Bunge kuwaka moto, wabunge wa CCM wala yamini, hoja zote za UKAWA kudhibitiwa

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
12647198_1029489773782147_8868677829432439358_n.jpg
 
Swala la Zanzibar peke yake litawaenyesha wabunge wa ccm achilia mbali agenda zingine
 
kama wamejiandaa kupinga hoja zote za upinzani ina maana wabunge wa ccm watakuwa wakushangaza sana maana wamejiandaa kupinga bila kujali hoja. na hapo mtakumbuka tulivyosema sisi kina gogo la shamba kwamba ccm ni ileile na kuwarejesha ccm madarakani ni kuongeza umaskini nchini
 
...inaeleweka...labda kushirikisha ktk nukta za kuzingatia, ni ukweli kwamba kimahesabu, jambo lolote ambalo ni la CCM, bila kujali limewasilishwa na nani bungeni,ndilo litakalopitishwa na bunge, na jambo, na hoja yoyote ambayo si ya CCM, hata kama litawakilishwa na mbunge wa CCM, hilo halitapitishwa.....
 
Ni kukosa uelewa mpana wa maana na malengo ya upinzani , maana siasa za tz zimekaa kishabiki shabiki tu kiasi kwamba zinatuchelewesha kusonga mbele , hivi unapokula yamini kudhibuti hoja za upinzani ndio kusema ccm peke yao ndio wana akili sana ? Nionavyo mimi wakitaka kuwapaisha wapinzani basi waendelee na ushabiki wa kusemaa ndioo hata kwenye hoja zenye maslahi na chama. Ukitaka mpinzani wako aishiwe hoja mpe nafasi ya kusema kisha fanyia kazi . Tanzania ya sahv ni waelewa wanajua kupima pumba na mchele . Nawapeni tahadhari ccm muondoe ushabiki mtachemka
 
Don't insult our intelligence Hilo rag inaweza kuwa chanzo cha habari?
 
Yuko wapi Werema aliyeita wenzake Tumbili? Maccm Kuban hoja za wapinzani si kwamba wameanza Leo,watabana lkn penye ukweli wataachia.Na jimbon tumewasubilia
 
Huu ni upuuzi kwa watu waliofilisika kisiasa! Kma CCM nia yao ni kwenda kupinga kila kitakachowasilishwa na upinzani ni sawa na kujichimbia kaburi na kumhujumu Rais Magufuli, Rais peke yake hawezi kuyajua majipu ya nchi hii lazima apate mawazo mbadala ya ushauri kutoka bungeni! Wengi wa wabunge wa CCM ni wanafki hawawezi kuibua mambo mazito zaidi ya kulala tu bungeni na kuisifia serikali tu.Sidhani hili jambo kama litampendeza hata Rais japo Ndungai anaonekana kukaa kichama zaidi.
 
Hapa ndipo ninapopata shida na hii nchi. Kwani bungeni ni majukwaa ya siasa au? Kwanini wasishikamane bungeni ili kuweza kuisimamia serikali kwa pamoja? yaani hapo wapinzani ndo wasimamizi alafu ccm wote ni serikali. Dah! Inaniuma kuona nchi yangu bado tatizo la bunge halijatatuka
 
Ccm kinatumia nguvu ya dola lakini kiuhalisia ni Chama mtu, chama hai hakijiandai kupinga mawazo hai ya upinzani Badala yake kinajiandaa kupokea mawazo ili kifanikiwe kuendesha nchi Kwa mafanikio ili kiendelee kukubalika zaidi
 
kama wamejiandaa kupinga hoja zote za upinzani ina maana wabunge wa ccm watakuwa wakushangaza sana maana wamejiandaa kupinga bila kujali hoja. na hapo mtakumbuka tulivyosema sisi kina gogo la shamba kwamba ccm ni ileile na kuwarejesha ccm madarakani ni kuongeza umaskini nchini
Hii ni sala tosha.....ameen
 
Kwa hiyo serikali ya Magufuli ni dhaifu haiwezi kujitetea mpaka wabunge wao waache kutimiza kazi waliyotumwa na wananchi na kufanya kazi ya kutetea mawaziri ambao kumbe ni mizigo
 
Wabunge wa Ccm ni sehemu ya serikali, kwahiyo wapo bungeni kwa ajili ya kuitetea serikali na sio kuisimamia. Na ndiyo maana utamsikia mbunge wa Ccm anaitetea serikali juu ya hoja iliyopo mezani kwa kuunga mkono hoja kwa asilimia mia halafu mwishoni ndipo anapo anza kulialia.
Utaratibu ambao Ccm imejiwekea kwa miaka mingi sasa ni kuwa endapo unefanikiwa kuupata ubunge basi wewe lazima uwe mstari wa mbele kutetea chama na serikali. Tofauti na hapo jua kwamba kipindi cha uchaguzi mkuu hasa kwenye mchakato wa kura za maoni za kumpata mgombea ndani ya chama juwa kwamba huna chako.

Hiyo ndiyo CCM chama dola, bila dola hakuna CCM.
 
Back
Top Bottom