Bunge la 10 kuamua hatma ya nchi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bunge la 10 kuamua hatma ya nchi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Yona F. Maro, Jan 30, 2011.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Jan 30, 2011
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Siku 3 zilizopita nilikuwa na safari kwenda sehemu moja nchini , nilipomweleza rafiki yangu mmoja kuhusu safari hiyo mara moja akaniambia kama naenda nihakikishe sikai mwanza muda mrefu siku hiyo na wakati narudi nisipite njia ya singida arusha moshi kwasababu maeneo ya huko wananchi hawatabiriki kwa sasa .

  Ingawa tuliharibikiwa na chombo kushindwa kwenda mahala Fulani kama mwanza , baada ya siku 1 mtu mmoja akanipigia simu kuniambia kinachoendelea huko na siku hiyo hiyo jioni yake ningepita babati pengine ningekutana na wale wananchi wenye hasira waliochoma moto mali kwenye mji huo .

  Hii ndio hali ya nchi kwa sasa hivi zamani tulizoea maandamano kuanzia kwenye miji mikubwa kama Dar es salaam , lakini leo hii tunaona maandamano na fujo zinatokea sehemu za vijijini kama Babati ambapo FFU kufika ni Taabu sana kwanza barabara na miundombinu mengine ni mibovu , Tunaongelea Huko mbeya vijijini kwenye mipaka ya nchi yetu wiki 2 zilizopita fujo zimetokea tena .

  Matukio hayo hapo juu yaliyotokea vijijini ni sawa na ile ya Tunisia tu kwa sababu yule kijana aliyejichoma moto , wananchi walioanzisha maandamano walitokea vijijni kwa njia mbalimbali mpaka kufika mji mkuu na kufanya kile walichokifanya na wengine kuendelea kumiminika kushinikiza mabadiliko ya uongozi mpaka sasa .
  Kwakuwa matukio haya yametokea wakati bunge la 10 ndio kwanza linaanza , binafsi nafikiri bunge hili linaweza kuzaa mabadiliko Fulani nchini , mabadiliko hayo hakuna anayeyajua labda mimi au wewe , lakini unapoona Gunia la Sukari kupanda toka shilingi alfu 60 mpaka 70 ndani ya wiki moja na mwananchi hawezi tena kwenda kununua sukari ujue kuna jambo , unapoona Euro ya ulaya imepanda ghafla ndani ya wiki moja toka 1997 mpaka 2045 ujue kuna shida .

  Na unapoona Askari mlinda nchi mshahara wake umekatwa bila sababu za msingi ujue kuna jambo linatakiwa nalo ni mabadiliko ambayo Mwanzo wake inaweza kuwa Bunge la 10 .
   
 2. Mupirocin

  Mupirocin JF-Expert Member

  #2
  Jan 30, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,596
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Mi nafikiri tuwaache wananchi wa vijijin waanze kwani toka zamani mabadiliko yanaanzia pembezoni kuliko mijini. Mi napenda maandamano yaanze hata sasa tumtoe jk.
   
 3. Shidende

  Shidende Member

  #3
  Jan 30, 2011
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Spirit ya maandamano inaambukizwa ndio maana unaona leo hapa wana andamana kesho kule wanaandamana! lakini na UTAWALA UNACHANGIA KIASI KIKUBWA WATAWALIWA KUCHOKA..
  Naomba kuwasilisha
   
 4. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #4
  Jan 30, 2011
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kichwa cha habari hakifanani na habari yenyewe ndugu yangu!Kwa nini umeandika hivi,mbona threads JF hazina price tag?
   
Loading...