini. HIZI NDOTO NI ZA ALINACHA.. UPINZANI IS THERE TO STAY... SUCK IT.
Mabunge ya wenzetu wanfikia hadi kuzichapa live, sisi bado tunaremba sanaaa.. KWA TANZANIA YA SASA HAKUNA MWANANCHI MLALA HOI ASIYEJUA MAANA YA KUWA NA MFUMO IMARA WA VYAMA VINGI.. NA WENGI WETU TUKA DETERMINE KUHAKIKISHA UCHAGUZI UJAO TUNAKUWA NA WABUNGE WANGI WA UPINZANI ILI DHARAU NA KEJELI NA KUPITISHA MAAMUZI KWA KURA ZA NDIOOOOOO IWE NDIO MWISHO WAKE. WAPO WABUNGE WENGI WA CCM WASIOPENDEZWA NA JINSI BUNGE LINAVYOENDESHWA.. NA WANAWASAIDIA SANAA HAO CHADEMA KUPATA UMAARUFU.. NDIO MAANA KILA KUKICHA HATA HUMU jf WANACCM MKO BUSY KUANZISHA THREAD ZA KUIDIDIMIZA CDM BADALA YA KUANZISHA THREAD ZA KUIINUA CCM.
Mnachosahau hata dada yako ukimkataza sana na kumwambia usiongea na yule mwanaume ni malaya, mhuni, mvuta bangi, mfanya fujo... mwisho wa siku utastaajabu pale utakapogundua jamaa anamega tunda kiulaini.
USHAURI- ANDIKENI MAKALA NYINGI ZA KUINYANYUA CCM ZAIDI, NA POTEZENI MUDA WENU MWINGI KUONGELEA CCM. CHA AJABU HATA VIONGOZI WA KITAIFA MIDOMONI IMEWAJAA CDM ZAIDI YA CCM. NYIMBO ZAO ZOTE NI CHADEMA, CHADEMA, CHADEMA, CHADEMA, CHADEMA, CHADEMA, CHADEMA....