Bunge kuzuia kurusha matangazo halitendi haki kwa watanzania

mwembemdogo

JF-Expert Member
Feb 28, 2016
2,282
1,252
Nimeshangazwa Na msimamo wa Bunge letu kuendelea kugomea vyombo vya habari Televisheni kurusha matangazo ya Bunge.

Wananchi ndio tuliowachagua hao wabunge Na ni sisi wananchi tunaotakiwa kujua wanafanya nini ndani ya Bunge. Kuzuia kurusha matangazo Spika anaficha nini ambacho anataka sisi tuliowapa dhamana tusikijue? Mbona Serikali hii inajinadi kuwa ni ya uwazi?Mbona Mawaziri wanadiriki mpaka kusafiri Na waandishi wa habari katika ziara zao ili wasikike iweje Bunge lizuie?

Tunaliomba Bunge liruhusu vituo vya Televisheni viruhusiwe kurusha shughuli za Bunge wakati wote wa Vikao.
 
Asilimia 80 ya habari za nchi hii zinatengenezwa na serikali...
. cc. Nape Nnauye ????
 
yaani uhuru na haki ya kupata habari kwa watanzania iko mashakani sana kwa sasa. yaani wako tayari TBC ashinde anaonyesha taarabu na filamu za kenya ila siyo Bunge. hii inaweza kutokea tanzania tu
 
Back
Top Bottom